Alichofanya Abacha kwa Ken Saro Wiwa ndicho anachofanya Samia kwa Tundu Lissu. Wanigeria waliona sawa enzi zile leo ni kitovu cha Ugaidi na Ufisadi.

Alichofanya Abacha kwa Ken Saro Wiwa ndicho anachofanya Samia kwa Tundu Lissu. Wanigeria waliona sawa enzi zile leo ni kitovu cha Ugaidi na Ufisadi.

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,494
Reaction score
57,869
Hakuna jipya chini ya jua.

Huu ni msemo maarufu sana unaomaanisha hakuna kitu kinachofanyika leo duniani kwenye maisha ya kawaida ya binadamu ambacho ni kipya.

Miaka ya 1990- 1997 nchini Nigeria alitokea Dikteta maarufu sana Duniani aliyejulikana kama Generali Sani Abacha. Kiongozi huyu wa mwisho wa Kijeshi katika taifa la Nigeria ndiye chanzo cha Nigeria tunayoiona leo yenye Ufisadi wa kutisha pamoja na vikundi vya Kigaidi ikiwemo Boko Haram pamoja na vikundi vya Utekaji vinavyoteka watu ili kupata fedha.

Miaka ya 1980- 1995 alitokea Mwanaharakati Maarufu sana Nchini Nigeria aliyejulikana kwa jina la Ken Saro Wiwa. Mwanaharakati huyu alikuwa anatetea haki za watu wa Nigeria ikiwemo jimbo lake la River State kunufaika kweli na rasilimali za Mafuta na Gesi zilizopo nchini mwao.

Kwa kuwa Mwanaharakati huyu alikuwa vocal sana, Serikali ya Sani Abacha ilimkamata, kumuweka Gerezani na baadae kumnyonga. Ken Saro Wiwa alinyongwa rasmi mwaka 1995.

Kunyongwa kwa Ken Saro Wiwa kulikuwa kama laana kuu kwa Sani Abacha na Nigeria kwa ujumla. Sani Abacha alifariki kwa ugonjwa wa shinikizo la Damu mwaka 1998 na tangu hapo Vikaibuka vikundi vya watu wenye silaha walioamua kudai madai ya Ken Saro Wiwa kwa njia ya Silaha na vingine kuanza kutumia silaha ili kupata mkate na kuendesha maisha.

Vikundi hivyo vya watu wenye silaha vilikuja kukua hadi kuzalisha vikundi vya kigaidi, Uhalifu wa Silaha na Utekaji tunavyoviona leo wakiwemo hawa Boko Haram.

Kuzimwa kwa Ken Saro Wiwa ndipo kumefanya leo Nigeria kuongoza kwa Ufisadi Afrika. Leo hii duniani kote Wanigeria wanafahamika kwa matukio ya wizi na Ufisadi.

Alichofanyiwa Ken Saro Wiwa ndicho anachofanyiwa sasa Tundu Lissu. Wote wana sifa moja. Ni wanaharakati wa kisiasa wanaopigania mageuzi ya kweli yanayotaka mifumo imara ya nchi inayohakikisha Wananchi wananufaika na Haki pamoja na rasilimali za taifa lao.

Wakati Tundu Lissu anapigana Tanzania ipate mifumo safi itakayozuia Ufisadi na kuhakikisha rasilimali za Taifa haziwanufaishi watu wachache, CCM wanapigana kumkandamiza Lissu ili wao waendelee kula keki ya Taifa bila bugudha huku Wananchi wengi wakiendelea kuwa na umasikini wa kutisha.

Wakati Tundu Lissu anapigana kuwe na mifumo ya uwajibikaji na uwazi ili kuhakikisha Ufisadi hautamalaki na wananchi wanapata Viongozi sahihi watakaoweza kuwawajibisha, CCM wanaanzisha vikundi vya utekaji ili kunyamazisha watu wote wanaoongea na kupinga maovu.

Hakuna tofauti yeyote kati ya namna Abacha alivyomfanyia Ken Saro Wiwa na namna Samia na CCM wanavyomfanyia Tundu Lissu.

Historia haijawahi kuongopa, kwa yanayoendelea Tanzania sasa, muda si mrefu tutakuwa rasmi kama Nigeria. Vikundi vya Utekaji na Uhalifu wa kutumia silaha vitapata nguvu na kuwa vikundi rasmi na Ufisadi utakuwa alama ya Utambulisho wa Taifa huku umasikini ukitamalaki kila kona kwa Wananchi wengi.
Screenshot_20250618_114438_Chrome.jpg
 
Hii ni cycle mbaya sana ya historia inayojirudia, Ken Saro Wiwa aliuawa kwa kusema ukweli, now Tundu Lissu anatishiwa kwa sababu anasimama kwenye haki na uwazi. Tanzania ikiwa haitaacha vurugu na ufisadi kuendelea, tutakuwa kama Nigeria, where corruption and kidnappings become the norm. Ni lazima tuchukue hatua, before it’s too late.
 
Hii ni cycle mbaya sana ya historia inayojirudia, Ken Saro Wiwa aliuawa kwa kusema ukweli, now Tundu Lissu anatishiwa kwa sababu anasimama kwenye haki na uwazi. Tanzania ikiwa haitaacha vurugu na ufisadi kuendelea, tutakuwa kama Nigeria, where corruption and kidnappings become the norm. Ni lazima tuchukue hatua, before it’s too late.
Hakuna mwenye akili huko TISS na JWTZ anayeweza kuona haya. Wote wapo kwenye upofu wa uchawa kwa CCM. Wanaona wameyamaliza maisha lwa visenti wanavyopata kuwasezesha kustarehe, kujenga vinyumba na kununua mashamba bila kusahau kula wanawake wazuri.

Hawajui wanayofumbia macho saivi soon yanaenda kuwatokea puani.
 
Taarifa za Tundu Lissu kuwekewa sumu huko Gerezani zinaenda kuhitimisha usahihi wa huu uzi.
 
Back
Top Bottom