Alibakari live interview on DJ sepetu show!!

Alibakari live interview on DJ sepetu show!!

Naam, swali zuri[emoji4] [emoji4] kuna kipindi nilikuwa nasoma, fani niliyokuwa nasomea ndio ilinilazimu kufanya utafiti, kwahiyo katika utafiti nilokuwa nafanya ilinilazimu nitumie njia mbali mbali kwa lengo la kupata taarifa sahihi. Baada ya kumaliza, nilifuta mpaka account. Sikuwa lengo baya nao.
Nimekuelewa vizuri kabisa Mkuu
 
Hapana kwa kweli kwani " Wema hauozi, ubaya hausahauliki na Mlipaji hafi"
Mzee umesoma madrasa sana sio kwa mwandiko huu ingawa bado siamini kama utaipotezea hiyo hela maana TV ngapi itakubidi kutengeneza kukusanya huo mkwanja!

Tunaendelea una dada zako nyumbani!?
Je uliwasaidia vipi kufikia hapo kama wameolewa kimalezi na kifedha!
 
Sawa! Je ukipewa million 200 na mchepuko umpige bao moja_ sorry!
Utakubali?wakati mkeo akiwa chumbani amelala wewe sebuleni!
Vile vile bahati nzuri sina tamaa ya fedha na naridhika na ninachokipata. Mwaka 2005, nakumbuka baada ya kumaliza shule, bi Mkubwa wangu siku moja aliingia chumbani mwangu bila mimi kujua na kuweka kwenye kabati langu la nguo begi dogo jeusi, lililokuwa na nembo iliyosomeka "Sport" mimi nilipoliona sikuwa na wasiwasi kuwa labda kuna kitu kibaya (silaha au mali ya wizi) imefichwa chumbani mwangu. Chumbani mwangu nilikuwa naingia na marafiki zangu ambao nao ni waaminifu. Hakuna hata rafiki yangu mmoja aliewahi kupekua.
Baada ya miezi miwili bi Mkubwa akaniambia nimpelekee lile begi sebuleni na nimsaidie kuhesabu. Nilihesabu zilikuwa Tsh 60milioni. Na sijaiba/wala kuibiwa hata thumni.
 
Mzee umesoma madrasa sana sio kwa mwandiko huu ingawa bado siamini kama utaipotezea hiyo hela maana TV ngapi itakubidi kutengeneza kukusanya huo mkwanja!

Tunaendelea una dada zako nyumbani!?
Je uliwasaidia vipi kufikia hapo kama wameolewa kimalezi na kifedha!

Ni kweli nilisoma sana madrasa
المدرست المعمور
Wadada ninao lakini bahati nzuri wao ni wakubwa kwangu, hivyo wao ndio walinilea, na bahati nzuri wote walikwisha olewa.
 
Mkuu alibakari unafikiri ni mambo gani makuu ambayo yanafanya vijana (hasa wakitanzia) wasiweze kujikwamua kimaisha.
Kufanya mambo kuzidi uwezo au kipato na vile vile kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja tena yanayokinzana yanarudisha nyuma. Mfano mzuri mtu unakuta yupo kwenye kutafuta lakini bado anaendekeza na starehe, hapo kwa akili yake anaona sawa lakini kwasisi twenye mtazamo tofauti hayuko sawa.

Tafuta kwanza starehe baadae
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom