Alibakari live interview on DJ sepetu show!!

Alibakari live interview on DJ sepetu show!!

Vile vile bahati nzuri sina tamaa ya fedha na naridhika na ninachokipata. Mwaka 2005, nakumbuka baada ya kumaliza shule, bi Mkubwa wangu siku moja aliingia chumbani mwangu bila mimi kujua na kuweka kwenye kabati langu la nguo begi dogo jeusi, lililokuwa na nembo iliyosomeka "Sport" mimi nilipoliona sikuwa na wasiwasi kuwa labda kuna kitu kibaya (silaha au mali ya wizi) imefichwa chumbani mwangu. Chumbani mwangu nilikuwa naingia na marafiki zangu ambao nao ni waaminifu. Hakuna hata rafiki yangu mmoja aliewahi kupekua.
Baada ya miezi miwili bi Mkubwa akaniambia nimpelekee lile begi sebuleni na nimsaidie kuhesabu. Nilihesabu zilikuwa Tsh 60milioni. Na sijaiba/wala kuibiwa hata thumni.
Mkuu naona kama unapoteza muda kutengeneza TV!! Kwanini usimuombe bi mkubwa mtaji unafanya biashara maana kama 60millions zilikuwa ktk begi vp benk!?
Au hauna skills za ujasiriamali?
 
Kufanya mambo kuzidi uwezo au kipato na vile vile kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja tena yanayokinzana yanarudisha nyuma. Mfano mzuri mtu unakuta yupo kwenye kutafuta lakini bado anaendekeza na starehe, hapo kwa akili yake anaona sawa lakini kwasisi twenye mtazamo tofauti hayuko sawa.

Tafuta kwanza starehe baadae
Nimekuelewa vizuri kabisa;
 
Mpaka umri uliofikia kwasasa ni vitu gani umejifunza kutoka kwa binadamu na maisha kwa ujumla?
 
Mkuu naona kama unapoteza muda kutengeneza TV!! Kwanini usimuombe bi mkubwa mtaji unafanya biashara maana kama 60millions zilikuwa ktk begi vp benk!?
Au hauna skills za ujasiriamali?
Niko vizuri kiasi kwani kuna kipindi niliwahi kupewa mtaji mdogo na mmoja kati ya madada zangu, nilifanya vizuri, nilikuza na mtaji lakini ilinilazimu niache ili kuendelea na masomo.
 
Niko vizuri kiasi kwani kuna kipindi niliwahi kupewa mtaji mdogo na mmoja kati ya madada zangu, nilifanya vizuri, nilikuza na mtaji lakini ilinilazimu niache ili kuendelea na masomo.
Ulishawahi onana live nahuyo mrembo Wa jf vipi muonekano wake ulivutiwa na nini zaidi!
Ushawahi mtumia M-PESA ama tigopesa?alikuomba?
 
Nimekuelewa vizuri kabisa;
Nimejifunza mengi sana miongoni mwa hayo ni
1. Usimdharau usiemjua
2. Msaidie mwenye kukuomba msaada
3. Ulimwengu huu huwezi kumridhisha kila mtu
4. Usimtuaini binadamu mwenzio
5. Simamia unaloamini kwenye kutafuta
6. Kama kweli unataka kufanikiwa achana na starehe wakati wa kutafuta
7. Muomba Mungu hachoki
8. Ukijaaliwa kupata wakumbuke na walio chini yako
9. Sio kila aliekaribu na wewe anapenda maendeleo yako
10. Usidhulumu na unapomkosea mtu muombe msamaha haraka, maana dua ya aliedhulumia hairudi nyuma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom