Ali Kiba - Lupela

Wimbo ni mzuri. Nimependa dancers wamecheza vizuri sana. Zaidi sana nimependa kwenye background wanavyoonekana tembo wakitembea kwa maringo.
 
Hebu ongea kama hiyo smartphone ya tecno h5 umenunua kwa hela zako na si kwa hela ya shemeji ..................... ( fafanua)
Ukweli ndio huo unajua nini kinafuata baada ya je utanipenda ambayo hata mtwara haijafika achilia mbali burundi
 
Fisi. ....! Huu muda unaomwombea Diamond mabaya ungeutumia kumshauri kiba aendane na soko la mziki wa sasa ungeeleweka vizuri. !
Huo ni ubunifu wake si kila vidio iendane na story ya wimbo tushazizoea sana vidio za aina hiyo
 
Huo ni ubunifu wake si kila vidio iendane na story ya wimbo tushazizoea sana vidio za aina hiyo
Hivi unafikiri wote wanajua kiswahili? Picha inaongea zaidi kuliko maneno. !
 
Mbona mnapenda watu washindane kwa nini..? Sijawahi kuwasikia hawa watu wawili wakutunishiana misuli hata siku moja, wao wanachokifanya ni kupiga hela tu basi, na mziki wao unauza sana mwisho wa siku wanakunja pesa nzuri tu huku sisi tukiendelea kupiga mapambio ya chuki, diamond anasain mkataba na voda kiba anapata dili na akina lupita ng'ongo...piga blaa blaa hapa wao wanapiga pesa
 
Ukweli ndio huo unajua nini kinafuata baada ya je utanipenda ambayo hata mtwara haijafika achilia mbali burundi
Hoja za kimuziki huna, na hapa sio kwa watabiri hapa tunaongea hoja.
 
Mtoto wa Tandale hakamatiki kwa sasa. Huyu kijana ni zawadi ya Mungu kwa watanzania. Pia tumeongezewa na zawadi ya Samatta. Kiba anaimba vzr sema ni mzito sana kufanya biashara ya Muziki. Anatunga na kuimba zaidi ya Diamond ila ndo hivyo hana maujanja ya kupenya sokoni. Wito wangu kwake ni kusaini WCB ili afikie malengo yake. Kama diamond anaishi vzr na madansa wake hata Kiba ajue atakuwa chini ya boss mwelewa.
 
Haaa kumbe Alli Kiba huwa anashindana na Domo nimekuwa nikimsikia mara kadhaa anakanusha kushindana na Diamond!!
 
Huyu mkosoaji hajui kitu..baada ya maelezo yake nimeitafuta hiyo video..ile ndio namna ilivyoandaliwa na haikukosewa imeamuliwa iwe tofauti..kikubwa ukosoaji wake umefanya watu waitafute na bila kujua ameipa promo ya bure.
 
Asa kwanini mnapoteza sana muda kumjadili???...tunaweza kuanzia hapo mjadala wetu.


Na mimi nawashangaa watu kumjadili na kumuita King of Karaoke wakati mimi nawajuwa kabisa mabingwa wa karaoke kwenye ile bar ya Oasis, ndipo nikaja hapa kuzima huu ubishi kwani najuwa yote yasemwayo juu ya Kiba si ukweli bali ni uzushi tu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…