Ali Kiba Fans' Special Thread...

Ali Kiba Fans' Special Thread...

Hapo sasa atoto,kwa iyo wajue wazi kuwa kiba hawezi pambana na mtu ambaye haja request battle,kijana MONDI alilianzisha mwenyewe jamani,alafu embu tutafakari hapo je kiba angetoa naye collabo...ni nani angepata kiki kati ya hao wawili ni yeye ambaye angejisifu kuwa amemuinua msanii wa muda kwenye B.fleva au kiba ambaye angekandiwa kuwa emerudi kupitia MONDI?...kutokana na tabia ya MONDI ya kujisifu KIBA alikuwa na kila sababu yakukataa kuimba naye kisha akaja toka na single yake menyewe ya MWANA iliyokubalika vizuri tu,alafu kuna sehemu humu nimeona diva Beyonce akielezea unafki Kwenye hii industry ya muziki wa B.fleva...yani alichokisema hakukosea kabisa embu ona OmmyDimpoz juzi tu Kwenye tuzo za KTMA alipiga picha na tuzo za KINGKIBA wakati alimpondaga huko nyuma kisa alikuwa rafiki wa MONDI haya sasa now haiivi na ata uyo MONDI mwenyewe...wewe umelionaje hili?..kama vipi mfungulieni Uzi wa kumchamba jamani ama neneee?..wote kwa pamoja(TEAM MONDI na TEAM KIBA) mumpe vidonge vyake...maana alimdharau king wakati ndo alimtambulisha Kwenye B.flavour kupitia track yake ya NAINAI,alafu akabugi kutokana na wema wakati alikuwa shemeji yake kwa MONDI... Huyu jamaa Mimi simuelewi kabisa asee.

Sie tuhangaike tu huyu anayetuhusu dear (The King), hayo ma_ungreatfull fools acha wajibebe wenyewe huko
 
Aiseee kweli Kiba ni fundi, umenifanya nikumbuke hicho kipande alichoimba, wallah acha tu watu waneng'eneke, ila sasa inatakiwa afanye kweli hadi watu wakimbie mji, watamuelewa tu aaah nilisahau washamuelewa ndio maana hawaishi midomoni.
Kiba ni msanii asiye na makuu ila kazi yake, wasanii wengine wanategemea skendo ndipo wabakie kwenye game.
 
haya hongera....but "kama" ni acc ya Diamond hapo kaongea fact

Je "Kutia kichefuchefu " ni sawa?

Well said!! Akiongea mondi sawa akiongea Kiba sio sawa!!! Uwiiii alafu mnatuita wachawi??? You guys beta get help
 
+kuna hizi habari ambazo global waliandika "Diamond amuita jokate makombo" na "kumbe mimba ya Zari ni ya katunzi". Sasa atakayeziamini/aliyeziamini hizi habari basi asisite kuiamini na hii ya Kiba!

+hao ndo global katika ubora wao.

Nyie acheni kuupoteza ukweli tuachane na izo habari za global kuhusu mimba ya zari juu ya diamond na iyo kichefuchefu ya alikiba coz ata Mimi siziamini izo,ila izo screenshots kuhusu dharau za MONDI kwa KIBA alisema mwenyewe kwenye account yake ya Twitter kabisa,nakumbuka hadi watu walicomment kuwa tatizo MONDI ndo anauingia usuperstar ivyo sio kosa lake.
 
Mkuu...kwa kukuelimisha tu usije ukakosea mara nyingine.


Hilo la mimba ni moja ya habari za kizushi kabisa...ndio maana naona hawa Global ni wazushi kwa habari zao zote
Sasa kumbe unajua global ni wazush inakuwaje uwaamini kwa habari ya kiba kuongea hayo maneno ikiwa hamna ushahidi?
 
Well said!! Akiongea mondi sawa akiongea Kiba sio sawa!!! Uwiiii alafu mnatuita wachawi??? You guys brta get help

wapi diamond amesema jamaa anatia kichefuchefu? by the way...Muziki wetu hauwezi kuendelea kwa upuuzi kama huu

At least Mondi anaitangaza nchi yetu

Manake kila sekta tumefeli
 
Sasa kumbe unajua global ni wazush inakuwaje uwaamini kwa habari ya kiba kuongea hayo maneno ikiwa hamna ushahidi?

kwa sababu hawa global kuna wakati hua wanaaminiwa sana humu;

Mfano kwenye habari kuwa "Diamond asema kiba anakula makombo kwa jokate"

Kwenye habari kuwa "Mimba ya zari ni ya Katunzi na sio Diamond"

Otherwise tukubaliane kwa ujumla wake kwamba habari zote za global huwa ni uzushi...Regardless imemuongelea nani
 
Mkuu nikwambie kitu? Tuvue uteam tuweke pembeni..
Ni iviii wewe si unamkubali dai? Na mimi si nina mkubali kiba? Ivi ni vitu viwili tofauti sawa sawa na simba na yanga. Au man u na Chelsea. Isipo fika mahali kila mtu akamind business zake tutajikuta wote ni wajinga. Wew unazani siku yanga na azam wakicheza simba watawashangilia wakina nani? Ukiwauliza sababu ya kufanya ivyo ni kwamba hakuna.
Sasa wew kama unamkubali dai ni maamuzi yako na hamna atakayeweza kukubadilisha na kama mimi namkubali kiba ni maamuzi yangu hamna atakayeweza kunibadilisha. Kila mtu amshauri msanii wake anaye mpenda ila sio kila kiba anachokifanya lazma mumfananishe na domo sio fair. Unaweza ukaona ukakausha tuu kwani ni lazimq kiba awe kama domo? Au domo awe kama kiba? Ushabiki ushatufanya tuonekane kama machiz fulan ivi kutetea adi ujinga kwa ajili ya uteam haitakiwi iwe ivyo kama kiba kazingua njoo useme kiba kazingua hapa na hapa sisi tutaungana na wew lakini kwenye kuzingua kwa kiba usilinganishe na mafanikio ya daimond coz kila mtu na ridhiki yake aliyepanga ni Mungu.
Imekaa poa mkuu si ndio? Yaah ukiona kiba kazingua njoo funguka tuu bila kum compare ili kuepusha mvutano

Aaaiiii watakuelewa sasa?!!! Wamesahau na ile ambayo sio ya global ni ya mtu wa karibu kabisaa wa mondi alisema wimbo wa mwana ulivyotoka walikuwa sebuleni wakiusikiliza na kuusifia huku mondi na mbunge wakiwa chumbani alipowasikia wakiusifia aliwamaid balaaaaa!!! Why amind km hana chuki?

Huyu mtakatifu mondi naye sasa aingizwe kwenye orodha tu ya watakatifu tujue moja.
 
Sawa mkuu kuna text kwa chini nimekujibu kua wew umesema global ni wazushi y uamini iyo issue ya kiba?

nimekusoma mkuu...Argument yangu ni kwamba kama tumeona global ni wazushi kwa habari hii ya kiba...Je tutawaaminije kwa habari zingine mfano ile ya Diamond kusema kIBA Anakula makombo kwa jokate?
 
Mimi naona kiba kazingua sana kwa chuki za hali ya juu alizoonyesha wazi kadri ya habari iliyowekwa

Hahaha!..acha izo wewe wa wapi mkuu?..sasa hao global kwa habari za MONDI huwaamini lakini za kiba unaziamini kabisa,sasa tuwaelewaje nyie wenzetu?...na kama mmeamini hii ya KIBA basi tuungane kusema zile habari za MONDI ni kweli pia bila chenga...ryt?
 
Nyie acheni kuupoteza ukweli tuachane na izo habari za global kuhusu mimba ya zari juu ya diamond na iyo kichefuchefu ya alikiba coz ata Mimi siziamini izo,ila izo screenshots kuhusu dharau za MONDI kwa KIBA alisema mwenyewe kwenye account yake ya Twitter kabisa,nakumbuka hadi watu walicomment kuwa tatizo MONDI ndo anauingia usuperstar ivyo sio kosa lake.

+mkuu kama hizo habari mbili nilizozisema hapo juu huziamini its okey.

+kuhusu hizo screenshot ulizozitoa hakuna mahali nimezipinga kwa sababu sina ushahidi wa kuzipinga. So kama ni kweli alisema ivo si sawa. Maana naona umekuja kiligiligi!
 
Mkuu...kwa kukuelimisha tu usije ukakosea mara nyingine.

Wamepima Kipimo cha Ultrasound kujua jinsia ya mtoto

DNA ni kipimo cha vinasaba(genes) ambacho kinaweza fanywa mtoto akishazaliwa.

Hilo la mimba ni moja ya habari za kizushi kabisa...ndio maana naona hawa Global ni wazushi kwa habari zao zote

Weeeeh do you think sijui dna ni nini??? Kamuelimishe huyo asojua maana ndio alosema hayo, kwikwikwiiiiiii
 
kwa sababu hawa global kuna wakati hua wanaaminiwa sana humu;

Mfano kwenye habari kuwa "Diamond asema kiba anakula makombo kwa jokate"

Kwenye habari kuwa "Mimba ya zari ni ya Katunzi na sio Diamond"

Otherwise tukubaliane kwa ujumla wake kwamba habari zote za global huwa ni uzushi...Regardless imemuongelea nani

Yaaah hapo ni sawa kabisa mkuu.
Ila kumbuka habari ya mimba ya zari global wameiandika tuu juzi lakini taarifa zilishavuja siku nyingi na tukajadili humu sana.
Taarifa za global hatupaswi kuziamini kabisa lakini ikitokea wameandika ivyo ikiletwa huku inajadiliwa kawaida tuu haijalishi inamhusu nani na kama ni kuikosoa global mbona tunaikosoaga sana?
Lakin celebrty bila umbea haiendi ndo maana wakiandika sisi tunaleta huku tunajadili kawaida na mambo yanaisha mbona? Kwani tangu ulishaona kuna bifu zinazoendelea za kitimu kama saivi? Ina maana b4 tuzo za kiba global walikuwa hawaandiki?
 
Sawa mkuu kuna text kwa chini nimekujibu kua wew umesema global ni wazushi y uamini iyo issue ya kiba?

Achana nae huyu anajitekenya na kucheka mwenyewe, do u think he/she ll ever get you?? Muache na mtakatifu wake.
 
Back
Top Bottom