MIMI ni mpenzi wa muziki wa nyumbani kuanzia bongo flava, taarabu, mchriku na kila aina ya muziki. mwanamuziki akifanya vizuri nitampenda tu na wakati wote najizuia kuchukua ipande. nampenda diamond na pia ally kiba ingawaje nampa credit za juu kidogo kiba nikitaka kumlinganisha na diamond ingawaje wote ni wazuri. pamoja na mambo mengine, ninachompendea diamond na vile anavyojituma. kama aliwahi kuisikia Number I ya Nemo na Dimpoz ana kila sababu ya kusema hivyo kwa sababu ile nyimbo 100% ni Naija
nikija suala la p skwea, kama ni ku-dis basi hajam-dis diamond kwa kuwa sizani kama diamond amewahi kufana naija style. wanamuziki wakubwa wa tz waliowahi kufanya staili ya naija ni ommy dimpoz na nemo. aidha, hata p-skwea nae wala huwezi kusema alikuwa na kitu nyuma ya pazia kwa sababu amesema wazi wazi bila kuficha kwamba anaupenda muziki ambao hujachanganywa na wa kinaija.