Alfajiri ya furaha kubwa! RIP DR. FUPI

@rrondo hakuna niliposema nawachukia matajiri ama nauchukia utajiri... Bali nimeelezea njia ya kupita... Hata mimi naupenda utajiri... Anayechekia utajiri au matajiri....! ni mtazamo wake usimhukumu.... Nimependa leo kuweka kumbukumbu sawa... Wakati wengine wakifurahi leo... Wengine wanatoneshwa makovu ya vidonda vilivyosababishwa na matokeo ya ubinafsi choyo na udhalimu
Leo nimekuelewaaa
 
Asante sana brother unatukumbusha,kuna vitu vinatokea Leo kwaajili yakulipia mabaya yetu ya jana.
Nakumbuka ilikuwa miaka ya tisini na kampuni husika ndio huyu alipatikana bila mikwaruzo tena walidondoka karibu watu wanne wa ofisi ya mkemia.
Kwamba hii familia inahusika na kufo cha Dr fupi?
Kampuni husika wakati huo iliwapoteza wafanyakazi wake wengi tu, wengine walifanyiwa unyama na ukatili wa kutisha na kutosha...
Kwenye maghala yake ya kuhifadhia nafaka wamiliki waliweka mbwa wengi sana kwa ajili ya ulinzi... Mbwa hawa walikuwa wakijisaidia kubwa na ndogo juu ya nafaka na hivyo kuzifanya nafanya kuharibika haraka kutokana na kinyesi kuoza na kutoa funza, haja ndogo kusababisha unyevu nknk.... Mfanyakazi aliyejaribu kutoa siri nje ndio ilikuwa kwaheri kubwa...! ama mwandishi wa habari aliyejaribu kufuatilia ilikuwa ama zake....
Tunapoungana na wengine kushangilia mafanikio yao ni vema tutafakari na njia walizopitia... But who cares!!!! After all the end justifies means
nimepata kitu
 
Madhara yatokanayo na vyakula huwa hayajitokezi haraka haraka kama madhara mengine

Huumiza taratibu na kwa style tofauti tofauti kati ya mtu na mtu.

Pia kumbuka huo mchele haukuuzwa kwa wakazi wa Tandale tu! Uliuzwa pembe zote za Tanzania, kuanzia mjini hadi vijijini, kwa mama lishe hadi kwa mwenyekiti wa kijiji!

Madhara ya chakula kisichofaa kwa binadamu kina uwezo wa kukudhuru wewe mlaji hadi atakayezaliwa kutokana na mbegu au yai lako!

Tatizo wabongo wengi tunachukulia poa Mambo haya na hatuyapi uzito stahiki! Ni sawa na tunavyochekelea mfumo mbovu wa elimu yetu sasa kwa sababu madhara yake hatutayaona leo wala kesho,ila baada ya miaka majibu yatakuwa hadharani

Magonjwa yanayotusumbua watanzania wengi,who knows kama sio hayo ma Michele ya kipindi hicho?
Mkuu nimekuelwa vizuri mno, ni kweli kabisa siku hizi kumekuwa na changamoto nyingi sana za kiafya mfano ongezeko la watu kupooza, saratani, kuishiwa nguvu za kiume(jambo linalopelekea ndoa/mahusiano kuvurugika) , kisukari mara matezi dume.

Yumkini huo mchele umekuwa chanzo kimojawapo cha niliyoorodhesha hapo juu pengine na mengine ambayo sijayataja.

Hakika ngamia ni rahisi kupenya.....
 
Aisee asante kwa kutufahamisha tulikuwa wadogo!

Nimejifunza kuacha kudandia mambo Na kusikitika pasipo kujua jambo kiundani!

Dunia ina mengi ya kutisha kwa kweli
Unahusishwa kutekwa kwa MO na hayo ya
Dr fupi? tatizo watawala tuliowapa mamlaka
 
Punch Line ni hii...

" Mbele ya nuru ya mafanikio ya matajiri nyuma yake kuna giza lililojaa udhalimu tupu.....
Ngazi za kuwafikisha watu wengi kwenye kilele cha mafanikio ya kibiashara zimeshikiliwa na mafuvu na mifupa ya wahanga wengi sana! "
 
Back
Top Bottom