Alfajiri ya furaha kubwa! RIP DR. FUPI

Alfajiri ya leo tarehe 20.10.2018 imepokelewa na watu wengi kwa furaha kubwa baada ya kuenea taarifa za kupatikana salama mfanyabiashara kijana bilionea Mohammed Dewji... Ni furaha kwa familia, ndugu jamaa na marafiki na wale wote wasioamini katika udhalimu.....

Mwishoni mwa utawala wa rais Ali Hassan Mwinyi (CCM) mwaka 1989-90... Lilitokea jambo baya sana lililoitia nchi yetu DOA kubwa sana... Mauaji ya kutisha ya Dr. Fupi aliyekuwa mkemia mkuu wa serikali kipindi hicho... Uzalendo wa nchi yake... Utu wema wake, uamunifu na chuki dhidi ya rushwa vilisababisha maisha yake yakatishwe... Akiacha mjane na watoto wawili
Udhalimu, uchoyo, ubinafsi kukosa huruma, hamu kubwa ya kupata kuliwafanya watu wanaojifanya watu Mungu sana kusahau utu wao na kufanya ukatili mkubwa kwa mtu aso hatia! Wakaichukua roho yake mchana kweupe, na kuiachia familia yake majonzi makubwa na machozi ya milele!

Nini kilitokea!?
Kulikuwa na kampuni moja iliyokuwa inajishughulisha na uuzaji wa nafaka... Kampuni hii ilikuwa na mabohari makubwa hapa DSM... Basi kukawa na uhitaji mkubwa wa mchele na ngano kipindi hicho, na kampuni husika ikaingiza tani za kutosha ili wananchi wapate chakula na kampuni ipate pesa
Mchele ule uliingizwa toka uarabuni kupitia Zanzibar nadhani.. Habari zikavuja kwamba mchele ule haukufaa kwa matumizi ya binadamu, ulikuwa umeshaharibika... Kuthibitisha tuhuma hizi ikabidi mkemia mkuu wa serikali aitwe kuupima...!
Mkemia akafanya kazi yake kwa uaminifu na weledi mkubwa akishirikiana na senior lab technician mmoja... Hawa wawili wakaheshimu kiapo chao cha kazi.. KUTENDA KWA WELEDI NA UAMINIFU... Dr Fupi akatoa majibu yake kuwa mchele ule haufai kwa matumizi ya binadamu, yoyote ayakayeutia atapata madhara makubwa ya kiafya yajayo taratibu....
Wenye mali wakapingana na majibu ya mkemia mkuu wa serikali... Malumbano yakaanzia hapo, vitisho nk... Lakini Dr Fupi akashikilia msimamo wake!
Mwishoni mwa wiki ile ya malumbano Dr Fupi akiwa nyumbani kwake akapata ugeni.. Kuchungulia getini akaona hawa si watu wema kwakuwa walikuwa wanaparamia ukuta... Dr kwa haraka akaomba msaada wa polisi wa vituo mbalimbali (alikuwa anaishi Oysterbay)
. Kituo no moja simu ilikuwa busy
. Kituo no mbili gari haikuwa na mafuta
. Kituo no tatu kilipokea wito lakini wakafika kwa kuchelewa kidogo...
Watu wale wabaya waliingia ndani kwake kwa kuvunja mageti na milango na wakamkuta Dr akiendelea kuomba msaada.. Walimkatakata mpaka akakata roho.... Wakaondoka bila kuchukua kitu chochote...
Wiki iliyofuata msaidizi wake akakaimu nafasi yake na kutoa haraka cheti cha ubora wa mchele husika na bidhaa husika ikaingizwa sokoni, huku familia ya Dr Fupi ndugu na jamaa wakiwa kwenye majonzi makubwa ya kumpoteza baba yao... Yule senior lab technician pia alikufa inasemekana kwa sumu....
Kampuni husika ilituhumiwa sana kwenye hili lakini wakati huo Mzee Malecela akiwa mwenye nguvu kubwa akalimaliza ajuavyo yeye....

Maneno ya Mungu yanasema ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuurithi ufalme wa mbinguni.. (Ngamia sio mnyama ni lile kamba kubwa la kushikilia chombo kinapoweka nanga ufukweni ama baharini)
Mbele ya nuru ya mafanikio ya matajiri nyuma yake kuna giza lililojaa udhalimu tupu.....
Ngazi za kuwafikisha watu wengi kwenye kilele cha mafanikio ya kibiashara zimeshikiliwa na mafuvu na mifupa ya wahanga wengi sana!

Ni weekend ya furaha MO kapatikana.... Ni weekend nyingine ya huzuni kubwa kwa familia ile ya Dr Fupi iliyopokwa mpendwa wao hali wakiwa bado wanamhitaji sana... Nitamlilia daima shujaa huyu wa uzalendo asiyekumbukwa popote!
Mshana ndugu yangu umenigusa ujue Dr. Fupi nina nasaba nae na haya unayoyasema niliyasikia sema akili ilikua haijakomaa vzr. RIP
 
Sasa baada ya mchele kuidhinishwa kuwa unafaa na wananchi kuutumia je madhara ambayo yalidhaniwa kutokea yalitokea?
Madhara yatokanayo na vyakula huwa hayajitokezi haraka haraka kama madhara mengine

Huumiza taratibu na kwa style tofauti tofauti kati ya mtu na mtu.

Pia kumbuka huo mchele haukuuzwa kwa wakazi wa Tandale tu! Uliuzwa pembe zote za Tanzania, kuanzia mjini hadi vijijini, kwa mama lishe hadi kwa mwenyekiti wa kijiji!

Madhara ya chakula kisichofaa kwa binadamu kina uwezo wa kukudhuru wewe mlaji hadi atakayezaliwa kutokana na mbegu au yai lako!

Tatizo wabongo wengi tunachukulia poa Mambo haya na hatuyapi uzito stahiki! Ni sawa na tunavyochekelea mfumo mbovu wa elimu yetu sasa kwa sababu madhara yake hatutayaona leo wala kesho,ila baada ya miaka majibu yatakuwa hadharani

Magonjwa yanayotusumbua watanzania wengi,who knows kama sio hayo ma Michele ya kipindi hicho?
 
Mkuu Mshana Jr hebu weka wazi kidogo..
Kwann umeandika maada hii Leo baada ya kupatkana kwa Mo?

Je hyo kampuni iliyokuwa imeagiza Michele ni kampuni gani?
Mmiliki wake ni nani?
Hahahaa! Akikujibu nitag mkuu! Maana nalikumbuka vizur tukio la mchele mbovu!
 
Mimi naisubiria katuni ya kipanya kwa hamu kubwa sana!
Next episode is loading.
tapatalk_1540016274175.jpeg
 
Back
Top Bottom