BAADA YA SHAURI LA MH ZITTO KABWE KUPATIWA UAMUZI WA MAHAKAMA,,NAJIULIZAA,,HIVI NI KWELI KWAMBA KAMATI KUU YA CHADEMA HAIKUWA IKIFAHAMU KWAMBA:-
Ibara 6.3.6(d) ya Katiba ya Chama chao cha Chadema inasema;"Kiongozi aliyechukuliwa hatua za kinidhamu na mamlaka yake ya nidhamu anayo haki ya kukata rufaa ngazi ya juu ya ile mamlaka yake ya nidhamu na uamuzi wa ngazi hiyo utakuwa wa mwisho".???
Kwamba Ibara 6.3.6(e) ya Katiba ya Chama;"Rufaa yoyote lazima ifanyike katika muda wa siku thelathini tangu tarehe ya kupokea rasmi kwa maandishi maamuzi ya mamlaka iliyotoa adhabu".,,na kwamba ;Kanuni za Uendeshaji zinatoa
UTARATIBU ambao unatakiwa ufuatwe ili kiongozi aliyeadhibiwa aweze kutumia HAKI yake ya kukata rufani kwa maneno haya??
Kwamba Kanuni ya 6.5.8 ya Kanuni za Uendeshaji za chama hichohicho cha chadema,inasema;"Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya msingi wa maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumuwezesha kuamua kukata rufani au la"??
Kwamba Kanuni ya 6.5.9 ya Kanuni za Uendeshaji;"Mwadhibiwa atakayeamua kukata rufani atatakiwa kufanya hivyo katika muda wa siku thelathini baada ya kuarifiwa uamuzi wa adhabu"??
Kwamba Kanuni ya 6.5.10 ya Kanuni za Uendeshaji;"Baada ya kutoa uamuzi kikao husika kinalazimika kuandaa taarifa kamili ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha ngazi ya juu.??
Na kwamba Taarifa hiyo, lazima ifike katika muda wa siku kumi na nne baada ya kikao cha maamuzi"??
NITASHANGAA KAMA TUNDU ANTIPAS LISSU ATAACHWA AENDELEE KUWA MWANASHERIA MKUU WA CHADEMA,BAADA YA MAKOSA HAYA YA KITAALUMA
NI WAZI ATAKUWA BILA KUMUNG'UNYA MANENO,,AMESHINDWA KUISHAURI VEMA,NA KISHERIA,KAMATI KUU YA CHAMA CHAKE,ILI IONE JINSI AMBAVYO ILIKUWA INAVUNJA VIPENGELE HIVI VYA KATIBA AMBAYO NDIYO SHERIA MAMA