Albert Msando: Hatushindani na chama au wanachama wa CHADEMA

Mwakalinga Bujo

JF-Expert Member
Oct 22, 2008
2,719
1,440
Wakili msomi Albert Msando ametoa yaliyo moyoni. Kupitia ukarasa wake wa Fb haya ndio aliyoandika.

By; Albert Msando

Kwa marafiki zangu,

Hatujashinda kesi dhidi ya chama. Hatushindani na chama au wanachama wa CHADEMA.

Natambua kwamba kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA mojawapo ya madhumuni ya chama ni kuendeleza na kudumisha Demokrasia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, kujenga utamaduni wa demokrasia katika jamii kwa kutambua haki za wengi katika maamuzi na pia kutambua haki za wachache kusikilizwa, kuheshimiwa na kulindwa, sambamba na kukubali ushindani huru, wa haki na wa wazi ....

Pia natambua kwamba kwa mujibu wa Katiba ya chama Wajibu wa mwanachama wa Chadema ni kuwa tayari kupambana na namna yeyote ya uonevu, ukandamizaji, udhalilishaji na ubaguzi.

Wajibu huu ni ndani na nje ya chama. Hatuwezi kutekeleza wajibu upande mmoja. Binafsi ninalo jukumu kutekeleza wajibu wangu kwa manufaa ya chama.

Kumekuwa na lawama, shutuma na malalamiko kwamba nilichokifanya kinadhoofisha chama. Napinga kwa nguvu zangu zote. Inawezekana kabisa nilichofanya kinadhoofisha watu wachache ndani ya chama ila sio CHAMA.

CHADEMA sio mtu binafsi. Ni taasisi. Wanachama wake ndio nguzo muhimu. Sio Zitto wala Mbowe wala Slaa. Hawa ni viongozi tu ambao wajibu wao ni kuendelea kujenga chama.

Uwezo wao upimwe kwa matokeo ya sasa. Sio kwa mvuto na haiba zao. Fundisho la haya yote ni moja: KUVUMILIANA SIO KUFICHIANA SIRI AU UDHAIFU. Kosa limetendeka na kukubali kosa sio dhambi.

Ni wazi kabisa kumekuwa na kutokuelewana kwa muda mrefu. Ni dhahiri viongozi wetu wamekuwa wanajua udhaifu wa kila mmoja wao. Lakini kwa sababu ambazo hazijawa wazi waliamua kukaa kimya. Au labda ilikuwa ni kwa kuamini kwamba yatamalizika bila athari. Sasa matokeo yake ndio haya.

Kinachohitajika sasa sio kutafuta mchawi. Ni jukumu la kila mmoja wetu kuwajibika ipasavyo na kuhakikisha suluhu inapatikana. Na niseme wazi kabisa, kama suluhu ni mtu kufukuzwa basi tuhakikishe hilo linafanyika kwa mujibu wa Katiba na Kanuni kwa kuzingatia haki za msingi kama ambavyo tumekuwa tukipigania.

Haki itendeke, na zaidi lazima ionekane imetendeka. Pamoja tunaweza.

Mwisho, tusiruhusu muendelezo wa 'ufuasi' wa watu ndani ya chama. Tuwe wafuasi wa misingi ya chama. Bado nafasi ipo ya kurekebisha pale tulipoangukia kama busara na hekima vitatumika.

Nawatakia kila kheri ndugu zangu.

"In a battle for the minority rights we have to promote the rights of the majority and we will remain united" AGM 2014.

Msando
 
Kwani Msando kashinda kesi gani kwa haya matambo..mwambie asubiri kesi iendelee kama hajaikimbia kizimba chake cha utetezi..alikuwa anataka ukaribu na LEMA jamaa akamshtukia kuwa ni msaka umaarufu na noti.

bila shaka wewe pia usingependa kufanya kazi isiyo na ujira
 
Huyu ndio anaeneza propaganda kwamba kashinda na sasa anataka suluhu ili aonekane mwema!,bado mnajaribu kushindana na chama na wanachama wake lkn hamta shinda.Ngoja kesi ianze na nakushauri mwambie Zito akachukue karatasi zake pale ofisini kuonyesha jinsi alivyovuliwa vyeo.Nendeni pamoja nae,nawe Msando diwani wa mabogini na huku hukai mabogini ulipewa kwa heshima ya chadema tu sasa subiri uone moto.
 
msando, najua hata wewe unajua kuwa zitto amepoteza sifa za kubaki chadema ila unachotafuta mkono uende kinywani.

Wakati unapoendelea kumsaidia zitto mahakamani pindi mnapokuwa faragha mwandae kisaikolojia kuwa hatakiwi.

mkuu hapo umenena ya kweli kbc msando yy apige mpunga wake na kujipatia umaarufu! Lkn huyu mnafki lzm ataondoka tu! Na tabasamu kama la chura
 
Da Freema Agyeman ... nilijiunga Chadema nikiwa chuo inspired by Zitto Kabwe...inaniuma kuwa nilimfuata snitch!

So umeamua kuachana na snitch na kufuata ma snichest...

Anyway, tunajua kuwa Kumfukuza sawa mnaweza na mtamfukuza, ila sababu za kumfukuza na utaratibu mnaoutumia sio. Muhimu kawafundisha hilo. Hataondoka Chadema kikondoo bali kishujaa.
 
Jinsi tu Msando alivyoongea anaonekana yuko smart sana kichwani,Ameongea point ya msingi sana.Haya wale wasioweza kabisa kutumia akili zao ipaswavyo katika kudadavua mambo ya msingi na hoja madhubuti kama hizi ni fursa yenu nyingine kuporomosha mitusi,kumwaga kashfa na kuwaita wenzenu majina ya dharau kama mlivyokwishaanza kufanya hapa.Hatuwalaumu ndio upeo wenu wa kufikiri ulipogotea hapo.Kwa tulio na akili zetu kubwa na huru Msando tumekuelewa sana na hongera kwa maneno ya busara na yenye kuonyesha ukomavu wa hali ya juu wa kifikra na kimawazo.
 
Hili ni suala la muda tu.Zitto lazima atatoka chadema kwa kufukuzwa au kwa kujiondoa mwenyewe.Tusubiri tu.Damu za waliokufa kwa ajili ya Chadema zinapiga kelele,msaliti atatoka tu hata ikulu ikiwa upande wake.
 
Zzk kiongoz wangu ww ni mbabe wa siasa za tz, unawanachama wakutosha, hata tukitoka chadema tukaunda chama we ukawa mwkt na tutakupa nafasi ya adhima yako ya kuwa pres. Candidate naamini tutashinda.
 
Back
Top Bottom