Albert Msando: Hatushindani na chama au wanachama wa CHADEMA

Albert Msando: Hatushindani na chama au wanachama wa CHADEMA

anapomtaja zzk kama "kiongozi" anamaanisha nn? Na anaposema "kosa limetendeka na kutenda kosa sio dhambi" anamaanisha Nan katenda kosa?
 
bila kusahau.

attachment.php
 
I am thinking out loud.....What if Mbowe&Co wakapatana na Zitto?
........#FaceDrop itahusika pale kati eeeeh?
Maana nahisi kuna watu wakuwa tu na Chuki....They are so blinded hadi wanasahau hii ni SIASA....These people did not meet barabarani.......na tusidanganyane kwa issue ya USALITI....Wenye akili tunajua these people ni wacheza kandanda wa Team moja...Wana Conflict ya interests tuuuu..ila kusema fulani mchafu,yule msafi ni argument ya watoto.....
Unless kama,mnajisikia tu kugombana,kutukanana,kulumbana ili kuchangamsha baraza.........Enjoy The Game.......
XoXo
Ntakasi Wa Nkasi..
 
Msando ni mwongo,pengine labda wameamuwa kuuwa demokrasia nchini kwa kushirikiana na chama tawala.Unafiki kitu mbaya sana.
 
Wakili msomi AlbertMsando ametoa yaliyo moyoni. Kupitia ukarasa wake wa Fb haya ndio aliyoandika.

By; Albert Msando

Kwa marafiki zangu,


Hatujashinda kesi dhidi ya chama. Hatushindani na chama au wanachama wa CHADEMA.

Natambua kwamba kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA mojawapo ya madhumuni ya chama ni kuendeleza na kudumisha Demokrasia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, kujenga utamaduni wa demokrasia katika jamii kwa kutambua haki za wengi katika maamuzi na pia kutambua haki za wachache kusikilizwa, kuheshimiwa na kulindwa, sambamba na kukubali ushindani huru, wa haki na wa wazi ....

Pia natambua kwamba kwa mujibu wa Katiba ya chama Wajibu wa mwanachama wa Chadema ni kuwa tayari kupambana na namna yeyote ya uonevu, ukandamizaji, udhalilishaji na ubaguzi.

Wajibu huu ni ndani na nje ya chama. Hatuwezi kutekeleza wajibu upande mmoja. Binafsi ninalo jukumu kutekeleza wajibu wangu kwa manufaa ya chama.

Kumekuwa na lawama, shutuma na malalamiko kwamba nilichokifanya kinadhoofisha chama. Napinga kwa nguvu zangu zote. Inawezekana kabisa nilichofanya kinadhoofisha watu wachache ndani ya chama ila sio CHAMA.

CHADEMA sio mtu binafsi. Ni taasisi. Wanachama wake ndio nguzo muhimu. Sio Zitto wala Mbowe wala Slaa. Hawa ni viongozi tu ambao wajibu wao ni kuendelea kujenga chama.

Uwezo wao upimwe kwa matokeo ya sasa. Sio kwa mvuto na haiba zao. Fundisho la haya yote ni moja: KUVUMILIANA SIO KUFICHIANA SIRI AU UDHAIFU. Kosa limetendeka na kukubali kosa sio dhambi.

Ni wazi kabisa kumekuwa na kutokuelewana kwa muda mrefu. Ni dhahiri viongozi wetu wamekuwa wanajua udhaifu wa kila mmoja wao. Lakini kwa sababu ambazo hazijawa wazi waliamua kukaa kimya. Au labda ilikuwa ni kwa kuamini kwamba yatamalizika bila athari. Sasa matokeo yake ndio haya.

Kinachohitajika sasa sio kutafuta mchawi. Ni jukumu la kila mmoja wetu kuwajibika ipasavyo na kuhakikisha suluhu inapatikana. Na niseme wazi kabisa, kama suluhu ni mtu kufukuzwa basi tuhakikishe hilo linafanyika kwa mujibu wa Katiba na Kanuni kwa kuzingatia haki za msingi kama ambavyo tumekuwa tukipigania.

Haki itendeke, na zaidi lazima ionekane imetendeka. Pamoja tunaweza.

Mwisho, tusiruhusu muendelezo wa 'ufuasi' wa watu ndani ya chama. Tuwe wafuasi wa misingi ya chama. Bado nafasi ipo ya kurekebisha pale tulipoangukia kama busara na hekima vitatumika.

Nawatakia kila kheri ndugu zangu.

"In a battle for the minority rights we have to promote the rights of the majority and we will remain united" AGM 2014.

Msando



hongera sana msando,

salam na ziwafikie huko TENGERU,,KILAM KITU HUYO MZEE ASIANGALIE KWA KUTUMIA MAKENGEZA KAMA YALE YA MKWE WAKE,MKAZA BINTI YAKE,,,ZAMA ZIMEBADILIKA HIZI,,

CHAMA KIWE NI CHA KITAIFA,,CHAMA KISIWE CHA KIKANDA,KIDINI NA KIKABILA,HILO HALIKUBALIKI
 
Msando ni mwongo,pengine labda wameamuwa kuuwa demokrasia nchini kwa kushirikiana na chama tawala.Unafiki kitu mbaya sana.

wachaga wengine mnazingua sana,hasa nyinyi sampuli hii,

wengine wana kengeza hadi vichwani mwao,

wengine kama nyinyi mnarembua rembua hadi vichwani mwenu,yani ili mradi tabu tuh kujitoa ufaham,,

HIVI UKANDA,UDINI NA UKABILA UTAWASAIDIA NINI NYINYI MAPIMBI??

HEBU KAZA MACHO HAYO,UNAREMBUA REMBUA NIN MTOTO WA KIUME??AU NI ..MTOTO SIO....,, MALIZIA MWENYEWE
 
Mimi nahisi hao jamaa wameamua kama wanaondoka, basi wataondoka baada ya kuiharibu CHADEMA. Hawataondoka hivi hivi tu. Ninatilia mashaka sana nia yao.
Right on the money, wameamua either wachukuwe uongozi au wavunje chama.I saw this coming.Kazi kweli kweli.Naanza kukumbuka yale maneno yako kuhusu mustakabali wa hiki chama.Very sad yani kwa demokrasia nchini.
 
wachaga wengine mnazingua sana,hasa nyinyi sampuli hii,

wengine wana kengeza hadi vichwani mwao,

wengine kama nyinyi mnarembua rembua hadi vichwani mwenu,yani ili mradi tabu tuh kujitoa ufaham,,

HIVI UKANDA,UDINI NA UKABILA UTAWASAIDIA NINI NYINYI MAPIMBI??

HEBU KAZA MACHO HAYO,UNAREMBUA REMBUA NIN MTOTO WA KIUME??AU NI ..MTOTO SIO....,, MALIZIA MWENYEWE
Mbona we kubwa jinga unamumunya midole ka choko.
 
Msando umewavua nguo wazandiki

msando karudia tu kuusema ukweli unaojulikana enzi na enzi,sioni alipomvua mtu nguo!wala bado sijamuona mzandiki hapo,anachosema msando ndiyo ukweli ambao sisi wadogo bado tuna shaka juu ya mienendo yao kama wanatembea juu ya ukweli huo,na kama ndivyo basi msando aongeze maneno kidogo juu ya andiko lake hilo kuwa !!yupo pale mahakamani kwa ajili tu ya kutafuta riziki yake binafsi.bila kujali uhai au mauti ya chama!! hapo tungemwelewa,ila kwa hoja zake nyingi zilizopita inaonekana hata yeye si msafi,na anafikiri kuwa ataweza kuwa msafi siku akiukwaa ubunge ambao ndiyo ndoto yake kuu.
 
Hili ni suala la muda tu.Zitto lazima atatoka chadema kwa kufukuzwa au kwa kujiondoa mwenyewe.Tusubiri tu.Damu za waliokufa kwa ajili ya Chadema zinapiga kelele,msaliti atatoka tu hata ikulu ikiwa upande wake.

na wale waliokufa kwa ajili ya CUF, na wale waliokufa kwa ajili ya uislamu ( mwembechai + zanzibar),, acheni hizo CDM.
Mbona wewe hukufa kwa ajili ya CDM upo mpaka leo,, aaaah kumbe huipendi CDM ndio maana hukufa!!!!
Mbona hamkuwaunga mkono CUF waliposema wameibiwa kura 2005??? CDM kweli wasaliti...
 
Back
Top Bottom