Albert Msando: Bashiru sio mla Rushwa

Albert Msando: Bashiru sio mla Rushwa

Pole sana kwa best wako kukutwa na hayo yaliyo mkuta na sasa sifa zake zoote zimeporomoka kama mchanga
Wala si best wangu, binafsi sitaki hata kumsikia kwenye chama abaki huko aliko.
 
Ogopa sana kitu kinachoitwa nyakati, kinachobadili watu si tabia ni nyakati, yaan muda utaamua tabia yako iwe namna gani? Kwa yale yanayotajwa dhidi yake kwanini ni yeye tuu na si wengine?
Naamini hivyo pia.
 
Kwenye wizi pana walakini kwa kweli. Ila aina ya uongozi wake ndio iliyomchafua sana. Ubabe ubabe.. Najiuliza sipati jibu - alikumbwa na nini Dr masikini?!! Maana ni kama madaraka yalimlevya. Yeye na yule jamaa mwingine wa ‘viete’. Waliendesha chama kama wanaswaga ng’ombe jamani!

Hapo kwenye ‘pengine walikuwa na jambo lao’, panafikirisha sana. Labda ni Mungu tu ndio ametuokoa na hilo jambo lao. Maana tusingeweza kulizuia. Au ni kweli ‘tunausalama’ mzuri sana kama wachache wasemavyo, kwamba imezuiliwa jambo hilo lisiikumbe nchi (japo siamini kama hao watu wanaweza kulisaidia taifa kiasi hicho, maana na wao walishakuwa watu wa kuabudu). Pole yake Dr.
Umenielewa vyema kabisa. Tunashukuru Mungu ametuepusha na hilo, binafsi nimeshukuru sana 😀
 
Endapo Taifa letu ndani ya CCM wakigombana au wanapogombana
Kutakuwa/kunakuwaga na upande mmoja ambao ni leftist na mwingine center-left

Bashiru ni Pure Leftist, ni mjamaa haswa

Mama Samia ni Center-Left Kwa kipindi kifupi nilichomuona

Hawa Center-Left ni Wabepari ndani ya ujamaa na niwanafiki na wako tayari kufanya lolote kwa faida binafsi.

Hawa Leftist ndio akina Mangula, Hayati Magufuli, Bashiru, Kabudi, Makongoro, Pinda

Majeshi ya Lowassa yakirudi CCM na Majeshi ya Kikwete yakirudi, Daah nchi sijui itakuwaje
 
Kwa ulivyo mtetea inaonyesha unamfahamu kwa ukaribu.

Ila jamaa yako cv zake ndiyo tayari zisha ingia doa
Ni kweli, ni kweli kabisa. CV imeingia mchanga na mama samia kamchomoa tu, tusemeni ukweli pale kachomolewa. Mama angetaka kufanya nae kazi angemuacha kwenye nafasi aliyopewa na hayati na angefanya nae kazi kila siku, na hata angemhitaji katika baraza la mawaziri angemuacha kule kule kama katibu mkuu, sababu kama sikosei katibu mkuu ni katibu wa baraza la mawaziri pia (naomba kusahihishwa).

Bado naamini kachomolewa na kaachwa apambane na hali yake.
 
Kwa uchapa kazi wake ananikumbusha msela wangu wa miaka ile Nicodemus Kashongole
 
Shida ni namna alivyoondolewa sio kwa ustaarabu kabisa, lakini kiuhalisia Dr Bashiru hakuwa seasoned civil servant kupewa nafasi kubwa vile.

Angeweza kufanya kazi na Magufuli aliemteua bila ya kuwa na credential kwa sababu zake personal. Ila kwa raisi mwingine yeyote ni ngumu kuwa na mtu asielewa maswala ya kusimamia serikali kama mshauri wake mkuu.

Kuondolewa kwake is just common sense Bashiru hakuwa na sifa ya nafasi aliyopewa siamini kama kuna sababu nyingine nje hapo, it was coming.

Kama ipo basi ushiriki wake huko ni kutokana na his gullibility kwa nafasi yake, wenzake wakamtumia kufanya yao.
 
Lazima msando amtetee bashiru maana wote walikua task force ya kuua na kuteka watu.....huyu msando alikua anatumiwa na jiwe yeye na bashiru na bashite kuwanyamazisha wakosoaji wa mwendazake

Akae kwa kutulia tuli maana michezo yake ya kula birian kwa bashite tunaijuwa.....Ameshawafunua vizibo sana vijana wengi huyu nyangumi
"Kwanza hizi nafasi ni za uteuzi na kila mtu anachagua mtu ambaye anataka afanye naye kazi na kwanini. Dkt Bashiru Ally alikuwa karibu sana na Hayati Rais John Magufuli alimwamini.

Kwa upande wangu binafsi namkubali na namwamini sana Dkt. Bashiru, mimi ni mmojawapo ninayesema Dkt. Bashiru sio mla rushwa, ana nidhamu na anapenda kazi yake.

Ni mtu ambaye analala masaa mawili, saa 10 kamili alfajiri ameamka hata kama mlilala wote saa 9 hivyo ndivyo tulifanya kazi wote.

Na hicho ndio kitu ambacho alikiona Hayati Rais Magufuli kwake. Naamini kule bungeni ataongeza kitu kikubwa sana" Albert Msando, Mwanasheria.
 
Msando katumia kipimo gani kujua Bashiru siyo mla rushwa?
 
Mbona ni mpayukaji na anaweza kuwa corrupt hata kama unampenda vipi
 
Back
Top Bottom