Albert Msando apotoka tena

Albert Msando apotoka tena

Nimesoma post zote toka mwanzo mpaka hapa naandika nimegundua mambo muhimu ambayo wengi hawayafahamu.
  1. Wengi wenu mmekariri sura ya sita kipengele (a) -(d) bila kujua nini kinaongelewa ndani yake.
  2. Kushindwa (akiwemo msando na zitto) kutoifautisha kati ya kufukuzwa uachama na uongozi.

UKWELI WA SURA YA SITA KANUNI ZA UENDESHAJI KAZI ZA CHAMA

Sura ya sita inahusiana na UANACHAMA (ADHABU ZA KINIDHAMU AU KUFUKUZWA CHAMA).

Nanukuu

"6.5 Taratibu zifuatazo lazima zizingatiwe katika kuchukua hatua za
kinidhamu:-

6.5.1 Kila tawi litaweka kumbukumbu/orodha ya wanachama wanaokoma kuwa wanachama wa tawi. Kumbukumbu itaonyesha jina kamili la mwanachama katika rejista ya wanachama tarehe aliyokoma kuwa mwanachama wa tawi na sababu za kukoma kuwa mwanachama.


6.5.2 Kwa mujibu wa ibara 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba, mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza:

(a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili.
(b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
(c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.

d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu (b), (c) hapo juu kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwanachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.

6.5.3 Mtu yeyote aliyepoteza uanachama wake kwa mujibu wa kifungu 5.4 cha Katiba atapoteza haki zake zote za uanachama na hatarudishiwa ada, zawadi au ruzuku yeyote aliyokwishaitoa kabla ya kupoteza uanachama wake.

6.5.4 Mwanachama aliyepewa adhabu na kikao kimoja cha kikatiba atakuwa na haki ya kukata rufani kwa kikao cha ngazi ya juu ya kile kilichompa adhabu.

6.5.5 Mwanachama aliyewahi kuachishwa ama kufukuzwa uanachama anaweza kuomba kurejea kwa maandishi kupitia ngazi iliyomfukuza akieleza sababu za kutaka kurejea. Maombi yake yatachunguzwa kwenye ngazi hiyo na kutolewa maamuzi na vikao vya ngazi moja ya juu inayofuata. Aliyesimamishwa au kufukuzwa na Kamati Kuu ataweza tu kurejeshwa na Baraza Kuu. Watakaofukuzwa na Mkutano Mkuu hawatakuwa na chombo kingine chochote kitakachotengua uamuzi huo.
6.5.5.Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.

6.5.7 Kiongozi mhusika, zaidi ya utetezi wa maandishi, atapewa nafasi ya kujieleza bayana mbele ya kikao cha mamlaka ya nidhamu.

6.5.8 Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya misingi ya maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumwezesha kuamua kuKata rufani au la.
6.5.9 Mwadhibiwa atakaye amua kukata rufani atatakiwa kufanya hivyo katika muda wa siku thelathini baada ya kuarifiwa uamuzi wa adhabu.


6.5.10 Baada ya kutoa uamuzi kikao husika kinalazimika kuandaa taarifa kamili ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha ngazi ya juu. Taarifa hiyo lazima ifike katika muda wa siku kumi na nne baada ya
kikao cha maamuzi. " mwisho wa kunukuu





SASA TUONE IBARA YA 5.4.3 NA 5.4.4 INASEMAJE

Nanukuu

"5.4 Kukoma kwa UanaChama


5.4.1 Kwa kujiuzulu mwenyewe kwa hiari yake.
5.4.2 Kutokana na kufariki.
5.4.3 Kuachishwa ama kufukuzwa na tawi lake ama ngazi nyingine ya Chama, kwa mujibu wa katiba kwa kukosa sifa za kuendelea kuwa mwanachama ama kuwa na mwenendo usioendana na Itikadi, falsafa, madhumuni, kanuni, maadili na sera za Chama. Mwanachama atakuwa na haki ya kuKata rufaa kwa ngazi ya juu kama hakuridhika na adhabu hiyo.

5.4.4 Bila kuathiri kifungu 5.4.3 cha katiba, Kamati Kuu inaweza kumwachisha ama kumfukuza mwanachama yeyote kwa utaratibu utakaopangwa na kanuni za Chama.


5.4.5 Kukosa sifa za uanachama.
5.4.6 Kufukuzwa uanachama wa Baraza la Vijana au Wanawake au Wazee kwa utovu wa nidhamu."

Mwisho wa kunukuu


ANGALIZO KUHUSU UONGOZI NA KUKOMA KWAKWE KWA MUJIBU WA KATIBA

Nanukuu

"6.3.4 Kukoma kwa Uongozi

(a) Kwa kiongozi kujiuzulu kwa hiari yake
(b) Kwa kiongozi kuachishwa uongozi au kufukuzwa uanachama
(c) Kwa kiongozi kushindwa kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa masharti ya katiba, kanuni au maadili ya Chama.
(d) Kwa kufariki
(e) Ibara hii inahusu pia uongozi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee ya Chama.

6.3.6 Mamlaka za Nidhamu na Uwajibishaji

(a) Kiongozi aliyechaguliwa na Mkutano Mkuu ataweza
kusimamishwa uongozi tu kama ifuatavyo:-
(i) Kiongozi ngazi ya Msingi na Kamati Tendaji ya Tawi
(ii) Kiongozi wa Tawi na Kamati ya Utendaji ya Kata/Wadi
(iii) Kiongozi wa Kata/Wadi na Kamati ya Utendaji ya
Jimbo/Wilaya.
(iv) Kiongozi wa Jimbo/Wilaya na Baraza la Mkoa
(v) Kiongozi wa Mkoa na Kamati Kuu.
(vi) Kiongozi wa Taifa na Baraza Kuu.
Kiongozi aliyeteuliwa na vikao vya uongozi ataweza
kusimamishwa au kuachishwa uongozi na kikao kilichomteua.
(c) Bila kuathiri masharti ya vipengele (a) na (b) hapa juu, kiongozi yeyote anaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kusimamishwa au kuachishwa uongozi na kikao cha juu ya ngazi yake ya uongozi.
(d) Kiongozi aliyechukuliwa hatua za nidhamu na mamlaka yake ya nidhamu anayo haki ya kukata rufaa ngazi ya juu ya ile ya mamlaka yake ya nidhamu na uamuzi wa ngazi hiyo utakuwa wa mwisho.
(e) Rufaa yoyote lazima ifanyike katika muda wa siku thelathini tangu tarehe ya kupokea rasmi kwa maandishi maamuzi ya mamlaka iliyotoa adhabu.
(f) Viongozi wa ngazi ya kitaifa waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wanaweza kusimamishwa uongozi endapo theluthi mbili ya wajumbe wa Baraza Kuu watapiga kura ya siri na kutokuwa na imani na kiongozi mhusika. Baraza Kuu litakuwa na wajibu wa kuteua atakayeshika nafasi hiyo kwa muda hadi uamuzi wa mwisho kufanywa na Mkutano Mkuu."

Mwisho wa kunukuu

HITIMISHO



  1. Kuhusu kuwavua au la uachama watuhumiwa , CHADEMA imefuata taratibu zote hapo ju. Zitto na wenzie wasubiri kuitwa na kamati kuu kwa mahojiano ya ana kwa ana. Baada ya hapo watapewa majibu ya maamuzi ya kamati kuu kwa maandishi ndani ya siku 14 toka mahojiano. Wanaweza kukata rufaa kama hawajaridhika na maamuzi
  2. Kuhusu kuvuliwa uongozi chadema walitumia katiba ibara ya 6.3.4 (c). Hili watuhumiwa waliitwa, wakahojiwa na kamati kuu, wote kwa pamoja wakakiri makosa kwa kuhusika na waraka wakaomba kujiuzuru nyazifa zao.
  3. Wanadai taratibu hazikufuatwa kuwapoka vyeo vyao. Ukivunja katiba na miiko ya uongozi hakuna cha taratibu, katiba iko wazi unapoteza wadhifa ulionao mara moja pamoja na kuchuliwa hatua zingine ikwemo kuvuliwa uanachama ambazo taratibu kwenye hili lazima zifuatwe kama ilivyoainishwa hapo juu.


Wakati ukiwa umenukuu, kipengele 6.3.4(c), kikiwa ni SABABU YA KUACHICHWA UONGOZI, LAKINI UMEKWEPA KUZUNGUMZIA NI MAMLAKA GANI YA UAJIBISHAJI, YENYE UWEZO WA KUIMPLEMENT KIPENGELE HICHO.

Nikukumbushe tu kuwa katiba inasema hivi

6.3.6 Mamlaka za Nidhamu na Uwajibishaji

(a) Kiongozi aliyechaguliwa na Mkutano Mkuu ataweza
kusimamishwa uongozi tu kama ifuatavyo:-
(i) Kiongozi ngazi ya Msingi na Kamati Tendaji ya Tawi
(ii) Kiongozi wa Tawi na Kamati ya Utendaji ya Kata/Wadi
(iii) Kiongozi wa Kata/Wadi na Kamati ya Utendaji ya
Jimbo/Wilaya.
(iv) Kiongozi wa Jimbo/Wilaya na Baraza la Mkoa
(v) Kiongozi wa Mkoa na Kamati Kuu.
(vi) Kiongozi wa Taifa na Baraza Kuu.
Kiongozi aliyeteuliwa na vikao vya uongozi ataweza
kusimamishwa au kuachishwa uongozi na kikao kilichomteua.
(c) Bila kuathiri masharti ya vipengele (a) na (b) hapa juu, kiongozi yeyote anaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kusimamishwa au kuachishwa uongozi na kikao cha juu ya ngazi yake ya uongozi.
(d) Kiongozi aliyechukuliwa hatua za nidhamu na mamlaka yake ya nidhamu anayo haki ya kukata rufaa ngazi ya juu ya ile ya mamlaka yake ya nidhamu na uamuzi wa ngazi hiyo utakuwa wa mwisho.
(e) Rufaa yoyote lazima ifanyike katika muda wa siku thelathini tangu tarehe ya kupokea rasmi kwa maandishi maamuzi ya mamlaka iliyotoa adhabu.
(f) Viongozi wa ngazi ya kitaifa waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wanaweza kusimamishwa uongozi endapo theluthi mbili ya wajumbe wa Baraza Kuu watapiga kura ya siri na kutokuwa na imani na kiongozi mhusika. Baraza Kuu litakuwa na wajibu wa kuteua atakayeshika nafasi hiyo kwa muda hadi uamuzi wa mwisho kufanywa na Mkutano Mkuu."

KWA MUJIBU WA VIPENGELE HAPO JUU NILIVYOVIQUOTE ZITTO KAMA KIONGOZI WA KITAIFA HAWEZI KUVULIWA NYADHIFA ZAKE NA KAMATI KUU, YEYE ANAWEZA KUWAJIBISHWA NA BARAZA KUU TU, TENA BAADA YA KURA YA SIRI KUPIGWA, NA HILO NDO LITACHAGUA MTU KUISHIKA HIYO NAFASI, NA HUYO MTU MWENYE KUISHIKILIA NAFASI HIYO ITABIDI ATHIBITISHWE NA MKUTANO MKUU.

SASA HII KAMATI KUU ITAJIPAJE MAMLAKA YA KUMVUA UONGOZI KIONGOZI MKUU WA KITAIFA KINYUME NA MADARAKA YAKE?
 
Haka ka BEN kanajikuta kenyewe ndio ka PLATO cha CHAGGADEMA,kweli hiki chama kimejawa mambululaaaaaaaaa
 
Hahaha ha.Hapana ....Let us call spade a spade!
Vijana mnauwa chama (CDM), ni wakati sasa kuunda taasisi ndani ya CDM kufundisha watu siasa mnafanya kama vile samba/yanga kwamba striker asipofungia timu siku ya derby eti kahongwa au msaliti...Khaa!Viongozi wa chama wanashutumiana JF inatufundisha nini, mwingine akitoa makala kwenye gazeti wengine wanaitafsiri watakavyo wao ili kuhalalisha walitakalo. Upande mmoja watuhumiwa wanajieleza dhidi ya shutuma, upande mwingine viongozi wapo majukwaani kuwaeleza wananchi yanayojiri wakihalalisha shutuma wakati watuhumiwa hawajatowa utetezi. Chama kinakuwa sasa suala la kambi haliepukiki na haya hujitokeza dhahiri miongoni mwa wanachama yanahitaji busara za hali ya juu kwenye chama kwa sababu hata kiongozi wa juu naye ana watu wake. Rejea UK Tony Blair alibanwa na chama chake kwa uamuzi wa kwenda Iraq na alijua hasimu wake ni Gordon Brown kabla ya uchaguzi aliachia ngazi lakini kwa utaratibu ndani ya chama ambao haukuleta mpasuko mkubwa chamani, vile vile conservative party ya UK Cameroon aliyachukuwa madaraka baada ya rafiki yake kushutumiwa kwamba hawezi kuongoza upinzani bungeni. Yote kwa yote ni siasa na kwa vyovyote lazima tukubali maamuzi ya vikao ila utetezi uheshimiwe, ila ni ngumu kuishinda CCM kwa hizi episode zinavyoendelea CDM........Kinana anazijua sana siasa za Tz na ukizingatia orodha ya wabunge wengi wa CDM walipata ubunge kwa makosa ya CCM (kwenye uteuzi wa wagombea) 2010 haswa kwenye majimbo yafuatayo, Arusha,Arumeru,Mbeya,Iringa,Tunduma,Ilemela,Musoma nk. inahitajika kazi kubwa kuliko ya katibu mkuu kwenda mikoani na kueza makosa ya zitto ambayo ni tuhuma badala ya kuibana serikali........na kuna jambo wewe kama ni mwanasiasa wa ukweli unahitaji kujiuliza, watuhumiwa wa ''usaliti'' wapo watatu lakini issue imekuwa Zitto, inawezekana kabisa ana ushawishi mkubwa kwa wananchi japo viongozi wanaaminisha wananchi kinyume. CDM ikiendelea na hili jambo naona kabisa upinzani unavyofifia........., kwa upande wa CDM kuna wabunge wanaoweza siasa za weledi mfano Mnyika,Slaa,Mdee,Zitto,Arfi hawa wanauwezo wa kuandika ripoti zenye ushawishi wa kitaifa ila kuna ambao yaani akiongea mara nyingi unaona anabishana na spika tu kujenga dhana kwamba wanaonewa.
 
Ben, nakubaliana na hoja ya vichaka vitatu. Kwanza haujui kama huyo aliyesema hayo maneno sio mwanachadema brother. Sio kila anayekosoa sio mwenzetu.

Pili, hoja yangu ni nyepesi sana. Ingeweza kujibiwa kwa NDIO au HAPANA.

Kwamba, je Kanuni zimefuatwa au la. Badala yake hoja inahama na kufanywa ni tatizo kati ya Albert na wanachadema wenzake au Albert na Chadema.

Na kuhamishwa huko kunafanywa makusudi na wale ambao ndio adui zetu. Wanajenga chuki kati yetu wanatuacha tuparuane.

We need to take a step back and think. And after all it's not as bad as its made to look. But only if we both wake up and stop it. My cent.


Mkuu asikupe taabu Ben huyo na mie hatujaanza leo humu kupishana hoja!!!!!
Ila hicho ndio chama chenu mkuu hakuna.jema isipokuwa ya kuoendeza upande fulani tu!!!!
Ukitoa wazo tofauti utaitwa gamba sijui mamluki,umetumwa na wewe sasa unaitwa masalia huk ndani kwenu!!!!!

Mimi si mwanachadema as well sina chama kabisa ila hatuwezi kukaa kimya sababu ni CDM,CCM na wengine ndio vyama vinavyoshikilia hatima yetu kwa matendo yao na sio kadi za mifukoni mwa wananchi!!!!!

Sikutakii mabaya brother ila kwa mawazo yako humo sijui kama utadumu!!!!!!
 
Kuna kipindi unatamani ulale tu na ushtukie imefika 2015 ukapige kura basi! Lakini haiwezekani inabidi ushuhudie tu hizi sarakasi.
 
Ben, nakubaliana na hoja ya vichaka vitatu. Kwanza haujui kama huyo aliyesema hayo maneno sio mwanachadema brother. Sio kila anayekosoa sio mwenzetu.

Pili, hoja yangu ni nyepesi sana. Ingeweza kujibiwa kwa NDIO au HAPANA.

Kwamba, je Kanuni zimefuatwa au la. Badala yake hoja inahama na kufanywa ni tatizo kati ya Albert na wanachadema wenzake au Albert na Chadema.

Na kuhamishwa huko kunafanywa makusudi na wale ambao ndio adui zetu. Wanajenga chuki kati yetu wanatuacha tuparuane.

We need to take a step back and think. And after all it's not as bad as its made to look. But only if we both wake up and stop it. My cent.

Huna hata aibu kuandika usichokiamini.

Kwa hiyo kwenda Serena kukitukana chama na Kamati kuu huku ukilindwa na Vijana wa UVCCM kwako ni sawa na sahihi kabisa.

Loh..wewe ni wa kuonewa huruma!
 
Bora msukule unaweza tumwa sehemu kuliko chuma chakavu lisilofaa kwa matumizi zaidi ya kurejeshwa kiwandani kutengenezwa product nyingine"wewe ni chuma chakavu"

kachumbari haikamiliki bila kutia mbwembwe zote ulizizitaja hapo
Teh teh teh unamaana skrepa..
 
Watu kama Msando hawatakiwi Chadema kutokana na misimamo yao ya kusimamia haki, Msando ni jasiri sana amejikita kwenye katiba ya chama chake wanaompiga wenyewe hawataki kuangalia katiba wanamsikiliza Mbowe na Lema.
 
I have no intention of putting my fate on politicians whom their only proffesional is conning voters_ my godfather,vitto corleone
 
Huna hata aibu kuandika usichokiamini.

Kwa hiyo kwenda Serena kukitukana chama na Kamati kuu huku ukilindwa na Vijana wa UVCCM kwako ni sawa na sahihi kabisa.

Loh..wewe ni wa kuonewa huruma!

Mbona nyie mnapata kura nyingi za urais na.hamtaki kujua uanachama wa supportrs wenu!!!!
Anasema anachokiamani na yupo tayari kukisimamia ndio maana kataka ushahidi wa hadhara ya Tanzania kupitia press!!!!!

Unawezaje kusema huyu mtu hajiamni tena ukiwa na fake ID wewe na yeye nani wa kuonewa huruma????!!!!!!

Wewe ni mfano halisi wa tofauti ya mzalendo na mfuasi!!!!!
 
Kama mambo ya kiserikali/utawala yangekuwa yanajadiliwa kama kifamilia(on family basis) ,vita ya dunia isingetokea_don corleone.
 
Uwazi wa hili jambo ndio linakera wahafidhina!!!!!
Wanataka umma usikie ya upande mmoja tu!!!!!

Asante Msando kwa kuweka kila kitu hadharani na usichoke kila linalojiri weka hewani ili kama haki ikichukua mkondo wake basi asiwepo wa kulaumiwa au kulaumu!!!!!!

Hao wanasheria wenzio wanaojidai kulaumu hapa achana nao kama wana nia ya kweli wangejitokeza kabla hata kushauri tu lakini umeanza wao wanapaka rangi sasa,ni waoga na wasio na uthubutu kama nao sio wahafidhina!!!!!!

Udiwani nini bana; hili la kutishiana kuvuana madaraka kwa kila jambo ndio linafuga wanafiki hapo chamani sababu kwa hili kila mtu atafunga mdomo sababu ukisema wanakuvua madaraka. Kuna vichaka vitatu sasa "vikao halali", "utaratibu wa chama" na "kinyume na wadhifa wake" humu ndio mtikisiko wa chama ulipo!!!!

Stop being over jubilant brother.Do you agree with him?Je wewe unakubaliana na hizo rhetorics kama Mwanachama wa CHADEMA?Be honest to ypurself!

Chadema ni chama cha kinafiki tu hakina maana. Leo hii MUNGI anamuita mawalla freemason? Ilikuwaje wakakubali kupokea kiwanja walichopewa nae ? Huu ni zaidi ya ushirikina.

Huna hata aibu kuandika usichokiamini.

Kwa hiyo kwenda Serena kukitukana chama na Kamati kuu huku ukilindwa na Vijana wa UVCCM kwako ni sawa na sahihi kabisa.

Loh..wewe ni wa kuonewa huruma!

Molemo, nitajie matusi yangu kwa Chama na Kamati Kuu. Nitaona aibu.

Ulinzi wa nini nahitaji? Unawapa sifa CCM wasizostahili hata kidogo. Katika maisha yangu CCM wangekuwa wameongea na mimi au wamenitumia kwa hata jambo moja wangejisifu sana. Hilo halitakaa litokee na wanajua hivyo.

Inawezekana kabisa wewe ni mwanaCCM unajidai Chadema kwa kusema uongo na uzushi ili ionekane kuna tatizo. Tunawashtukia na tutawakomesha. Ujanja wenu wa kuchonganisha kwa kutumia kivuli cha kutojulikana kimefika mwisho.

Hatuendekezi upuuzi. Na kama ni mwanachadema na unaamini unachosema nipigie simu unieleweshe na mimi nitakuelewesha. Hakuna sababu ya kujificha. Nitumie PM na nitajadiliana na wewe vizuri tu.
 
Nadhani wewe ndio unatakiwa kutiliwa mashaka uwezo wako wa kuelewa sheria maana unaonegea mambo ya kusikia pasipo kuwa na facts. Kwenye huo waraka kuna mahali popote jina la Zitto Kabwe limetajwa? Hata kama lingekuwa limetajwa kuna ushahidi kuwa alihusika kuuandaa? Leo mimi nikiandaa waraka nikaweka jina la Mbowe utalazimisha kuwa Mbowe anaufahamu? Mbona CDM wanataka watu waamini kuwa Video ya Lwakatare ni ya kutunga lakini haohao hawataki kukuli kuwa ZZK hausiki na kuandaa waraka Leta ushahidi kuwa alihusika kuandaa nasi tutakuamini.

Jaribu kuwa great thinker acha kusukumwa na chuki binafsi, mhukumu mtu basing on facts beyond reasonable doubts siyo kwa kusikia story za kwenye vijiwe vya kahawa.

Naona hata wewe umeendeshwa na mihemko.Kwa nini unatumia kesi ya Lwaks kama ref;CDM waliposema ni ya kugushi wana ushahidi wao,ambapo pindi ukihitajika watautoa.Halikadhalika wanaposema MM ni muhusika pia nategemea wana ushahidi vilevile.Ila kutumia Kesi ya Lwaks kutaka kumtetea Zitto,huo ni upuuzi.

sikutegemea Zitto kama ni mdhaifu kiasi hiki.Kwa akili yangu ndogo, ningetumia muda huu kuandaa utetezi wangu wa kutosha,nikaukabidhi kwa hiyo CC.then nikasubiri maamuzi yao.Kama nimeonewa taratibu nyingine zingefuata baada ya maamuzi yao yote.Kwa hili analolifanya ameishaonyesha, anatafuta huruma ya wananchi ili akipigwa chini,atafute watu wa kumuunga mkono.
Kwa mtizamo wangu ,huyu ni mtu wa kufukuzwa tu,anaonyesha ana matatizo sana.Anaonyesha pia ni mtu asiyependa kuongozwa kwa kufuata taratibu.
 
Watu kama Msando hawatakiwi Chadema kutokana na misimamo yao ya kusimamia haki, Msando ni jasiri sana amejikita kwenye katiba ya chama chake wanaompiga wenyewe hawataki kuangalia katiba wanamsikiliza Mbowe na Lema.

Jasiri ni Chenge tu aliyewaambia kwamba Gamba lake limefika kiunoni na halivuki, wote mmefyata mkia mpaka Alhaji Mkwele naye kimyaa!
 
Ben saa tisa alasiri,jiandae kuficha uso wako kipindi ZZK atarejeshewa madaraka

Kwa hiyo Lumumba mmejiandaa kumrudisha madarakani?

Kukusaidia zaidi soma MAWIO la leo Uk wa 4
 
JF,

Issue sio Msando Albert ni nani au kwa nini anatetea.

Issue ni rahisi natetea nini na utetezi wangu uko based kwenye nini.

1. Utaratibu wa kumvua Zitto nyadhifa haukufuatwa.

2. Sababu zilizotolewa ni circumstantial. Hazijitoshelezi. Zote zinatokana na waraka wa Mwigamba.

Kabla ya kutukana, kudharau na kukejeli yajadiliwe ninayoyasema na sio mimi.

Kama kijana, mwanachadema mwenye taaluma ya Sheria nina wajibu kusema haya. Sasa nikosolewe makosa yangu kwa nafasi hizo tatu na sio vinginevyo.

Mpaka sasa hakuna mahali ambapo hoja inatolewa ya wapi sistahili kusemea. Jazba hazijengi wala kuelekeza njia sahihi kama lengo ni kujenga.

Ila kama nia ni kupiga story tu kumaliza siku ni sawa pia.

Msando Albert,

Ikithibitika kuwa taratibu hazikufuatwa, je hiyo itafuta tuhuma walizopewa Zitto na wenzake? Na hivyo kufuta nia (intention) ya Kamati Kuu kuwaadhibu Zitto na wenzake? Hata wakimrejeshea Zitto nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu, atafanyaje kazi na timu ambayo inaamini kuwa Zitto ni msaliti? How will he fit in? Katika hali hiyo, chama kitaimarika vipi?

Na ukiacha taratibu, hizo tuhuma 11 ni zipi na majibu yake ni yapi? Sina hakika kama kwenye taarifa yako ya jana ulijibu tuhuma 11. Did you? If not, I am inclined to believe it was strategic. Kwa nini hizi tuhuma 11 zisiwekwe wazi ili wote tupime uzito wake? Mwenye kuzifahamu hizi tuhuma, tafadhali.
 
hahaha makamanda wana hasira Tundu Lissu kagaragazwa. Sasa hivi hawana jinsi zaidi ya kumrushia tofali msando au wamfukuze kabisa.

Maana kwa hoja hawamuwezi kabisa na lazima utasikia wana sema kumchukulia hatua maana kamdhalilisha mwana sheria wa chama kuonekana amepitisha maamuzi yanayo kihuka katiba yao.

Yani lissu anatoa hukumu (1) bila hata ya kusikiluza?nasikia kwenye kikao cha kamati kuu iliyotoa maamuzi ya kijuha Tundu Lissu alitaka wafukuzwe hata bila kusikilizwa maana kuandaa mtu kugombea uenyekiti ni uhaini hila mtei kumuandaa arfi si uhaini maana yeye ni chadema chumbani.

Fikiria mtu kama Tundu Lissu alivyo dikteta ndio mwanasheria wa chama chao.

Tundu Lissu alishindwa kumuwajibisha Godbless J Lema kwa kumpiga mwigamba tofali lakini ana jigamba ni mpigania haki.

Huyu Tundu Lissu ameshindwa kuwakemea redbragad kuacha utekaji na uporaji (2) badala yake amejikuta ana kubali kuwa lwakatare alipanga tukio la utekaji hila alirekidiwa na ludo(kamsome kwenye maelezo yake kwenye tukio la ludo)alaf bado wana muita mtu makini.

Huyu tundu lissu na lema ndio wataichimbia kaburi chadema.


Mkuu, hata kama humpendi Lissu mpe haki yake. Kwenye RED (1) yeye hakutoa hukumu-cc ya chama ndio imetoa hukumu, yeye alitakiwa kuwasilisha tu. Kumbuka msemo wa wahenga- Mjumbe hauwawi. CC haikuwa kikao cha mtu mmoja wala wawili, na kwa kawaida kuna kuafikiana na kutoafikiana katika mjadala. Hivyo kupelekea kupigwa kura, hivyo watakaoshindwa lazima waunge mkono upande ulioshinda. Hivyo unamkosea Lissu unavomshambulia kuwa kahukumu.

Kwenye RED (2) ni ule ule upofu au mahaba uliyonayo kwa Zitto unakufanya uwapakazie REDBRIGADE. Nani Katekwa na kuporwa?? unaweza kuthibitisha hilo?? Kumbuka mdomo ni mali ya mtu na halipii kodi, hivo anaweza sema lolote muda wowote. Kimbembe kinakuja kwako wewe utakayepokea maneno usioyajua na kuanza kushabikia.

 
Hivi hizi pesa anazomwaga bwana zitto kwa watu kama hawa si angejiwekea hifadhi zikamsaidia baadae? au ndo sikio la kufa halisikii dawa?

Kwani anatoa mfukoni au zinatoka mfuko mkuu wa Serikali kwa kazi za TISS?
 
Back
Top Bottom