Void ab initio
JF-Expert Member
- Mar 1, 2015
- 5,723
- 5,662
- Thread starter
- #81
Pole saana Mh. Zitto Zuberi Kabwe na hongera kwa CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO. Kwani kwenye mpambano wa aina yeyote lazima kuwapo na mshindi na mshindwa. Binafsi sina uhakika kwa kinachoenedelea kuwa kinatokana na watu wenye dhamira moja ama ni dhamira tofauti zenye maslahi binafsi?
Napata wakati mgumu saana pale ambapo chama kinachosisitiza demokrasia kuwa na sheria ya kumtimua mwanachama wake yeyote atakayekwenda kupeleka mashtaka ya aina yeyote mahakamani dhidi ya chama hicho na akashindwa. Mh. Zitto aliona kwamba hatendewi haki na chama chake Je angekimbilia wapi kama sio kwa Mtafsiri wa sheria? Nafikiri chadema kama chama cha demokrasia basi hapa hakina budi kufanya mabadiliko ili kuwa mfano hai kwani tumeshuhudia katka nchi za jirani zetu wale wote waliokuwa hawakutendewa haki ndani ya taasisi za ndani za serikali wamekuwa wakikimbiza mashtaka yao UGHAIBUNI.
Kihistoria kuna habari ya kwamba ndani ya chadema kulikuwa na mgogoro wa kimaslahi kati ya Mh Zitto zuberi kabwe na viongozi waandamizi wa chama hicho, baadae shutma zikarudi kwa Mh. Zitto kushirikiana na CCM pamoja na taasisi za juu za serikali katika kudhoofisha hali ya upinzani hasa Bungeni. Sina hakika na shutuma za Chadema kwa kuwa uwezo wa Mh. Zito Kabwe wa kujenga hoja juu ya kuikosoa serikali ulishuhudiwa na watanzania wote. Na kuhusu mgongano wa maslahi, kwa kumbukumbu zangu ni kwamba si wa kwanza Mh. Zitto kutamka hayo bali kuna waliotangulia ambao walijaribu kutoa hoja za Kukijenga chama imara CHADEMA kwa kupingana na maslahi na matakwa ya viongozi waandamizi lakini waliishia umauti.
Naomba niseme kwamba kwa hayo yote yaliyokuwa yanaendelea ndani ya chadema ni dhahiri kwamba nchi hii bado haina upinzani wa kweli wenye dhamira ya kumkomboa Mtanzania bali una upinzani wa kichama wenye maslahi na chama..Nomba nikitakie safari njema CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO na pia namuomba mungu amuongoze Mh Zitto Zuberi Kabwe katika jitihada zake za kumpigania Mtanzania, nina imani bado wananchi wa kigoma na watanzania wote tuna imani na Mh. Zitto Zuberi Kabwe katika harakati za kumkomboa mtanzania.
Mkuu hakika umesema ukweli mtupu.