Albert Msando acha kutetea tumbo lako. Hauna uwezo wa kudadavua na kujua mambo kama Prof. Shivji

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,126
4,169
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga Wakili Albert Msando amesema mkataba uliosainiwa baina ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mamlaka ya usimamizi wa Bandari nchini (TPA) na serikali ya Dubai kupitia Kampuni ya DP World ni wa jumla kwakuwa kifungu cha Pili 'C' cha mkataba huo kinasema kutakuwa na mikataba midogo midogo (HGA) ambazo zitataja haki za kimkataba zote kuhusiana na yale ambayo pande hizo mbili zimekubaliana

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi (CCM) unaofanyika Wilayani Korogwe, Mkoani humo Wakili Msando amewashukia wanataaluma wa sheria wanaopotosha umma kwa kutafsiri tofauti vifungu na vipengele vilivyopo kwenye mkataba huo na kueleza kuwa hapo inaonesha utofauti ulipo kati ya watu waliosoma sheria na mawakili kama yeye

Aidha ameeleza kuwa mawakili pia wametofautiana kwenye utendaji kazi kwakuwa wapo waliobobea kwenye uwakili wa uwekezaji kama yeye lakini wengine ni mawakili wa mirathi, ndoa nk, hivyo ameshangazwa kuona mawakili wa mirathi wanakuwa wazungumzaji zaidi kuhusiana na masuala ya DP World na hivyo kujikuta wakifokafoka

Amesema makubaliano hayo yanaonesha umakini wa serikali kwa kumhakikishi muwekezaji kuwa kampuni itakayoanzishwa hapo ni lazima iwe kisheria na kwamba mojawapo ya jukumu walilonalo DP World ni pamoja na kuanzisha kampuni hapa nchini itakayotekeleza makubaliano hayo

Ameeleza kuwa DP World wakifungua kampuni hapa nchini maana yake ni kwamba kampuni hiyo itasimamiwa na kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria za Tanzania kwakuwa imesajiliwa hapa nchini

Ameendelea kuufafanua mkataba huo kwa kueleza kuwa, hakuna ardhi itakayohamishwa kwenda kwa kampuni iliyofunguliwa hapa nchini au Dubai.

Chanzo: Jambo Tv
 
Mpaka hapa tulipo, tuliwashawapuuza wote watetezi wa DPWORD na hata atokee nani, wote ni wa kupuuzwa
 
Huyu DC tangu aingize Midole yake kwenye "X-Zibit" ya Gigi mahela amekuwa na Magundu sana! Nina wasiwasi wadudu washapanda kichwani na kumuwehusha.
 
Shivji ndo anaejua Sana na kushauri serikali iendeshe Bandari?
Shivji hajui kuanzia Marekani Hadi China Hadi ujerumani Hadi South Africa kote huko serikali zimeshaacha kuendesha bandari?

Shivji kabaki Karne ya 20...Karne ya Nyerere,Mao..Stalin na Karl Marx
 
Back
Top Bottom