Albadir iliyosomwa Tanga

Albadir iliyosomwa Tanga

Umeanza vizuri ndugu mshana,lakini baadae niktatafsiri hisia yako aaah kumbe imani na siasa!basi vitu hivyo ni kama maji na mafuta.
 
Wakati USA na nchi nyingine zilizoendelea wana pishana kwenda kwenye anga za juu ka vile wanaenda kariakoo sokoni,sisi tunashabikia albadir ambayo ni uchawi mtupu! MUNGU iponye Tanzania.
 
Umeanza vizuri ndugu mshana,lakini baadae niktatafsiri hisia yako aaah kumbe imani na siasa!basi vitu hivyo ni kama maji na mafuta.
Mitazamo haiwezi kulingana na tafsiri pia
 
Wakati USA na nchi nyingine zilizoendelea wana pishana kwenda kwenye anga za juu ka vile wanaenda kariakoo sokoni,sisi tunashabikia albadir ambayo ni uchawi mtupu! MUNGU iponye Tanzania.
Tunamsingizia Mungu mengi sana
 
Watu wasipo kunywa pombe tbl na sbl watauzia wapi mizigo yao?????. Maana huko ndiko serikali inaongoza kujiingizia kodi
 
Kuna mwingine leo alikuwa anaropokaropoka hovyo tena ni kiongozi mkuu, hovyo kabisaaaa
Whatever you insult your prezdaa..rem you insult yoself and all the country..
Kwa ufupi mfano' babako akiwa mlevi mpaka anajikojolea ukiwa unamcheka na masela,una aibika wewe na familia yako yote.
 
Njaa baba njaa
IMG_20171003_193142_975.jpg
 
Inasemekana ndio albadir mbaya zaidi kuwahi kusomwa, maana madhara yake yalikumba hata wasiohusika. Ilisomwa kwa niaba ya Mzee mmoja wa kidigo baada ya kuchoka kuibiwa nazi zake na vijana wa Tanga mjini, na alifikia maamuzi hayo baada ya kutoa onyo na tahadhari!

Albadir ile ilikausha majani ya njia walimopita wezi, visu vilivyotumika vilikatikakatika, punda aliyebeba alikufa, gari ya punda ikiharibika vibaya, wezi wote walikufa wameachama huku nguo za siku ya tukio zikiwa kama zimemwagiwa tindikali, miili yao ilioza kwa kasi ya ajabu hata kabla ya kuzikwa, yeyote alinunua ama kuhusika na zile nazi alipata madhara ya ugonjwa na kifo.....

Inasemekana makaburi ya wale wezi vijana wane, hayakuota majani kwa miaka mingi. Tukio la kushambuliwa TL liliwaumiza na kuwasononesha watu wengi, ndani na nje ya nchi.. Wengi walilichukulia kama uonevu mkubwa

Kitu hicho kikapelekea kuja na wazo la kusoma kisomo cha albadir kwakuwa kulikuwa na hisia kwamba haki haitatendeka...
Visomo husika vilisomwa japo si kwa mafanikio sana kwakuwa zilitumika nguvu kubwa sana kuvizuia lakini vilisomwa kwa siri kwenye baadhi ya maeneo...

Lakini hata kama visingesomwa ile hali tu ya kusononeka kwa watu wengi kwa pamoja na kutajataja visomo, kiroho hali hiyo ilileta athari kwa wahusika (hapa nitapingwa na baadhi ya watu)

Baada ya hapo yameanza kutokea mambo ambayo ukiyatazama kwa jicho la kiroho kisha ukaunganisha dots ni kama vile kuna uhalisia unaoshabihiana na visomo vilivyosomwa....

Athari za visomo vya albadir wakati mwingine si lazima afe mtu, bali hata kuchanganyikiwa na kuharibikiwa kwa mambo pia yaweza kuwa ni matokeo ya kisomo

Visomo vimepingwa na kukosolewa kwa maelezo marefu mengine yakiwa hayaeleweki lakini asikudanganye mtu kisomo ni kisomo tuu. Usijaribu kabisa kukidharau

Jerry Muro kijana aliyechipukia kwenye uandishi wa habari hata kufikia kupata tuzo, ni muwewesekaji namba moja.. Achana na yaliyowahi kumkuta huko nyuma bado alikuwa anaweza kuandika hoja na ikaeleweka....

Lakini sasa inafika mahali unamuonea imani... Haeleweki anaandika nini na kila anachoandika kinakuwa na mapungufu mengi kuliko ya goma langu cocochanel

Najiuliza Jerry anayejivunia kupata degree moja nchi tatu tofauti ana nini na CHADEMA? Ana nini na TL!? Ana nini na akina Nasari na Lema? Ni kisomo kimempata ama kuna asili yenye mizizi mirefu iliyokuja kuzaa chuki kubwa namna hii? Je kuna wakati pengine alitaka kuingia CHADEMA na kutegemea apate nafasi halafu akakosa?

Vyovyote iwavyo Jerry ni mhanga mkubwa wa yanayotokea sasa na yamemjeruhi kwa namna ya kipekee kabisa na ni katikati ya kiwewe hicho anakaribia kuwehuka kabisa na kuropoka hata ambayo hakupaswa kuyasema... Kuna faida katika kuweweseka kwake!

Kuna faida kwenye kuropoka kwake! Anatufunulia mengi ambayo tungetumia muda mwingi na nguvu pia kuyajua. Ni wakati wetu sasa tuvute viti, tukae kimya tuli kabisa tutege masikio, wanaoweweseka wanazidi kuongezeka... Visomo haviendagi bure
Wengine wameanza kukana kauli zao za siku ya mei mosi hatapandisha mshahara mpaka biashara itakapokua nzuri!amesahau serikali haifanyi biashara
 
mshana jr unachioongea ni sahihi kabisa, nilishuhudia pemba. Miaka ya 1998 kuna mzee aliibiwa karafuu zake, na alitangaza kua atasoma albadiri. akatafutwa mwalimu na akamuaga aende chini ya mkarafuu achukue udongo eneo lote lililozunguka mkarafuu. ukaletwa ule udongo na mwalimu akasema kwa vyovyote wezi lazima watakua wamekanyaga.
mwalimu akipiga albadiri(kule pemba tunaita halbadiri), kilichotokea kati wezi wanne watatu walikufa. uyo mmoja aliyepona alikwenda kuomba msamaha baada ya kuona wenzake wamefariki, lakini pia alikua chizi (mwendawazimu au mpungufu wa akili) na aliambiwa akaoneshe walipozificha. walipokwenda walikuta viroba viwili vya karafuu zote zimeoza na kiroba kimoja zilianikwa mpaka lakini karafuu hazikukauka (kwa kawaida karafuu huanikwa juani zikimalizwa kuvunwa). niliondoka pemba 2001 lakini bado huyu mtu alikua chizi. albadiri ikipata msomaji haimuachi mtu salama hata siku moja.
 
Back
Top Bottom