Alaa! Kumbe wamiliki wa DOWANS ndo hawa!?

Alaa! Kumbe wamiliki wa DOWANS ndo hawa!?

Jamaa wametupapasa, wametutekenya, sasa Walichobakiza mabwana hawa ni kutupiga miti, I mean miti riali kabisa tena kwa kupanga foleni.
Inauma sana, lakini ndo hivyo unyonge na ubwege wetu ndiyo umetufikisha hapa.
 
LAZIMA JK awe na 10% japo hawajamtaja. unadhani hii movement haijui? naamini kaibariki akisubiria mlingula dili ikimachua.
 
1) Rostam Aziz.
2)Eduard Ngoyaye Lowasa.
3)Nimrod Mkono.

Hawa jamaa ni wamafia wapo kila mahali kwenye rada wao, epa wao, IPTL wao hivi mbona tunasumbuliwa na kikundi cha watu hata hawazidi kumi nasi tuko zaidi ya 40Mil.

Lazima tutafute dawa 2015 ndio mwisho wao.
 
Wakitaka kulipa watuambie hao watu wanaolipwa hizo fedha ni wakina nani
 
Wakitaka kulipa watuambie hao watu wanaolipwa hizo fedha ni wakina nani
Mtaona tuu hizo pesa zitalipiwa kupitia Bank M ili kudhibiti habari. Si mnajua Namba 3 ni mmiliki wa hiyo Bank.
Nchi hii tunafanywa vilaza sana!
 
Wananchi wengi kwa mujibu wa gazeti la Majira wamehoji na kumtaka JK ahakikishe wammiliki wote wa DOWANS wanatangazwa hadharani kabla ya malipo yaliyopitishwa na maamuzi ya kisheria.................

Wamehoji uhalali wa kuilipa kampuni ambayo wamiliki wake ni hewa....................

'Mwenye Dowans atajwe kabla ya kulipwa'

Na Waandishi Wetu

SAKATA la malipo ya sh. bilioni 185 kwa Kampuni ya DOWANS iliyorithi mikoba ya kampuni hewa ya Richmond imezidi kuchafua hali ya hewa baada ya wananchi kumtaka Rais Jakaya Kikwete kumtaja hadharani mmiliki wa kampuni hiyo
kabla ya kulipwa mabilioni ya fedha za walipa kodi.

Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti kutoka mikoa mbalimbali, wananchi hao wamesema wanasikitishwa na kauli ya serikali kukubali kuheshimu sheria kulipa Dowans fedha hizo wakati mmiliki wake hajulikani hadi sasa.

�Tunataka serikali, hasa Rais Kikwete, atuonyeshe mmiliki wa Dowans, ajitokeze hadharani mbele ya vyombo vya habari tumfahamu. Haiwezekani nchi ikashindwa kesi na hewa, maana hadi leo hatujui mmiliki wa Dowans ni nani.

"Pia tunataka hiyo hukumu ipelekwe kwa Jaji Mkuu ili baadaye ilitolewe hadharani kwa vyombo vya habari tujue inasemaje,� alisema Bi. Catherine Maliwa wa Kigogo Dar es Salaam.

Alisema katika historia ya Taifa la Tanzania haijawai kutokea nchi ikashindwa kesi na mtu asiyejulikana na kuonya viongozi wa Serikali wanaohusika kutothubutu kutoa hata senti kulipa Dowans bila wamikiki wake kujulikana na kujitokeza hadharani.

“Jambo linalotusikitisha ni kuwa Richmond ni Kampuni feki na wamiliki wake hawajulikani, iweje Kampuni feki ambaye mmiliki wake hajulikani kuuzwa kwa Dowans, mtalipa pesa mashetani?� alihoji Bi. Maliwa.

Alisema hivi sasa Watanzania wamechoshwa na viongozi wazembe wanaowabebesha mzigo wajane na maskini huku wahusika wakibaki salama na kufurahia maisha ya anasa kwa jasho lao.

Alisema baada ya hatua ya Rais Kikwete kumtangaza mmiliki wa Dowans na mwenye kampuni hiyo kujitokeza hadharani na nakala ya hukumu kukwekwa hadharani kwenye vyombo vya habari wahusika wote wachukuliwe hatua za kisheria suala la kulipa fedha hizo liwe la mwisho.

Mkoani Shinyanya wananchi walisema licha ya Mahakama ya Kimataifa ya kusuluhisha migogoro ya kibiashara (ICC) kuipa ushindi Dowand, utekelezaji hauwezekani hadi mmiliki wake ajulikane kwa Watanzania wote.

Walisema ni ajabu na mshangao kwa shirika la serikali kupelekwa mahakamani na mtu asiyejulikana huku baadhi ya viongozi waandamamizi wakionesha kwa haraka dalili ya kutaka kulipa adhabu hiyo kwa mtu asiyefahamika.

“Umefika wakati kwa Rais Kikwete abebe jukumu la kuwafahamisha rasmi Watanzania mmiliki halisi wa Dowans, itakuwa ni miujiza na aibu kwake kulipa fedha hizo kwa mtu asiyejulikana. Watanzania hatujawa wajinga kiasi hicho, kila mara serikali imekuwa ikieleza wazi kutomfahamu mmiliki wa Dowans,� alisema Bw. Fredy Mmassy.

Wananchi hao walihoji kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa serikali inaheshimu sheria na kwamba ikibidi haina ujanja zaidi ya kulipa mabilioni hayo kwa Dowans.

Rais atueleze na amtaje huyo mtu, vinginevyo Watanzania hatutokubali fedha hiyo ilipwe, na hata ikilipwa kwa nguvu waelewe iko siku tutaidai kwao, alisisitiza Bw. Mmassy.

Wananchi hao walisema mbali na Rais Kikwete kumtaja mmiliki wa kampuni hiyo pia awaeleze Watanzania mwakilishi wa serikali aliyeiwakilisha TANESCO katika mahakama ya ICC.

Walisema imefika wakati wa serikali kuweka wazi mkataba kati yake na kampuni hewa ya Richmond pamoja na ule wa Dowans ili kila kitu kifahamike na Watanzania wajionee wenyewe ni wapi TANESCO inapotiwa hatiani kabla ya fedha hizo kulipwa.

Katika hatua nyingine wananchi hao walimtaka Rais Kikwete kuangalia upya maamuzi ya TANESCO kupandisha bei ya umeme na kuweka wazi kuwa hali hiyo haiendani na maisha yao duni na umasikini uliokithiri.

Tunaomba Rais Kikwete kama kweli anawathamini Watanzania waliomchagua kwa moyo mmoja basi, azuie ongezeko la bei mpya za umeme, viongozi wetu wameonesha wazi kutokuwa na huruma na watu wao, wanakubali kulipa sh. bilioni 185 na kuongeza bei ya umeme,� alisema Bw. Masunga Jilaba, mkazi wa kitongoji cha Ndembezi mjini Shinyanga.

Hawa wana haki ya kufanya hivyo kwa sababu hawatoi hata chapa moja mifukoni mwao kwa ajili ya kulipia umeme, uchungu wataupata wapi? Ni Watanzania masikini wanaohangaikia hata mlo wao wa siku ndiyo watapaswa kulipa deni hilo la Dowans kupitia ankara za kila mwezi za matumizi ya umeme,� alisema Bw. Jilaba.

Wananchi hao walisema ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 18.5 ni dalili ya wazi kuwa wateja wa TANESCO ndiyo wanaopaswa kuilipa Dowand na kwamba hilo halihitaji mtu kuwa na elimu ya chuo kikuu kufahamu kuwa kampuni hiyo ni ya mfukoni na kuna watu wanafaidika nayo kwa njia moja au nyingine.

Katika hatua nyingine wanachi hao wamehoji kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Bw. Edward Lowassa, kwamba wananchi watangulize upendo kudai katiba mpya na kumtaka atafute kwanza upendo na huruma kwa Watanzania.

“Najiuliza ni upendo gani anaounzungumzia, yeye anajua upendo tumeumizwa na mengi ikiwemo mikataba mibovu, kama angejua upendo nchi isingeingia katika mkataba wa aibu wa Richmond wakati akiwa madarakani,� alisema Bi. Maliwa.

Alisema Bw. Lowassa anapaswa kuwaomba radhi Watanzania kwanza ili kuonesha upendo badala ya kujifunika shuka nyeupe wakati ndani kuchafu.

Wakati huo huo serikali imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kusitisha mikataba yote na makampuni ya uzalishaji umeme ikiwemo IPTL na Songas ili fedha zinazotumika kulipa capacity charge zitumike kununulia mitambo itakayomilikiwa na serikali.

Umefika wakati wa serikali kukatisha mikataba mibovu inayowakamua Watanzania katika uzalishaji umeme hata kama ni kulipa fidia basi fidia ilipwe ili fedha zinazolipwa kila siku kwa makampuni hayo zielekezwe katika kununua mitambo yetu sisi wenyewe,

Kwa hii Watanzania tutakuwa radhi hata kama nchi itaingia gizani kwa miezi miwili mfululizo ni bora iwe hivyo, na katika kipindi hicho umeme kidogo unaozalishwa na TANESCO yenyewe uelekezwe katika maeneo nyeti tu ya uzalishaji, ili mradi tu baada ya muda mfupi tuwe na mitambo yetu wenyewe,� alisema Bw. Juma Shukuru.

Imeandaliwa na John Daniel Dar na Suleiman Abeid, Shinyanga

3 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... unajua dhambi inayomtesa kikwete - hadi sasa anaamini kuwa urais wake amepewa na mafisadi na mtandao wake and haujui kuwa alipewa madaraka haya na wanananchi wote -japo kwa uchaguzi wa mwaka 2010 (ameingia kwa wizi), namshauri athibitishe kwa sasa kuwa ni rais wa wananachi na si rais wa kulinda maslahi ya Lowasa, Karamagi na Rostam, naamini historia haitamlinda kama anavyowalinda akina Mkapa siku nguvu ya umma itakavyoamua kuchukua hatua
December 26, 2010 9:52 PM
blank.gif

Anonymous said... Tatizo kubwa tulilonalo Watz ni mkuu wa nchi ndio cheche. watu wanafikiri urais ni pambo la kutaka kujaribu usilojua na kupata sifa kwamba nami nishakuwa rais, kumbe cheo hicho ndio muelekeo sahihi au mbaya wa nchi. nchi yetu inaenda mrama kwa kuwa rais hana vision ya kilichompeleka ikulu. iko hivi, kikwete ajiandae kupanda kortini siku nchi hii ikichukuliwa na wapinzani. anatetea maovu kwa hiyo yeye ndie atakaewajibishwa.
December 26, 2010 10:44 PM
blank.gif

Anonymous said... +Watanzania sisi ni wazuri sana wa kusifia na kusahau.Kwenye kampeni tulimwimbia sana na tukasahau maovu yote aliyoyafanya.Cha muhimu ngoja tuendelee kuumia maaana zawadi zetu walishatupatia wakati wa kampeni,kanga kofia na soda.Na hali hii iendelee kuwa ngumu mpaka 2015 ili tupate akili.
December 26, 2010 10:59 P
 
Kwa maoni yangu hastahili kulipwa hata senti tano kwa sababu aliidanganya Serikali ili kupewa mkataba na pia alishindwa kutimiza masharti yote ya mkataba hivyo hastahili kulipwa.

~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*
'Mwenye Dowans atajwe kabla ya kulipwa'

Na Waandishi Wetu
Majira

SAKATA la malipo ya sh. bilioni 185 kwa Kampuni ya DOWANS iliyorithi mikoba ya kampuni hewa ya Richmond imezidi kuchafua hali ya hewa baada ya wananchi kumtaka Rais Jakaya Kikwete kumtaja hadharani mmiliki wa kampuni hiyo kabla ya kulipwa mabilioni ya fedha za walipa kodi.

Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti kutoka mikoa mbalimbali, wananchi hao wamesema wanasikitishwa na kauli ya serikali kukubali kuheshimu sheria kulipa Dowans fedha hizo wakati mmiliki wake hajulikani hadi sasa.

Tunataka serikali, hasa Rais Kikwete, atuonyeshe mmiliki wa Dowans, ajitokeze hadharani mbele ya vyombo vya habari tumfahamu. Haiwezekani nchi ikashindwa kesi na hewa, maana hadi leo hatujui mmiliki wa Dowans ni nani.

"Pia tunataka hiyo hukumu ipelekwe kwa Jaji Mkuu ili baadaye ilitolewe hadharani kwa vyombo vya habari tujue inasemaje,” alisema Bi. Catherine Maliwa wa Kigogo Dar es Salaam.

Alisema katika historia ya Taifa la Tanzania haijawai kutokea nchi ikashindwa kesi na mtu asiyejulikana na kuonya viongozi wa Serikali wanaohusika kutothubutu kutoa hata senti kulipa Dowans bila wamikiki wake kujulikana na kujitokeza hadharani.

Jambo linalotusikitisha ni kuwa Richmond ni Kampuni feki na wamiliki wake hawajulikani, iweje Kampuni feki ambaye mmiliki wake hajulikani kuuzwa kwa Dowans, mtalipa pesa mashetani?” alihoji Bi. Maliwa.

Alisema hivi sasa Watanzania wamechoshwa na viongozi wazembe wanaowabebesha mzigo wajane na maskini huku wahusika wakibaki salama na kufurahia maisha ya anasa kwa jasho lao.

Alisema baada ya hatua ya Rais Kikwete kumtangaza mmiliki wa Dowans na mwenye kampuni hiyo kujitokeza hadharani na nakala ya hukumu kukwekwa hadharani kwenye vyombo vya habari wahusika wote wachukuliwe hatua za kisheria suala la kulipa fedha hizo liwe la mwisho.

Mkoani Shinyanya wananchi walisema licha ya Mahakama ya Kimataifa ya kusuluhisha migogoro ya kibiashara (ICC) kuipa ushindi Dowand, utekelezaji hauwezekani hadi mmiliki wake ajulikane kwa Watanzania wote.

Walisema ni ajabu na mshangao kwa shirika la serikali kupelekwa mahakamani na mtu asiyejulikana huku baadhi ya viongozi waandamamizi wakionesha kwa haraka dalili ya kutaka kulipa adhabu hiyo kwa mtu asiyefahamika.

“Umefika wakati kwa Rais Kikwete abebe jukumu la kuwafahamisha rasmi Watanzania mmiliki halisi wa Dowans, itakuwa ni miujiza na aibu kwake kulipa fedha hizo kwa mtu asiyejulikana. Watanzania hatujawa wajinga kiasi hicho, kila mara serikali imekuwa ikieleza wazi kutomfahamu mmiliki wa Dowans,” alisema Bw. Fredy Mmassy.

Wananchi hao walihoji kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa serikali inaheshimu sheria na kwamba ikibidi haina ujanja zaidi ya kulipa mabilioni hayo kwa Dowans.

Rais atueleze na amtaje huyo mtu, vinginevyo Watanzania hatutokubali fedha hiyo ilipwe, na hata ikilipwa kwa nguvu waelewe iko siku tutaidai kwao, alisisitiza Bw. Mmassy.

Wananchi hao walisema mbali na Rais Kikwete kumtaja mmiliki wa kampuni hiyo pia awaeleze Watanzania mwakilishi wa serikali aliyeiwakilisha TANESCO katika mahakama ya ICC.

Walisema imefika wakati wa serikali kuweka wazi mkataba kati yake na kampuni hewa ya Richmond pamoja na ule wa Dowans ili kila kitu kifahamike na Watanzania wajionee wenyewe ni wapi TANESCO inapotiwa hatiani kabla ya fedha hizo kulipwa.

Katika hatua nyingine wananchi hao walimtaka Rais Kikwete kuangalia upya maamuzi ya TANESCO kupandisha bei ya umeme na kuweka wazi kuwa hali hiyo haiendani na maisha yao duni na umasikini uliokithiri.

Tunaomba Rais Kikwete kama kweli anawathamini Watanzania waliomchagua kwa moyo mmoja basi, azuie ongezeko la bei mpya za umeme, viongozi wetu wameonesha wazi kutokuwa na huruma na watu wao, wanakubali kulipa sh. bilioni 185 na kuongeza bei ya umeme,” alisema Bw. Masunga Jilaba, mkazi wa kitongoji cha Ndembezi mjini Shinyanga.

Hawa wana haki ya kufanya hivyo kwa sababu hawatoi hata chapa moja mifukoni mwao kwa ajili ya kulipia umeme, uchungu wataupata wapi? Ni Watanzania masikini wanaohangaikia hata mlo wao wa siku ndiyo watapaswa kulipa deni hilo la Dowans kupitia ankara za kila mwezi za matumizi ya umeme,” alisema Bw. Jilaba.

Wananchi hao walisema ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 18.5 ni dalili ya wazi kuwa wateja wa TANESCO ndiyo wanaopaswa kuilipa Dowans na kwamba hilo halihitaji mtu kuwa na elimu ya chuo kikuu kufahamu kuwa kampuni hiyo ni ya mfukoni na kuna watu wanafaidika nayo kwa njia moja au nyingine.

Katika hatua nyingine wanachi hao wamehoji kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Bw. Edward Lowassa, kwamba wananchi watangulize upendo kudai katiba mpya na kumtaka atafute kwanza upendo na huruma kwa Watanzania.

Najiuliza ni upendo gani anaounzungumzia, yeye anajua upendo tumeumizwa na mengi ikiwemo mikataba mibovu, kama angejua upendo nchi isingeingia katika mkataba wa aibu wa Richmond wakati akiwa madarakani, alisema Bi. Maliwa.

Alisema Bw. Lowassa anapaswa kuwaomba radhi Watanzania kwanza ili kuonesha upendo badala ya kujifunika shuka nyeupe wakati ndani kuchafu.

Wakati huo huo serikali imeshauriwa kuangalia uwezekano wa kusitisha mikataba yote na makampuni ya uzalishaji umeme ikiwemo IPTL na Songas ili fedha zinazotumika kulipa capacity charge zitumike kununulia mitambo itakayomilikiwa na serikali.

Umefika wakati wa serikali kukatisha mikataba mibovu inayowakamua Watanzania katika uzalishaji umeme hata kama ni kulipa fidia basi fidia ilipwe ili fedha zinazolipwa kila siku kwa makampuni hayo zielekezwe katika kununua mitambo yetu sisi wenyewe,

Kwa hii Watanzania tutakuwa radhi hata kama nchi itaingia gizani kwa miezi miwili mfululizo ni bora iwe hivyo, na katika kipindi hicho umeme kidogo unaozalishwa na TANESCO yenyewe uelekezwe katika maeneo nyeti tu ya uzalishaji, ili mradi tu baada ya muda mfupi tuwe na mitambo yetu wenyewe,” alisema Bw. Juma Shukuru.

Imeandaliwa na John Daniel Dar na Suleiman Abeid, Shinyanga
 
Kumbe nyimbo hizi za ufisadi watz wanazifahamu,lakini mbona wamekuwa mazezeta kuonesha hasira zao kwa vitendo?huu utamaduni wa kuwa mabwege na kulalama tu,tutauacha lini?kwa nini tunakubali kuburuzwa,kunyonywa,kunyanyaswa na wachache ilhali uwezo tunao?shime watz,tuondoe woga tupambane na hii mijitu kwa vitendo.Tujitokeze kwenye maandamano siku ikifika.
 
Gazeti la the CItizens la leo linasema.................."Tanzania can not avoid paying DOWANS"

Wakati gazeti la Majira lina nadiwa na kichwa cha habari kisemacho ya kuwa................."Mbivu na Mbichi za DOWANS kujulikana wiki ijayo"

The CItizens linaashiria ya kuwa AG kama tayari ameridhika na hukumu iliyotolewa na haiwezi kupingwa....hivyo malipo hayana utata....lakini majira linaonyesha ya kuwa AG tayari kamaliza kuipitia hukumu tajwa...........lakini hakuna uamuzi juu ya malipo tajwa.....................

Yupi ni sahihi kati ya the Citizen na Majira?

Lakini tupo wengi tunaoamini ya kuwa wale wote waliozuia mitambo ya DOWANS kinyume na sheria wanapaswa kufikishwa mbele ya sheria kwa tuhuma za criminal negligence..........na kulisababishia taifa hasara ya mabilioni bila ya sababu yoyote ile ya kimsingi....................na kwenye orodha hiyo ya kushitakiwa Dr. Idrissa Rashid aliyekuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Tanesco enzi hizo aongoze hiyo orodha ya washitakiwa pamoja na wasaidizi wake wa karibu.........kwa kulitia hasara nchi kwa kukusudia.................Walijua mkataba wa DOWANS ulikuwa umekwisha na ya kuwa hawadaiani nao sasa Tanesco walizuia mitambo ya DOWANS kwa sababu zipi?..........Hoja ya kuwa DOWANS walikuwa wanadaiwa na TRA haikuwahusu TANESCO na ilikuwa nje ya mkataba wao wahusika sasa waliamua kutafuna mfupa ulioishinda TRA kwa sababu zipi na kwa manufaa ya nani?

Haitoshi kabisa kwa AG kuzungumzia uharaka wa kuwalipa mafisadi ambao hata majina yao ya wamiliki wa DOWANS ni siri kubwa na huku watendaji ndani ya TANESCO na Wizara ya Nishati wakiachiwa waendelee kutesa huku wakisubiri mgao wao wa ujambazi huu dhidi ya raia wanyonge wa Tanzania................

Shame on everybody behind this debasing saga...............
 
Mbivu, mbichi za Dowans wiki ijayo

*Mwanasheria mkuu amaliza kupitia hukumu
*Waziri Ngeleja ajiandaa kutoa taarifa rasmi

John Daniel na Grace Michael
SIKU moja baada ya wananchi kuja juu na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kumtaja kwanza mmiliki wa Kampuni ya Dowans kabla ya kulipwa mabilioni ya walipa kodi, serikali imeahidi kutoa taarifa rasmi juu ya
sakata hilo wiki ijayo.

Kutolewa kwa taarifa hiyo wiki ijayo inatokana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredereck Werema, kukamilisha kupitia jalada la maamuzi ya Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara (ICC) na kuwasilisha mapendekezo yake Wizara ya Nishati na Madini.

Nimefanya kazi hiyo na nimeimaliza. Nimetoa maamuzi kuhusiana na kilichokuwemo humo ndani na nimewasilisha kwa Waziri wa Nishati na Madini, hivyo nendeni huko atawaeleza,� Jaji Werema aliwaeleza waandishi wa habari, Ikulu baada ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu Mohamed Othamn Chande.

Alipohojiwa zaidi kuhusu alichoshauri na 'kiu' ya wananchi kuhusu wamiliki wa Dowans, Jaji Werema alisema: Jamani msiwe mnaongea kama bata ebu itafuteni hiyo hukumu inaonesha kila kitu na wamiliki wa kampuni hiyo mtawajua humo hivyo katafuteni hukumu.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu, Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja alikiri ofisi yake kupokea jalada la ushauri kutoka kwa Jaji Werema kuhusu Dowans.

"Ninachoweza kukuhakikishia ni kuwa nimetaarifiwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameleta taarifa hiyo baada ya kupitia jalada husika.
"Ninawaahidi Watanzania kuwa serikali itatoa taarifa kamili juu ya suala hilo wiki ijayo, siwezi kusema zaidi kwa sasa kwa kuwa hata mimi sijapitia hiyo taarifa," alisema Bw. Ngeleja.

Alipoulizwa kuhusu uhalali wa madai ya sh. bilioni 185 za Dowans, Bw. Ngeleja alisema hawezi kuzungumza suala hilo kwa sasa kwa kuwa hajapitia jalada husika ili kujiridhisha.

"Nakuomba vuta tu subira, serikali itatoa taarifa kamili juu ya suala hilo wiki ijayo kama nilivyokwambia. Kila kitu kitajulikana wazi hakuna kitu cha kuficha, nipe tu muda," alisisitiza Bw. Ngeleja.Awali vyanzo vya vya Majira ndani ya Serikali na nje vilieleza kuwa malipo halisi ya Dowans si sh. bilioni 185 kama ilivyotangazwa awali na kwamba kiwango hicho kilipandishwa na wapambe wa kampuni hiyo kinyume na hali halisi.

Habari hizo zilieleza kuwa Jaji Werema ametoa ushauri mzito kwa serikali, ikiwemo kuwa makini zaidi katika mikataba na uvunjaji wake ili kuepusha nchi kuingia gharama kubwa kulipa fidia ya mabilioni ya fedha bila sababu.

Hata hivyo, Jaji Werema hakuwa tayari kuzungumzia kwa undani kwa maelezo kuwa yeye si msemaji bali mwanasheria na maadili yake hayamruhusu kusema lolote kwa kuwa hakutumwa kufanya hivyo.

Habari kutoka vyanzo vyetu ndani ya Serikali vilieleza kuwa malipo halisi ya Dowans kwa mujibu wa hukumu ya mahakama hiyo ni dola milioni 64 karibu sawa na sh. bilioni 90 za Tanzania.

"Katika hali inayotia mashaka taarifa ya ICC inasema madai ya malipo ya bilioni 185 kwa Dowans ni feki na yamepikwa na wapiga debe wa kampuni hiyo nje na ndani ya nchi kwa malengo wanayojua wao.

Malipo halisi yanatajwa kwa ni tuzo ya dola milioni 64.2, lakini wanasheria wa masuala ya usuluhishi wanasema hata hiyo tuzo ya milioni 64.2 si mwisho, bado TANESCO wanaweza kuirekebisha kupitia Judiciary Review katika Mahakama Kuu ya Tanzania," alisema Chanzo chetu.
Chanzo hicho kilisema wakati shauri hilo likiendelea katika mahakama hiyo jina la mbunge mmoja lilitajwa kama mwakilishi wa kampuni hiyo hapa nchini.

"Majina ya wamiliki wa Dowans haikutajwa, lakini aliyekuwa anaiwakilisha kampuni kortini alimtaja mbunge huyo kuwa ndiye mwakilishi wa Dowand nchini, ni jambo la kawaida katika biashara," kilisema chanzo chetu.Chanzo hicho kilidai kuwa tatizo kubwa iliyosababisha Tanzania kushindwa katika ushauri huo ni maandalizi hafifu ya mwanasheria aliyewakilisha TANESCO.

Ilielezwa kuwa mwanasheria huyo alienda katika shauri hilo akiwa na hoja moja tu ya 'mkataba wa kampuni ya Richmond iliyouzwa kwa Dowans usivyo halali' na baada ya kushindwa na upande wa utetezi hakuwa na njia nyingine.

"Katika mazingira haya ya sasa ni ngumu sana Tanzania kukwepa kulipa japo kiasi halisi kitakacholipwa si bilioni 185 kama ilivyotangzwa," kilisema chanzo chetu.

2 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Hebu tumuulize Asange atutengulie kitendawili hiki! cha nani haswa ni dowans, richmond, kagoda etc!
December 27, 2010 10:00 PM
blank.gif

JOJAS BRAND said... Mh.Rais JK,ninaomba sana utumie busara ulionayo katika kutatua tatizo la Dowans.Viginevyo utazidisha machungu makubwa sana kwa watanzania ambao wengi wao ni maskini wa kupindukia.
December 27, 2010 11:29 PM
 
Huyu ndiye mmiliki wa Dowans na atakayelipwa Sh.185 bilioni.
WanaJF.
Kwa kuzingatia sakata zima la Richmond na mchakato mzima wa kurithiswa Dowans, wananchi wasisumbue sana vichwa vyao kujua mmiliki wa mkampuni hayo hewa. Jibu rahisi la wamiliki wa Dowans ambalo halihitaji uchunguzi wala uchakachuaji. Mmiliki na kinara mkuu wa dowans ni Rostam Aziz. Na kwa taarifa yenu, huyo RA na wenzake tayari walishapeleka invoice Hazina hata kabla ya Mwanasheria Mkuu hajatoa tamko lake ya kuilipa Dowans. Aidha, RA na mafisadi wengine wanaishinikiza serikali ifanye malipo hayo kwa awamu, na kwa kuanzia wanataka walipwe chapchap Sh.10 bilioni.

Hivyo, suala la malipo ya Sh.185 bilioni ni mpango mahsusi ambao una mkono wa baadhi ya vigogo serikalini na CCM wasioitakia mema nchi hii kwa kile kinachofahamika kuwa ni kulinda cashflow ya mafisadi kwa lengo la kufanikisha mchezo mchafu wa kumpata “Rais wao” kwenye uchaguzi mkuu 2015.

Tujadili……..
 
Grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!!!!!NATAMANI NIMNYONGE RA KWA MIKONO YANGU KISHA NILE FIGO ZAKE.
 
Laiti Watanzania wangefumbuka macho kwa stail ya viongozi waliopo....HAKIKA ...VIONGOZi wangeburuzwa barabarani kama Samuel DO wa Liberia. Kwa taarifa tu haya malipo malipo ya Sh.185 bilioni ni mpango mahsusi wa baadhi ya vigogo na mafisadi kujiandaa na uchaguzi wa serikalini kwa lengo la kumpata "Rais wao" kwenye uchaguzi mkuu 2015. Sasa hapo ndipo WATANGANYIKA tulivyoliwa!
 
Mimi naanza ibada rasmi ya kuwaombea wote wanaohusika kwa makusudi kuidhulumu nchi yetu na watu wake ili waanze kupoteza matumizi ya viungo vyao muhimu katika miili yao. Siombi wafe, la naomba wapoteze nguvu za viungo kama miguu, mikono ili wawepo kushuhudia Mungu akiirejesha nchi mikononi mwetu. Kama wapo wanaotaka, waniunge mkono.
 
Inabidi tuchapishe mabango kama ya uchaguzi ili kuwaweka hadharani hawa akina ROSTAM,LOWASA NA CHENGE WAO,kwani ni watanzania wachache wanaopata fursa ya kusoma hizi habari hasa humu ndani ya JM, inabidi iwe kampeni kali kuliko ya uchaguzi ili kushinda ufisadi mimi nitatoa million 5 kwakuanzia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom