Mwakyembe na Sitta lazima wanajua majina ya wamiliki wote wa Dowans | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe na Sitta lazima wanajua majina ya wamiliki wote wa Dowans

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Anold, Feb 4, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,378
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Sakata la Dowans bado linaendelea, Watanzania kama kawaida yetu ya kuingizwa mkenge na kushikia bango kiasi cha kuamini mambo bila kuwa na uhakika na undani wa jambo husika bado tunajitahidi kujiridhisha na kuunga mkono wanasiasa kuwa kamwe Downs isilipwe. Kimsingi pamoja na kuwa jambo hilo la kulipwa Downs limeniudhi kwa kiasi kikubwa lakini nimeamua binafsi niulize wanaojua jambo hili kwa kina ili nisije kuwa mmoja wa watu waliounga mkono kitu wasichokijua undani wake na kuingia mkenge.

  Kwanza naomba niulize kuwa hivi inawezekana Spika mstaafu hata yeye hajui majina ya watu wenye umiliki wa Downs? Je Mwakyembe na timu yake waliopewa jukumu la kuchunguza sakata zima la Downs, katika uchunguzi wao hakukuwa na kipengele cha kuhakikisha wamiliki wote wa Dowans wanafahamika?

  Baada ya kamati ya Dk. Mwakyembe kuwasilisha walichokiona na kutoa mapendekezo yao Bungeni, Bunge lilipata nafasi ya kujadili hoja kwa kina kiasi cha kukubaliana na mapendekezo yaliyotolewa ya kuvunja mkataba na Kampuni ya Downs. Nijuavyo mimi baadhi ya wabunge ni watu waliobobea katika taaluma ya sheria na nilikuwa na imani kuwa jazba zile walizozionyesha wakati wa kuchangia hoja zilikuwa zimezingatia nguvu ya kisheria na hakuna madhara yoyote ambayo yangetokea kama mkataba wa Downs na Tanesco ungevunjwa kwa uharaka uliopendekezwa na kamati ya Dk. Mwakyembe, nimeweka neno uharaka, maana kwa mujibu ya maelezo tunayoyasikiasikia ni kuwa mkataba ule ulikuwa unakaribia kumalizika hivyo kama subra ingechukuwa nafasi yake huenda janga hili lisingetupata.

  Watanzania nilazima tuwe makini sana na wanasiasa wetu kwani inavyoelekea baadhi yao wameshasoma hisia za watanzania na sasa wanajaribu kutoa hoja au matamko ambayo wanafikiri yatakonga nyoyo za watanzania/wafadhili bila kuzingatia uhalisia wa jambo na ukweli uliopo hii yote ni kujiweka vizuri kwenye nafasi zao za kisiasa ili baadaye waungwe mkono na watanzania. Wanasiasa wengi wameamua kuziweka kando taluma zao na kutumia uwanja wa siasa bila kujali athari zinazoweza kuwapata wananchi kama tunavyoshuhudia hili sakata la Dowans.Ni bahati mbaya sana kuwa jambo hili watanzania tuliowengi hatulijui vizuri, viongozi wetu nao inavyoelekea hawalijui vizuri ndiyo maana ni mwezi tu sasa umepita ndiyo waziri wa nishati na madini wakati anaongea na waandishi wa habari ndiyo jana yake alisema ndiyo alipata kujua wamiliki wa downs ambapo bado watanzania wanaamini kuwa kuna wengine wamiliki muhimu hawakutajwa.

  Haya ni maswali magumu sana, japo majibu yake sidhani kama yangekuwa magumu kama jambo hili lisingegubikwa na usiri ambo si kamati ya mwakyembe wala msajili wa makampuni wameamua kutoweka wazi mambo hayo ambayo naamini kwa vyovyote wao wanaelewa majibu yake ila kutokana na sababu wanazozijua wenyewe wameamua kuegemea upande wa kisiasa zaidi bila kujivika ujasiri wa taaluma zao. Nijuavyo mimi aibu ya maiti anayeijua ni mwoshaji, Mwakyembe na kamati yake ndiyo waliokwenda kuosha maiti ambayo ni Dowans inakuwaje leo wakae kimya kujua maiti hiyo ilikuwa ni ya jinsia gani? Watanzania sasa wanajichanganya, wanataka kujua nani mmiliki wa Dowans cha ajabu hata waliokuwa wadau muhimu kwenye sakata hili ambao ni wanasiasa wamejiunga kwenye mkumbo huu ili kujaribu kujivua lawama. Wanasheria waliobobea nao wamekaa kimya huku wengine wakijaribu kutumia vyombo vya habari kupinga ulipwaji wa kampuni hiyo bila kutueleza bayana mgogoro wa kisheria unaotupa nguvu ya kupinga hukumu hiyo tunaupata wapi?

  Kwa vyovyote kuna wanasheria waliotuwakilisha katika kesi hiyo kwanini wasiwekwe kiti moto watujulishe watanzania mwenendo mzima wa kesi hiyo ulivyokwenda hata tushindwe? Je ni sababu zipi zilizowafanya waridhike na hukumu iliyotolewa bila kutoa pingamizi lolote? Wanasheria hawa ni watanzania kweli? Hayo ni maswali yanayonisumbua, pengine wana JF Mnamajibu mazuri ila tusipokuwa makini na tukaendelea kuungamkono na kushabikia mambo tusiyoyajua undani wake huenda tutaingizwa mkenge ambao naamini maumivu ni mara mbili ya haya tuliyoyapata.
   
 2. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  Si hao tu JK anajijuwa, EL anajijuwa............RA anajijuwa............. Pinda anawajuwa/anajijuwa................
   
 3. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  bana usinikumbushe.kumbe gesi ya Tanzania tunayotumia majumbani ni Imports?? DU na Songas wanafanya nini??? hii balaaaaa,, NASEMA SASA aLGERIA IKITOKA HUKO tANZANIA NASEMA HATULIPI dowani
   
 4. N

  Nsesi JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2011
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 374
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu, usizunguke, ujumbe huo mtumie JK kwani yeye ndiye lazima awafahamu
   
 5. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,982
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Jibu Mkuu soma Mwana Halisi ya Tar 9/2/2011 wahisika wote wapo hapo. Polisi Usalama wa taifa na TAKUKURU Wac hukue hatua tuu!!!!!!!!!
   
 6. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  mbona hata mm nawajua tena woteeeeeeeeee.....1.RA
   
Loading...