Al-Jazeera: Tanzania govt relocates its capital from the port city of Dar es Salaam to Dodoma

Waandishi wa habari Tanzania wengi wanatafuta penye maslahi, kama tetemeko la ardhi Kagera walishindwa ndio waweze kuandaa documentary ya kuhamia Dom?

Wenzetu mbele wameendelea, waandishi wao wanajua wanachokifanya. Huku kuna redio na TV hazizingatii taaluma bali tantalila zako tu na kujulikana.

Unategemea wamchukue mtu km Gigy Money akaandae documentary?

Kweli inasikitisha. Sio waandishi wa habari tu, tumekosa umakini karibu kila upande. Unfortunately!!! Ni kama hatujitambui
 
Makala nzuri. Natamani ingekuwa ndefu zaidi. Zaidi ya wafanyakazi wa serikali 28,000 kuhama Dar? Aiseeee. Hapa bado wale wa sekta binafsi wanaofanya kazi karibu na serikali kuu na taasisi zake. Kweli Dar itakuwa ya kipweke.
 
I don't think it is well balanced. Hakuna upande wa pili, kuna maoni ya Waziri na wananchi ambao wote wana support move ya serikali.

Nape, kwa mfano, hajabanwa aseme fedha zitatoka wapi, you know waandishi wa nje wakija kuripoti habari za third world na viwango vyao pia vinashuka, kiongozi wa nchi za nje akisema atafanya jambo fulani anaulizwa how, hela zitatoka wapi, hawezi ku get away na response ya "we will raise the money..." jibu rahisi sana hilo, uta raise funds vipi, utaongeza kodi, utapitisha michango au utalima nyanya? Na unaposema uta raise the funds ina maana uliamua kabla hujapata hela, ulikurupuka?

Halafu the whole story is upside down, imepinda, kuna mambo ambayo mwandishi wa Al Jazeera hawezi kuyajua ili atengeneza well balanced coverage.

Serikali, kwa mfano, imekuwa na a consistent push to de-centralize and expand the government, wanaongeza mikoa, majimbo, wilaya mpya, na zaidi sasa kuna sera ya e-government, lengo likiwa ni kusambaza the epicenter ya serikali.

Sasa leo Nape utasemaje dhumuni la kwenda Dodoma ni kwa manufaa ya administration? Yani utawala kukusanyika mahali pamoja. Inawezekana dhumuni la mwaka 1973 la kwenda Dodoma lilishapitwa na wakati.

Sasa mwandishi wa Al Jazeera hawezi kujua hizi sera na mipango mingine ya nchi kiasi cha ku cover story kama hii in a well balanced manner. Mtanzania angeweza, lakini bahati mbaya nchi hii hakuna mwandishi mwenye spine ya kusimama mbele ya a vicious attack dog jamii ya Nape Mnauye kumswalisha maswali.
Nakubaliana na wewe, kuna vitu vingi hakuvigusia, ila ni kwa sababu ya muda. Ila hii ni news tu na sio lengthy feature ambapo mleta habari anaingia kuliangalia suala la kuhama kwa undani zaidi kwa kuangalia hayo yote uliyoyahoji. Sidhani kwamba kwa yeye kutokuwa Mtanzania kumefanya asiweze fanya hivyo bali ni suala la muda. Ningependa kuona kipindi maalumu au documentary itakayo zungumzia hili suala kwa undani zaidi na kuangalia pande zote. Kipindi cha Kuelekea Dodoma cha TBC ingawa kinazungumzia mazingira ya Dodoma tu na utayari wake kuwapokea wafanyakazi wa serikali, kimejitahidi kuelimisha zaidi juu ya Dodoma.
 
Nimeona Nape anatiririka kimombo hapo. Ila jamaa wanafanya coverage nzuri sana hata huchoki kuangalia taarifa zao. Al- jazeera is my favourity news channel
 
Ila ss ni developing country wao wapo developed tyr tena kitambo...cc ndioo lazima tusue sue....baada tuje chekwa na wajukuu zetu tulivyo kuwa wazembe wa kufikiri
 
nawaheshimu waliopita for four form six hatimaye bachelor ya mass comm. na sio hilo tu tena ni creative in media industry wanagusa sector effectively including film directing, documentaries, media, technology etc
 
Tujitahidi kujikaza kuongea kiingereza kinachoeleweka hatuna ujanja kwani hii ni lugha ya dunia. Nashauri viongozi wa haswa serikali hii wafanyiwe brush up ya miezi sita ya kuongea kiingereza. Tusipoangalia tutashindwa kufanya argument kubwa kwenye mijadala mikubwa inayohitaji uwezo wetu wa kushawishi jumuhiya na mashirika ya kimataifa
Hahaha linmhusu waziri aliehojiwa,he could do better than that jmn
 
Leo nikiwa nimekaa mchana hapa naangalia Al-Jazeera mara nikaona makala nzuri kabisa ikiongelea serikali ya Tanzania kuhamia Dodoma.

Nilichoona na kujifunza na kushangaa ni kwamba mbona hawa watu wanakuja wanafanya makala nzuri namna hii na kitu kinachovutia kuangalia namna hii wakati huo sisi tukashindwa.

Ni hayo tu, ngoja niwape makala yenyewe.

======
Published on 6 Oct 2016

Tanzania’s government has started relocating its capital from the port city of Dar es Salaam to Dodoma.

The move aims to centralise government ministries after being scattered since the country gained independence more than 50 years ago.

But as Al Jazeera's Fahmida Miller reports, the project is not without its challenges.


Makonda anawatafuta sana mchana unaangalia TV..
 
Yaani Mtanzania akiongea English ni kama comedian khah! Mpaka muandaaji Wa documentary anatoa airtime ya sekunde tano tu and then anahadithia vizuri kilicho ongelewa na aliyeulizwa au kutoa maoni...

Kanifurahisha jamaa aliyefurahia kwa jamaa kuondoka yaonesha wazi misafara yao ni kero... Wajipange ati we have to raise the money.... Wakati Mkulu alisema fedha zipo..!
 
Wale wanaomsifia kingereza cha Nape kwenye hiyo clip,walahi inadhihirisha Lugha hile ni janga la kitaifa.Angalia manager wa cafe alichokuwa naongea 2 year .....3 year ndo nini
 
Kiswahili kifutwe shule za msingi maana kimetufanya tuwe wajinga tusiojua elimu haswa kiswahili liwe somo moja tu mengine yafundishwe kwa English mbona Rwanda wameweza baada ya kuchange from French to English na wamepiga hatua kuwafikia sio Leo na ushauri tunapata kutoka kwao... Unakuta kiongozi lina goma huku mitoto yake ipo English schools na wananchi ujinga unaongezeka
 
Wale wanaomsifia kingereza cha Nape kwenye hiyo clip,walahi inadhihirisha Lugha hile ni janga la kitaifa.Angalia manager wa cafe alichokuwa naongea 2 year .....3 year ndo nini
Nepi Utakuta kesha jisifia ebwana wee nimepiga ngeri acha kabisa nadhani Obama akisikia atanipa tano....

Na huyo meneja anajua kuuliza idadi ya vijiko vya sukari kwenye coffee... Maoni kwa ombo wapi na wapi kazoea kuelekeza washroom
 
kuna ma RIPOTA wa ITV ambao nikiweka CV zao humu utaomba ndimu ili usitapike
TV hiyohiyo kuna mtu wao anaripoti toka kule yalikotokea majanga Daaaaa!!ni shida aisee ile sauti tu utadhani kawekea kitu cha moto mdomoni halafu mdomo wameubana asikiteme acha kabisa.Nadhani hata elimu mmmmm!!
 
Back
Top Bottom