Al-Jazeera: Tanzania govt relocates its capital from the port city of Dar es Salaam to Dodoma

Tujitahidi kujikaza kuongea kiingereza kinachoeleweka hatuna ujanja kwani hii ni lugha ya dunia. Nashauri viongozi wa haswa serikali hii wafanyiwe brush up ya miezi sita ya kuongea kiingereza. Tusipoangalia tutashindwa kufanya argument kubwa kwenye mijadala mikubwa inayohitaji uwezo wetu wa kushawishi jumuhiya na mashirika ya kimataifa
Mkuu unamshauri nani hapo WABONGO!!!!!?? unapoteza muda kiingereza kwao ni ukoloni bila kujua kwamba hiyo lugha ni ya dunia na huwezi ukaikwepa,hapa ni unafiki tu.
 
Daah, kumbe English sio mchezo wa ukuti aisee!!

Nimemuona Nape anavyo struggle kutamka na kuunda sentensi mpaka nikajisemea kimoyomoyo......duu kumbe tuko wengi!!

Nakuuna mkono 100%
Jamaa mweupe kuongea hatar.
Tuendelee na vingeri vyetu vya kutongozea. Love u sweet heart!!
Hapo kila mtu fundi. Lakn wakija wazungu tuwe tunakula kona!!
Maana hii ni aibu
 
Waandishi wa habari Tanzania wengi wanatafuta penye maslahi, kama tetemeko la ardhi Kagera walishindwa ndio waweze kuandaa documentary ya kuhamia Dom?

Wenzetu mbele wameendelea, waandishi wao wanajua wanachokifanya. Huku kuna redio na TV hazizingatii taaluma bali tantalila zako tu na kujulikana.

Unategemea wamchukue mtu km Gigy Money akaandae documentary?
Huku tunaweza mambo madogo madogo kama Imooooooo
 
Watangazaji na marepota wetu wa TZ wanakosa credibility kwa sababu zifuatazo,

1. Wengi uelewa wao katika fani ya habari ni mdogo mno. (Huwezi walinganisha na wakenya)
2. Matumizi ya technolojia ya kisasa kwao baado kabisa (wanashindwa kwenda na wakati)
Mfano, mechi za TZ hawawezi kuweka hata summary ya magoli yaliyofungwa sson baada ya mechi, licha ya kuwa na
re-play za kila goli lakini mechi za ulaya wanaonyesha jinsi magoli yalivyofungwa.
3. Wanapeana kazi kwa misingi ya Dini (Utakuta TV moja watangazaji karibu wote ni wa dini moja) No competition, no
religious balance.
4. Wanapeana kazi kwa misingi ya Kabila - No credibility competition.
5. Ni washamba sana. Mara kwa mara mtangazaji anasoma karatasi. Kichwa chake ni up and down always!
6. Hawajui kuchangua nguo za kuvaa - Tazama TBC1.
7. Habari nyingi zina ukakasi mkubwa. mengi yanafichwa makusudi.
8. Hawana uzalendo wa nchi. i.e Hawajui namna ya kuitangaza nchi yetu.
NB: Mtu wa nje ya TZ anaweza kuitangaza vizuri nchi kuliko watangazaji wetu.

NAJUA SIJAPATIA YOTE LAKINI UKWELI NI MWINGI.

umeongea kweli tupu, ila kupendelea kuangalia habari za =kenya sio suluhu, Maana Kenya Mwandishi anathaminiwa zaidi kuliko sehemu zinginezo. wanalipwa fedha nyingi zaidi na kuthaminiwa sana!
Ndiyo maana napenda kuangalia TV za Kenya.
 
reporters wengi wa tanzania hasa tv,walikuwa wapiga picha za harusi,wengine walikuwa wanasagisha mashine za unga, ma mc wa harusi hivyo hawana elimu na weledi pia,

al jazeera hawapokei pokei habari tu,hata anayezitoa lazima awe na vigezo.

kuna ma RIPOTA wa ITV ambao nikiweka CV zao humu utaomba ndimu ili usitapike

Ulivyosema kama vile umemsema jamaa moja katikati ya nchi!
 
Back
Top Bottom