Al-Jazeera: Tanzania govt relocates its capital from the port city of Dar es Salaam to Dodoma

Waandishi wa habari Tanzania wengi wanatafuta penye maslahi, kama tetemeko la ardhi Kagera walishindwa ndio waweze kuandaa documentary ya kuhamia Dom?

Wenzetu mbele wameendelea, waandishi wao wanajua wanachokifanya. Huku kuna redio na TV hazizingatii taaluma bali tantalila zako tu na kujulikana.

Unategemea wamchukue mtu km Gigy Money akaandae documentary?
Wanahangaika mahakamani kuripoti "umahiri" wa Mwanasheria Yule Uchwara!
 
kweli kabisa , wafanyakazi wengi wa tanzania wanafanyia kazi njaa njaa tu wala hawafanyi kwa passion... unakuta mtu anasikia tu kuwa kazi flani inalipa siku hzi , basi ndio kukimbilia huko ,,,, jana nilishtuka kuja kusikia kuwa mzee muhogo mchungu eti nae sasa hvi ni mtangazaji wa radio east afrika
mkuu huyo mtu anatangaza kipindi gani?? hii sasa ni hatari!!
 
hatari,kuna haja TCRA iwalazimishe wawe na minimum number of graduates,na iwalazimishe wanaojihusisha na utafutaji habari wawe na minimum qualification kwenye mambo ya habari,may be form four na cheti cha journalism,awe repota au laa,kuna mmoja geita alikuwa mpiga picha za harusi,na kabla alikuwa msagishaji kwenye mashine za mpunga,mweusi tiii nafikiri kwa sababu ya zile mashine za enzi zile za dizeli
Ha ha ha haaaaa!! Mkuu ndoo huyu wa radio pendwa yenye watazamaji wengi kila ikifika 20:00???
 
mkuu huyo mtu anatangaza kipindi gani?? hii sasa ni hatari!!
kuna ripota.mmoja yeye hata kufunga vishikizo vya shati hajui,muda wote amelewa,anatamka maneno hayasikiki,usipokuwa makini unaweza kudhani umevamiwa na kichaa au kanjanja,yuko very rough hovyohovyo,anapatikana kanda ya ziwa
 
reporters wengi wa tanzania hasa tv,walikuwa wapiga picha za harusi,wengine walikuwa wanasagisha mashine za unga, ma mc wa harusi hivyo hawana elimu na weledi pia,

al jazeera hawapokei pokei habari tu,hata anayezitoa lazima awe na vigezo.

kuna ma RIPOTA wa ITV ambao nikiweka CV zao humu utaomba ndimu ili usitapike

Mkuu nimecheka sana
 
Leo nikiwa nimekaa mchana hapa naangalia Al-Jazeera mara nikaona makala nzuri kabisa ikiongelea serikali ya Tanzania kuhamia Dodoma.

Nilichoona na kujifunza na kushangaa ni kwamba mbna hawa watu wanakuja wanafanya makala nzuri namna hii na kitu kinachovutia kuangalia namna hii wakati huo sisi tukashindwa.

Ni hayo tu, ngoja niwape makala yenyewe.


Kwa hili la Aljezira kuitangaza Tanzania inawafanya hata wale wa mataifa mengine kuijua nchi yetu na mikakati yetu ya maendeleo, sio kutangaza mabaya tuu mfano njaa,magonjwa na mengineyo yasiyofaa.Karibuni mashirika mengine ya utangazaji ya kimataifa mje mfanye documentaries za kutosha kwa mema mengi yaliyopo nchini mwetu.
 
TATZO VITUO VYETU VYA HABARI HAVI AJIRI WATU WENYE ETHICS ZA KAZI MANA WENGI WAO NI BABA KANTUMA
 
Watangazaji na marepota wetu wa TZ wanakosa credibility kwa sababu zifuatazo,

1. Wengi uelewa wao katika fani ya habari ni mdogo mno. (Huwezi walinganisha na wakenya)
2. Matumizi ya technolojia ya kisasa kwao baado kabisa (wanashindwa kwenda na wakati)
Mfano, mechi za TZ hawawezi kuweka hata summary ya magoli yaliyofungwa sson baada ya mechi, licha ya kuwa na
re-play za kila goli lakini mechi za ulaya wanaonyesha jinsi magoli yalivyofungwa.
3. Wanapeana kazi kwa misingi ya Dini (Utakuta TV moja watangazaji karibu wote ni wa dini moja) No competition, no
religious balance.
4. Wanapeana kazi kwa misingi ya Kabila - No credibility competition.
5. Ni washamba sana. Mara kwa mara mtangazaji anasoma karatasi. Kichwa chake ni up and down always!
6. Hawajui kuchangua nguo za kuvaa - Tazama TBC1.
7. Habari nyingi zina ukakasi mkubwa. mengi yanafichwa makusudi.
8. Hawana uzalendo wa nchi. i.e Hawajui namna ya kuitangaza nchi yetu.
NB: Mtu wa nje ya TZ anaweza kuitangaza vizuri nchi kuliko watangazaji wetu.

NAJUA SIJAPATIA YOTE LAKINI UKWELI NI MWINGI.
Ndiyo maana napenda kuangalia TV za Kenya.
 
Back
Top Bottom