Al Huda, Sykes na Siasa za Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Al Huda, Sykes na Siasa za Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by August, Aug 13, 2009.

 1. A

  August JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,510
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Mimi ningependa kuwaomba wazee wangu Ali na Abbas Pamoja na Wahariri wa Al Huda na wasomaji wake, kwamba vita ya ufisadi si dhidi ya Kikwete au dhidi ya uislamu, na ndio maana sisi wengine tukiwa ni wakristo wa kweli au la tunamsema Mkapa , Lowasa na hata Sumaye na wengine walioleteleza nchi kuangamia namna hii etc, hivyo tunaomba tushirikiane pamoja ili tuweze kuishinda hii vita bila kuhusisha ufisadi na Dini, tukigawanyika ndipo mafisadi watakapo pata njia ya kutokea. Ninavyo elewa kuna wakristo/waislamu n wapagani wazuri na vivyo hivyo tunao wabaya.
  sasa nia yetu ni ipi kufanya ubaya kwa sababu upande wa pili nao ulifanya ubaya?
  nafikiri cha kufanya ni kurekebisha na inapowezekana kuadhibu kwa yule aliye fanya makosa. ili hatimaye tuweze kula hiyo Keki ya taifa vizuri kwa faida ya Vizazi vyetu, vya sasa na vitakavyo kuja.
   
 2. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  naona habari iko nusu nusu.tuweke wazi nini kimejiri?
   
 3. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,102
  Trophy Points: 280
 4. A

  August JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,510
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  kilicho jiri ni kwamba wamesema ni waislamu walio leta uhuru na ndio waliomsaidia nyerere, na wakamshutumu, nyerere kwa ufisadi aliofanya kwa kuwaweka ndani masheikh 1964/8 baada ya mmaasi ya jeshi 1964, na pia kumuhamisha sheikh moja usiku usiku kwa kutumia vyombo vya dola kumpeleka zanzibar, pili kuwaondo watu walio pigania uhuru na kuwapa madaraka watu wasio na uchungu na vita vya uhuru, zaidi wamemshutumu mama maria kwa kuto mshauri mwalimu kuhusu ufisadi aliofanya, pia kusema ufisadi ulifanyika awamu ya kwanza na ya tatu, yaani kipindi cha nyerere na mkapa, pili wameshutumu mali ya uislamu kuchukuliwa na serikali na mpaka leo hii haijarudishwa kwa mfano shule ya lumumba, na pia kushutumu kauli za baadhi ya viongozi wa ccm sasa wanaosemea mambo ya ufisadi na kuziona ni juhudi za kutaka kumwangusha kikwete, na pia kushutumu waraka wa wakatoliki, na kuziona kama ni juhudi hizi hizo za kumwangusha kikwte. sasa inawezekana nimeelezea isivyo au mwandishi wa al huda kapindisha kauli za hawa wazee etc. lakini kwa habari zaidi nende mjengwa.blogspot.com uka scroll down utaiona hiyo habari.
   
 5. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  kwani kuna tatizo gani wao kama raia kutoa mawazo yako?
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  inaelekea wewe unaptwa sana na mijadala ya kugombania uhuru

  thread zipo tele humu au ndio mambo ya flooding?
   
 7. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,102
  Trophy Points: 280
  maudhui ya makala hiyo ni kuwaziba mdomo Maria Nyerere na Malecela ili wasiendelee kukemea ufisadi. Makala imekwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa hawa (Malecela na Maria Nyerere) wanakemea ufisadi kwa kuwa ni wakristo na wametumwa na maaskofu.

  Waraka unataleta dhana ya kuwaficha mafisadi katika kichaka cha dini, kwamba kukemea ufisadi ni kuiangusha Serikali ya Kikwete ambaye ni Muislam. Pia makala inaeleza kuwa utawala wa awamu ya kwanza na tatu (Nyerere na Mkapa) ndo ulikuwa wakifisadi na ulihujumu Waislam.

  Makala hii ni bovu kuliko, ever seen like this...
   
 8. A

  August JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,510
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  tatizo langu sio mambo ya uhuru wala nini, bali ni utengano unaojengwa kupitia mambo yasiyo na haki , kwa mfano ufisadi ukifanywa au mtu akiwa dhaifu , basi aegeme kwenye dini ili imlinde au kundi la watu fulani watumie dini kulinda uovu wao, kwa waislamu kupigania uhuru au kuleta uhuru ni jambo jema na nipo proud of it, lakini sitakuwa na furaha wewe gt unininyeme keki ya taifa kwa sababu mimi sio miongoni mwenu? na hapa nilipoleta hii mada siiongelei on the basis ya nani kaleta uhuru ndio maana sijaiweka huko?
   
 9. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mimi hawa wakina Sykes wananishangaza! Hawa wakati ujamaa umebana ile mbaya ni peke yao waliokuwa na Travel Agency! Nakumbuka hata kadi za kuchanjia (Vaccination Certificates) zilikuwa zinatoka kwao. Hawa walikuwa ma-commission agents wa kwanza. Yote haya wakati wengine hata kufuga kuku walikuwa hawaruhusiwi! Leo wanamuona Nyerere mbaya? Mbaya kwa kunyang'anya shule pungufu ya ishirini za waislamu Tanzania nzima wakati kwa wamisheni wenzake alinyang'anya shule, vyuo hadi mahospitali makubwa (Bugando na KCMC)?

  Hawa wanaona ni wao tu watu wa pwani ndiyo waliogombea uhuru? Wanawasahau wakina Dr. Vedastus Kyaruzi na John Rupia ambao walikuwa mstari wa mbele hata wakati wa TAA? Au bado wana usongo na Nyerere kwa kumpiku ndugu yao Abdulwahid Sykes kuwa rais wa kwanza wa TANU? Mbona huyo huyo Nyerere alikubalika kwa wakina Mufti. Hassan Bin Amir, Sheikh Abdallah Chaurembo, Sheikh Nurdin Hussein n.k.? Bila shaka waislamu walikuwa wengi kwenye TANU ya mwanzo. Lakini hii sababu ya kusema wao ndiyo waliopigania uhuru peke yao. Mbona wasukuma hawatambi kuwa wao ndiyo watanzania pekee wakati ndio wengi? Na ukweli ni kwamba pamoja na wingi wao, waliweka udini pembeni, na kumchagua kiongozi ambae waliona atawafaa. Na kweli, akishirikiana na wakina Zuberi Mtemvu, Bibi Titi Mohamed, Rashid Kawawa na hao wakina Sykes na wakina Oscar Kambona, Stephen na Peter Mhando, Japhet Kirilo, Joseph Kimalando, Patrick Kunambi na wengine kibao ambao walitumikia lakini hawakutajwa, walitimiza azma yao. Ni kweli kuwa watu wa pwani walikuwa mbele katika yote haya lakini bila kukubalika na kuungwa mkono na watu wa bara (ambako wengi walikuwa wamisheni) huo uhuru usingepatikana.

  Hawa watu wazima wasitake kuandika upya historia kwa vijihisia vya kipuuzi vya udini. Nyerere aliwabeba sana na ni lazima wamshukuru kwa hilo. Hii sense of entitlement itawapeleka pabaya. Wasitake kuharibu walichojenga kwa machungu na kujitolea. Tuwakumbuke kama mashujaa wetu na si watu wanaotaka kutuvuruga. Walichofanyia nchi hii ni kikubwa mno na wasitake kuharibu kwenye hizi saa za magharibi! Mbona hawakusema yote haya wakati mwenyewe yupo hai?

  Amandla.........
   
 10. A

  August JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,510
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  in othewords walishalipwa ujira wao kwa kupigania uhuru, Abbas Balozi mpaka kajiuzulu juzi juzi tu, akapewa Board ya ATC na Plant and Equipment Hiring Agency (PEHACO) ambayo leo hii imekufa, Ali na hiyo travel Agency na Insurance, angekuwa na akili leo hii jubilee Insurance isinge tamba, kiwanda cha Soda tanga akakibadilisha kuwa Depot ya bia za Kenya. Sasa sijui walikuwa wanataka nyerere mpaka awapigie magoti au leo hii watanzania waelewe wao ndi wao hakuna wengine katika nchi hii?
  Hapa ndipo watu wanapo potoka au kama wana bifu na kina malesela au Maria wapeleke huo ugomvi wao huko huko, na sio kuharibu nchi. Lakini inawezekana mwandishi ndio kapindisha kauli yao kuhusiana na jambo hili, maana malengo yamwandishi yanaweza kuwa tofauti na malengo ya muhojiwa. naona Tanzania tunataka kuwa Kama Lebanono, wakati Misri na uislamu 90% wao wanaishi pamoja, sisi tulio changia ndio tunaendeshana puta. kwa Waafrika ndio tulivyo?
  GT ndugu ndugu yangu nategemea tutaendelea kuheshimia katika mambo ya msingi na kutembeleana si tunakuwa na Green Zone au Red Line. Ndio msingi wa thread yangu.
   
 11. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kwa bahati mbaya sidhani kuwa mwandishi amekosea. Haya maneno yapo muda mrefu na hapo yamepata platform. Kuna wengine humu waliishawahi kunishauri kuwa nikamsikilize Mzee Sykes ndiyo nijue ukweli kuwa waislamu ndio waliotukomboa isipokuwa Nyerere aliwachezea faulu! Hatari ni kuwa hawa wazee wanatumia ukweli kuwa walikuwepo wakati wengi wetu hatukuwepo wakati ule kutaka kuiandika upya historia! Wako ambao Nyerere aliwasahau lakini si wakina Sykes, Rupia, Mwapachu n.k. Wanavyomwandama sasa ni kumuonea.

  Amandla.....
   
 12. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,102
  Trophy Points: 280
  I love JF, asante Fundi Mchundo, umetoa maelezo yanayonikumbusha historia niliyokuwa nasimuliwa na babu, kiasi cha kusahau baadhi ya majina. Kweli JF tunavichwa vinavyokumbuka hata late 1950s. Thanks Mkuu.

  Ninachikiona ni kwamba hawa wazee wanafanya makosa sana kumshambulia mama Maria. Wanampa majonzi sana huyu mjane mzee, mama wa Taifa. Mama Maria ameeleza hisia zake juu ya nguvu ya mafisadi iliyopo sasa. Lakini wao hawajajibu juu ya haya mafisadi yanayotuumiza sasa, bali wanamshutumu kuwa hakuwa mshauri mzuri kwa mumewe!

  Pia Al-huda limewatumia hawa wazee kwa maslahi ya kidini zaidi. Ukiangalia kwa undani gazeti hili linalenga kuchochea ubaguzi wa kidini. Tena wameweka wazi kuwa utawala wa awamu ya kwanza na tatu (Nyerere na Mkapa) umewaonea waislam meaning that utawala wa Mwinyi na Kikwete umewafaa waislam. hii ni aibu tupu
   
 13. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  hao akina SYKES,their time has come and gone,there was a time when nyerere amebana private ventures wao aliwaachia wakawa miungu mtu,sasa biashara imekuwa katika a level playing field competition is forcing them into oblivion wanasema wamesahauliwa in the process wanajaribu ku rewrite history-kuna watu wanaweza lalamika but not them
   
 14. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Siamini kuwa Mzee Sykes amemnyoshea kidole Nyerere waziwazi hivyo. Hata hivyo itakuwa ni makosa kama kila mtu asiyekubaliana na UMASIHA wa kina Anna Kilango, Mengi, Kimaro, Mwakyembe and company basi ataonekana mpuuzi, mjinga, fisadi nk na wanaokubaliana nao ndio wazalendo na watu wema.

  Namuheshimu sana Mama Maria kwani ni wazi ndio anabaki kuwa alama pekee iliyobaki ya UTANZANIA ambao wengi tupo mbioni kuuvuruga. Hata hivyo amefanya makosa makubwa kujiingiza katika kundi la kina Mama Kilango na Mengi. Ingelikuwa vyema akatoa maoni yake sehemu nyingine na katika hadhira tofauti na aliyokuwepo.

  Kuhusu haya ya kuwa waislamu naamini waliokuwa wengi kuamini kuwa kelele za UFISADI na Waraka wa WAKATOLIKI ni mbinu za kumchafua KIKWETE hatupaswi kuzidharau na wala kuzikejeli hata kama zinaweza kuwa zisiwe za kweli lakini zimo miongoni mwa waislamu walio wengi na ni sehemu kubwa ya watanzania.

  Ni wajibu kwa wanaona tofauti kujaribu kuelewa ni kwanini baadhi ama walio wengi miongoni mwa waislamu hapa nchini wafikirie hivyo. Ina maana wao hawalioni tatizo la UFISADI? Ina maana wao wanapendelea UFISADI uendelee. La hasha. Ni historia.

  Kama ambavyo siasa za ubaguzi na kutumia vyombo vya habari walizotumia mtandao dhidi ya Salim, Malecela, Kitine, Sumaye na wengine zikakarudia na ndivyo ambavyo siasa za KUMMALIZA Ally Hassan Mwinyi wakati ule zinawala wale ambao wanapambana na UFISADI wa enzi hili. Kwa waislamu walio wengi ni vigumu kuona nia njema katika mapambano ya ANNA, ALOYCE, MWAKYEMBE, MAPUNDA, METHOD na wengine wanapopambana na UFISADI ambao ukweli ulishamiri sana wakati wa BENJAMINI ambaye sio tu hawakumpigia kelele enzi hizo lakini hata alipoondoka wakamfanyia sherehe maalumu za kuutangazia umma kuwa ni "mwenzetu". Hivi mmeshasahau misa iliyoongozwa na Mhashamu Pengo na familia ya MKAPA pale St Peters na baadaye ule uzinduzi wa kitabu cha mke wa LOWASSA miezi michache baada ya Lowassa kusimikwa rasmi ufalme wa UFISADI ndani ya bunge "tukufu".

  Katika hali kama hii ukijumlisha na historia ya ALLY HASSAN MWINYI ambaye alifikia hata kuambiwa ameoa mtoto wa shule(JK ameshapewa wake watatu hadi sasa), kila biashara mjini ni ya Mama Sitti (juzi nilikuwa Morogoro nikaonyeshwa hoteli naambiwa ya Mama Salma), mnategemea kutakosa waislamu wenye kushuku nia haswa ya hii vita ya UFISADI (sina uhakika kama ni vita dhidi ya ufisadi).

  Haya ndiyo mazingira ambayo Mzee Kingunge anashindwa kuwaeleza wazi anaposita kuingia katika mkumbo wa kucheza na "timu ya ushindi" katika suala la Waraka wa kiuchungaji wa kanisa la katoliki". Sio yaliyomo bali hali ya kisiasa na kijamii haindani na utoaji waraka huo.....Na kwa yeyote mwenye busara na uvumilivu ni rahisi kung'amua hilo.....

  omarilyas
   
 15. A

  August JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,510
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Sasa kutumia akili zetu si tumbane Mkapa au Lowasa kwa madhambi yao, si wamueleze Kikwete , bwana tatizo letu au haki itendeke kamata mkapa, kamata lowasa etc etc badala ya kumuacha asichukue hatua, au na yeye apitishe madili yake, tutakuwa tuna tatua tatizo au kukuza tatizo.
  Kwa sababu msingi wa matatizo mengi ya watanzania ni kutotendeka kwa haki sehemu nyingi na ufisadi wa mali na haki pia za watu. na hapa ni watu wa pande zote wapagani/waislamu na wakristo.
  Na kama ulivyo sema huamini kama wazee hao wamesema hivyo, ndio maana nami nikasema labda mwandishi au muhariri ameongezea yake.
   
 16. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mimi pia ni alama ya Tanzania,hajabaki pekee tupo sisi pia.
   
 17. S

  Shamu JF-Expert Member

  #17
  Aug 14, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Conservative thinking is a way to solve our corrupt government. Tuachane na fikra za KIJAMAA kuilaumu na kuitegemea Serikali kila siku. Kila mtu ajitegemee mwenyewe na Si kutegemea Serikali. Let the Free Market to solve our problem.
   
 18. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #18
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kaka nlikuwa ni maana ya kuwa Mama Maria anawakilisha taswira ya Mwalimu ambayo kwangu mimi naamini kuwa ndio nguzo pekee ya UTANZANIA ambao manyang'au wetu, wa ndani na wa nje wameshindwa kuibomoa hadi sasa.

  omarilyas
   
 19. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #19
  Aug 14, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nilidhani ukiongelea CONSERVATISM in Tanzanian sense unamaana UJAMAA? Huu ujinga wa mnachoita SOKO HURIA (Soko hovyovyo) haukufakamiwa miaka michache iliyopita? Una maana Tanzania ilianza na those dissastrous Washington made SAPs za 1980s to 90s ambazo hadi leo tunachezeshwa ngoma zake? Soma ushuhuda wa mmoja wa mitume ya SAPs kama Josef Stiglitz ujue ni jinsi gani mnajidanganya....

  UJAMAA is CONSERVATISM to TANZANIA....Zaidi dawa zote za corruption ya nchi hii ipo ndani ya maadili ya TANU na kurasimishwa na AZIMIO LA ARUSHA ambalo lilikuwa ni azimio la kujenga mfumo wa kijamaa ambao wasaliti wake wakuu ndio WAHUBIRI wakuu wa mnachoita SOKO HURIA...ama soko hovyohovyo...

  omarilyas
   
 20. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #20
  Aug 14, 2009
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo Mtandao kwa kutumia vyombo vya habari ulikuwa unawaonea wakristo? Kama jibu ni ndio, mbona kuna mchanganyiko wa dini kwa victims wa mtandao?
   
Loading...