omarilyas
JF-Expert Member
- Jan 24, 2007
- 2,130
- 145
Mimi nawachukia watu wanaoendekeza udini! kwani hapa msikitini au kanisani? nenda kwenye jukwaa la dini mkabishane haya mambo yenu.
Mimi binafsi nachukia sana. aliyokuwa anayakataa Nyerere ndiyo haya mnayaleta ya kuangaliana kwa misingi ya dini zenu na kujadili hoja kwa misingi ya dini zenu.
Iam sorry to say this lakini huwa wakati mwingine ninaona kuna upande una inferiority complex kwasababu ya dini yao. sasa tukijitizama katika hiyo misingi tutachukiana na tutashindwa kufanya kazi pamoja huku tukijiapiza kwamba watu wa dini hii watakuwa juu kuliko wa dini nyingine n.k utafikiri mna nguvu za kimungu.
Hebu jamani tupambane kupigania kuondoa umaskini katika taifa letu badala ya kuwa busy na mambo yasiyokuwa na tija.
Dini zinatusaidia kuishi maisha ya kumpendeza mungu hapa duniani kila mmoja katika imani yake lakini haipaswi kutumika kutugawa kwa misingi ya imani ya mtu.
I wish tungekuwa hatuweki thread za namna hii mahali kama hapa au kama zikiwekwa basi ziwekwe kwenye jukwaa la dini huko.
Labda sijakuelewa vizuri. Una maana kujadili UDINI ni kuendeleza udini?
Inaelekea wale makada wa CCM wanaolalamika kuwa kujadili ufisadi ni kuhatarisha usalama wa nchi, maslahi ya chama na kupoteza muda hawako pekee.
UDINI, UKABILA, UFISADI, UBAGUZI WA RANGI, CHUKI ZA KISIASA ni MAJANGA makubwa ambayo bila ya kujadiliwa kwa uwazi kamwe hayawezi kupigwa vita kwa umakini ambao utamsadia kumuondeleza mtanzania Kiuchumi, kisiasa, kijamii na hata kiimani.
Tatizo linakuja pale tu masuala hayo yanapojadiliwa kwa chuki, kejeli, dharau na usisi na uwao uliojaa prejudices....
Kuhusu huu muono kuwa kuna baadhi ya watanzania wana inferiority complex ni wazi kutakuwa na wenye kugubikwa na superiority arrogance ambao huwaona wengine kama inferior. Lakini pia usishangae kukuta hao unaowaona wana inferiority complex ukweli ni kuwa nao pia wana tatizo la superiority arrogance la kujiona kuwa mradi wao wana imani fulani ambayo wanaamini ndiyo imani iliyo bora na ya kweli basi wengine ambao wana imani tofauti ni lazima wawe inferior na wamepotea. Haya yote ni matokeo ya kimfumo kuanzia ngazi ya famili, jamii na kisiasa ambayo ni muhimu yakajadiliwa kwa uwazi, nidhamu na busara ili KUJISAHIHISHA na kujiepusha mabaya yatokanayo na JANGA kama hii la UDINI.
omarilyas
Last edited: