Mpango wa Kanisa ni kujenga 'informed conscience' ili waumini wake au wanajamii wachague kile wanachoona ni chema bila kujali dini, itikadi ya chama au kabila la mtu.
Kwa kifupi, Kanisa Katoliki linahamasisha waumini wake (na pia watu wengine) waweze kutumia kura yao vizuri (to learn how to vote responsibly) kuepuka kuwachagua viongozi wasiowajibika au wanaoweka maslahi yao mbele na maslahi ya nchi nyuma - tuchague viongozi wanaotupunguzia na sio wanaotuongezea umaskini, maradhi na ujinga.
Tunataka tuchague viongozi bora - wawe, Wakristo, Waislamu au waumini wa dini za asili - sisi hilo hatujali. Tunajali kiongozi bora na mwenye uchungu na nchi yake na huyo anaweza kuwa Mkristo, Muislamu au anayeamini dini za jadi au dini nyingine.
Kama viongozi wa dini hawawezi kuwajenga waumini wao katika haki, amani na upendo hata sioni kwa nini kuwe na sababu ya kuwa dini au dhehebu. Kwa hiyo, kwa mambo yanayojenga jamii ya Watanzania na kuwafanya waendelee, Kanisa lazima lishiriki (contribute to) kwa hali na mali katika kufanikisha 'that common goal'. Hiyo ni 'moral obligation'.
Kanisa lisiposhiriki (yaani kama wanakanisa) hawashiriki katika kuleta maendeleo au kupata viongozi bora (wawajibikaji) basi Kanisa au dhehebu hilo halimfai mtu yeyote.
Kinachokatazwa ni kupigia debe kundi fulani la watu kwa vile Kanisa ni lazima liwe neutral - linawahusu waumini wote (na pia kama watu wengine wataona ina faa, basi watu wote). Tuwe tunajaribu kuona kama kitu fulani ni 'constructive' au 'destructive'.
Mimi ni Mkristo, lakini nikisikia mahubiri ya Waislamu yanayonijenga, ninayafuata kwa vile ni 'constructive' yanatoka kwa Mungu na sitajali yamesemwa na nani. Lakini pia nikisikia mchungaji, padre au askofu fulani (ingawa ni muumini mwenzangu) anahubiri kitu ninachoona hakijengi, sitakifuata kwa vile nitaona ni 'destructive'.
Truth is never contained in a particular faith system; it's beyond that. Hivyo, let's affirm what's good even if it is said by people we do not share the same faith system.