Al-Huda inaeneza uongo dhidi ya Kanisa Katoliki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Al-Huda inaeneza uongo dhidi ya Kanisa Katoliki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magobe T, May 28, 2009.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Nimekuwa nikisoma gageti la Al-Huda lakini naona baadhi ya habari zake ni za uongo - hasa kama zinahusu Ukristo au Kanisa Katoliki. Huwa najiuliza kwa nini mtu mwenye akili timamu akae chini na aanze kuandika kitu anachoamini siyo kweli na ni kwa maslahi ya nani?

  Katika toleo Na. 281 (Alhamisi Mei 28-Juni 3, 2009) ukurasa wa mbele gazeti hili limeandika:

  KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2010...
  Kanisa Katoliki laanza mchakato kuweka utawala mpya Tanzania
  . Lapita nyumba kwa nyumba kuhamasisha
  . Ladai kutoa mwongozo kwa waamini wake

  Ukisoma habari hii, utaona ni mwendelezo wa upotoshaji ulioanzishwa na gazeti la The Sunday Citizen la Mei 3 mwaka huu. Katika ukurasa wa mbele wa The Sunday Citizen lilichachapisha 'story' kuhusu Kanisa Katoliki na kuipa kichwa cha habari ambacho ni 'twisted'.

  Kilisema hivi: 'Catholic church pushes for choice of next president' na kueleza: 'The Catholic Church in Tanzania has launched a comprehensive project whose aim is to influence the 2010 electorate process, and ensure that the country gets a leader of the Church’s choice.'

  Ukisoma kijitabu kinachozungumzwa na kile ambacho gazeti hilo lilitaka kieleweke kwa wasomaji na pia kile ambacho gazeti la Al-Huda linapigia debe ni vitu tofauti kabisa na nia na maelezo ya kijitabu/vijitabu vyenyewe au Kanisa lenyewe. For how long are we going to continue doing this?

  Kwa nini mwandishi/mhariri wa Al-Huda asisome hicho kijitabu au vijitabu kwanza kuliko kuendeleza uongo au kuna maslahi katika uongo? Pamoja na mambo mengine, moja ya uongo ulisomemwa na gazeti hili unaonekana katika 'quotation' iliyotumiwa na gazeti hilo na inaenda hivi:

  "In the last two years Council of Elders thrice met the President of Tanzania to press issues of common interest." Haya ni maneno gazeti la Al-Huda linasema limeyatoa kwenye tovuti ya Kanisa Katoliki na limeyatafsiri hivi: 'Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita Baraza la Wazee lilikutana na Rais wa Tanzania mara tatu kushinikiza masuala yenye maslahi kwa Kanisa.'

  Sasa, tafsiri ya 'issues of common interest' ni kweli 'masuala ya maslahi kwa Kanisa'?

  Nia ya chombo chochote cha habari ni kuielemisha jamii juu ya mambo yanayowahusu na kutafuta njia za kuyatatua (kama ni matatizo), kuyakabili (kama ni changamoto) na kuyandeleza (kama yanajenga) na siyo kusema uongo dhidi ya dhehebu au dini fulani.

  Watanzania lazima tubadilike. Dini maana yake ni chombo kinachoendeleza 'spiritual values' ili waumini wake wawe na imani na kutenda mema. Dini siyo chombo cha malumbano na tukitumia imani zetu kupotosha umma hatufanyi hivyo kwa sababu ya dini zetu bali ubinafsi wetu. Kuendelea kiimani au kijamii ni kupiga hatua katika ukweli, uwajibikaji, haki, kuunganisha watu na siyo kuwafanya wawe maadui.
   
 2. C

  CHANGA Member

  #2
  May 28, 2009
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Nakuwekeeni attachment ya Mpango wenyewe . sasa twaweza sema kama kanisa linataka kuweka watu wao
   

  Attached Files:

 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  mkuu asante sana kwa kutuwekea attachment hii.

  kanisa limeongea aina tofauti ya uongozi, ndani ya kanisa lenyewe na nje ya kanisa,

  waumini wanatakiwa kujua ni watu gani wanfaa kuliongoza kanisa na pia wapi wanafaa kuongoza jamii nzima ya watanzania.
  ni kweli kuna mambo mengi yametokea na kila mwenye akili timamu anajua kuwa kuna mahali mkuu wanchi alikuwa anasikiliza na kutolea maamuzi mambo ya kusikia bila kufatilia na kujua,(hii si sifa ya kiongozi bora).sasa kanisa linataka watu waelewe nani zaidi atafaa kuyatimiza yale anayoahidi kwa kuwajua viongozi vizuri na si kuchagua sura, pesa zao.
  anyway kwa jumla sikuona mahali ndani ya kijalida hiki kanisa limesema mwaka 2010 lazima rais atoke kanisa katoliki.
   
 4. C

  CHANGA Member

  #4
  May 28, 2009
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15


  Na huu ndio uzalendo ambao wote tunapashwa kuwa nao. Viongozi wa dini wana kondoo wao ambao ndio wanataabika na malisho yao. Ni vyema kila mojawao achukue initiatives za jinsi hiyo ili mwisho wa siku tupate viongozi watakaolinda malisho ya kondoo wao.
   
 5. I

  Isskia Member

  #5
  May 28, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  MwanaHALISI Toleo Na. 137 Jumatano Mei 20-27, 2009

  KANISA KUTIKISA JK 2010

  · LalEnga kubadili mwelekeo wa siasa

  · Labaini kasoro katika utawala

  Na Aristariko Konga

  KANISA Katoliki Tanzania limejipanga kuleta mabadiliko makubwa ya kiuongozi nchini, MwanaHALISI limebaini.

  Tayarai mpango wa kanisa umeanza na taarifa zinasema hatua ya utekelezaji iliyofikiwa hadi sasa ni ya kuridhisha.

  Mchakato wa kanisa ulioanza Januari mwaka huu unalenga mafanikio ya kwanza yapatikane katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaofanyika mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwaka kesho.

  Mpango wa kanisa umelenga kuamsha waumini na wananchi wote kwa ujumla ili washiriki katika kuleta mabadiliko makubwa ya uongozi wan chi, kuanzia vitongoji, mitaa, vijiji hadi ngazi ya taifa.

  Huu ni mpango shirikishi wa iana yake unaolenga kutoa elimu juu ya uongozi bora, viongozi bora na jinsi ya kuwapata wawakilishi sahihi wa wananchi.

  Mchakato wa Kanisa ambao tayari umechapishwa kaitka vijitabu mbalimbali, unalenga upatikanaji viongozi bora mwaka kesho, lakini unafanya maandalizi ya uchaguzi wa 2015 kwa vile tathmini ya hatua ya kwanza inakamilika mwaka 2011.

  MwanaHALISI imepata vitabu hivyo mahusis kwa mpango huo ambavyo vimetolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), vyenye ratiba ya utekelezaji hadi 2011.

  Ratiba ya mpango huu iliyobeba kichwa cha “Mpango wa Kichungaji Kuhamasisha Jamii Kuelekea Uchaguzi” ineleza pia kuwa “Mungu alimpa binadamu wajibu wa pekee, siyo tu mlinzi na mdhamini wa dunia… bali pia kuwa mshiriki katika kuumba na kutunza.”

  Kanisa linasema kuwa katika miaka ya hivi karibuni limegundua matatizo mengi ya uongozi ambayo yanahitaji kujadiliwa na kutafutiwa tiba.

  “Uongozi unahitaji watu wenye sifa ya huduma, wanaojali, waliowazi, wanaowajibika, wanyenyekevu, wenye hekima na upendo… Lakini uongozi kila mara unashwaishika kutenda kinyume na hayo na kuwa na uchoyo na kutumia madaraka vibaya,” linaeleza kanisa.

  “Uongozi unahitaji watu wenye sifa ya huduma, wanaojali, waliowazi, wanaowajibika, wanyenyekevu, wenye hekima na upendo… Lakini uongozi kila mara unashwaishika kutenda kinyume na hayo na kuwa na uchoyo na kutumia madaraka vibaya,” linaeleza kanisa.

  .

  Katika kijitabu kingine CPT wametoa “mada za kuongoza maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2010,” ambazo ni Uongozi Mintaarafu Ufunguo wa Mabadiliko nchini Tanzania, na Vipaumbele kwa Misingi ya Mafundisho ya Kanisa kuhu Jamii.

  Mada nyingine ni Mfumo wa Kisheria Tanzania: Mapengo na Changamoto zake, Haki za Binadamu katika Sera za Biashara na Fedha, Hifadhi ya Jamii, na Mtazamo wa Kimaadili katika Mfumo wa Siasa na Uchumi.

  Katika mada ya Uongozi Mintaarafu, kanisa linasema viongozi lazima waaminike na wawajali watu, kwa kuwatendea haki na siyo kufukuzia mali na utajiri na kwamba fikra na taratibu mpya zinahitajika kuwezesha umma kushirika katika kufanya maamuzi.

  “Hatujajipanga kujiongoza, ila kwa ushawishi wa watu kukubali yale wataalam na viongozi wa kisiasa wanavyoamini ni mazuri kwa ajili yao,” kanisa linaeleza.

  Kama ratiba hiyo ya Kanisa Katoliki itatekelezwa kama ilivyopangwa, na wananchi wengi wakafikiwa na kupewa elimu hiyo, kuelekea uchaguzi mkuu wa 2010, basi kunaweza kutokea mabadiliko makubwa ya safu ya uongozi wan chi mwaka ujao.

  Mpango huu unadhihirisha kuwa kuna mambo ambayo yatakuwa yamewashtua maaskofu wa Kanisa Katoliki na hata viongozi wengine wa dini.

  Mchakato huu unaweza kuleta mabadiliko ambayo pengine historia ya nchi hii haijawahi kushuhudia tangu uhuru, kama ratiba ya kanisa itafuatwa na kutekelezwa kikamilifu.

  Ratiba inaonyesha ilianza kutekelezwa Januari mwaka huu kwa Baraza la Maaskofu (TEC) kufanya mkutano wa Taifa kwa kutengeneza program na wahusika walikuwa wakurugenzi wa kichungaji na wajumbe wa Tume ya Haki na Amani.

  Kazi ya kukamilisha program katika mfumo wa vijitabu ilifanyika Februari na mpango wa kutuma mpango huo kwenye majimbo ulitekelezwa Machi, walengwa wakiwa maaskofu, wakurugenzi wa uchungaji, majimbo na viongozi wa Tume ya Haki na Amani wa majimbo.

  April mwaka huu kulikuwa na mikutano ya kila jim bo la kuzindua program, walengwa wakiwa mapadre, watawa, halmashauri na vyama vya kitume na taasisi. Walionza ni mapadri na watawa, wakfuatiwa an walei.

  Semina kwa ajili ya wale na vyama vya kitume katika ngazi ya parokia zilianza mwezi huu na zitaendelea hadi Juni. Walengwa ni halmashauri zinazojumuisha viongozi wa jumuiya ndogondogo, vyama na kamati ya ngazi hiyo.

  Programu itafikishwa katika jumuiya ndogondogo kati ya Julai na Septemba na walengwa watakuwa waumini na wakazi. Wasimamizi wa kazi hiyo ni paroko na halmashauri ya parokia.

  Oktoba hadi Desemba 2009 kutakuwa na mijadala na utekelezaji katika ngazi ya jumuiya ndogondogo na vyama vya kitume. Wasimamizi watakuwa paroko, kamati ya utendaji na viongozi wa jumuiya hizo.

  Mkutano wa Taifa wa tathmini ya kwanza ya uelimishaji wananchi utafanyika Januari 2010, miezi tisa kabla ya uchaguzi mkuu kwa kushirikisha wakurugenzi wa kichungaji na wajumbe wa Tume ya Haki na Amani.

  Februari hadi Septemba 2010 kutakuwa na mwendelezo wa mijadala na utekelezaji, vinavyolenga waumini na wakazi katika majimbo, parokia, jumuiya ndogondogo na wananchi kwa ujumla.

  Hatua hii ndiyo itaongoza hadi uchaguzi mkuu ifikapo Oktoba 2010. Mkutano wa Taifa wa tathmini ya pili ya mpango huu utafanyika Januar 2011, ili kubainisha ajenda baada ya uchaguzi.
   
 6. N

  Nzinyangwa Member

  #6
  May 28, 2009
  Joined: Aug 27, 2008
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sawa, wewe unalalamika juu ya upotoshaji, je wewe una maoni gani kuhusu mpango huo. Hebu tupe uchambuzi kidogo kuhusu yaliyomo. mimi nimesoma na ninaendelea kutafakari kwa kina. Je huku si kuchanganya dini na siasa?
   
 7. C

  CHANGA Member

  #7
  May 28, 2009
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Ni vyema kama unaendelea kutafakari. sasa sijui hilo swali ni nama ya kuomba tukusaidie kutafakari au ndio jibu la tafakari yako. Siasa ni itikadi na dini Je? Kama nayo ni itikadi then vilikwishachanganyika siku nyingi kabla ya Mpango wa Pengo!
   
 8. I

  Isskia Member

  #8
  May 28, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Unajua kuna watu wengine labda wana zile chuki za ndani ya damu, sababu Alhuda ndio wameandika ndio kwa upande wake upotoshaji, Je Mwanahalisi je? nadhani itakuwa ni uelimishaji sababu ni gazeti la kira raia, Ni bora tuwe tunatafakari saana kabla ya kutoa.
   
 9. C

  CHANGA Member

  #9
  May 28, 2009
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mwanahalisi imetoa kilichopo kwenye mpango huo tu, sioni wapi inapotosha
   
 10. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Mi nakushukuru sana mdau,
  Nchi yetu ni masikini wa kutupwa pamoja nakwamba tunapotoshwa mara kibao na watawala(sio viongozi) wetu kuwa uchumi wa nchi unapaa kwa kasi ya ajabu, hivi ni vichekesho na wachekeshaji(watawala) wanapata ujasili wa kuchekesha kwa kuwa tu wanaochekeshwa wanacheka bila kujua wanachochekelea.Kumbe uchumi umepaa matumboni mwao na katika familia zao.Haya yote ni matokeo ya mfumo mfu wa uchumi wetu ulioegemea kuwalinda wala nchi(wachukuaji maana sijaona mwekezaji hata mmoja).Haya yote ni matunda ya utawala mbovu(unaohubiriwa kuwa utawala bora katika lugha ya kuchekesha).Tungekuwa na uongozi wanaoweka mbele maslahi ya Taifa na watu wake hakika tusingekuwa hapa tulipo(MIAKA ZAIDI YA 40 BAADA YA UHURU).Bado hatujapata MTANZANIA HALISI(yaani Mwana Halisi wa Tanzania) anaeweza kusikitikia umasikini wetu,shida zetu,dhiki zetu,ufukara wetu nk.Tunataka kiongozi ambaye yuko tayari kuleta maendeleo ya wote,ambaye hayuko tayari kufichwa ndani ya mifuko ya mafisadi,ambaye yuko tayri kudaiwa maendeleo,ambaye anaujasili wa kutamka kuwa nikishindwa kuwaletea maendeleo msinichague tena(japo hii inaweza kutokea tu katika nchi ya kusadikika),mwenye machungu ya kwelikweli. Ndio maana kwa Mtanzania anaeona mbali na mwenye uchungu na nchi hii na mwenye maadili mema kama alivyo Mchungaji au Padre haishi bila kujiuliza kwa nini sisi ni masikini kiasi hiki.Tatizo la msingi linabakia kuwa UONGOZI MBOVU usiojali.Kwa nini tunakuwa na uongozi mbaya usiojali?Ni kwa sababu wanaochagua hawana elimu nzuri juu ya nani anafaa kuwa kiongozi.Katika nchi kama ya kwetu ambayo wale maadui wetu wakubwa watatu wa kudumu (umasikini ,ujinga na maradhi) hawajaondoka na hakuna dalili ya kupungua achana na kuondoka ,ni vyema Wanajamii wakapewa japo elimu ya namna ya kupata viongozi kwa maendeleo yao na kama inavyotarajiwa.Katika nyanja za kijamii Hakuna umakini ulio bora zaidi kama umakini wa mtu kuweza kumchagua kiongozi anayefaa.
  Inasikitisha kuona baadhi ya vijarida vya magazeti(kama al-huda) vinataka kuupotosha umma wa watanzania kuwa Kanisa Katoliki linaandaa viongozi kwa ajili ya 2010.Huu ni upuuzi mtupu,hapa ieleweke kuwa Kanisa haliandai mtu wa kuongoza nchi linaandaa watu namna ya kuchagua viongozi na hii ni kutokana na sababu nilizoziainisha hapo mwanzo.Tunacho taka ni maendeleo na maendeleo yatakuwepo tu iwapo uongozi utakuwa imara na uongozi imara utapatikana tu iwapo wanaochagua wana elimu kama hiyo.Tuangalie tulipofikia sasa tuangalie tumejikwaa wapi kama kuna mashimo ambayo aidha tulikuwa tunayaona lakini tukayafumbia macho ama hatukuyaona wakati tunapita basi tuyafukie upesi kabla hali haijawa mbaya zaidi na kukiathiri kizazi hiki na kijacho.
  Wadau Tuwekeni kando mambo mambo ya Dini tuwekeni mbele mambo ya mustakabari wa taifa letu.
  Naamini nimesomeka.

   
 11. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Alhuda sio wa kwanza kuindika habari hii kwanini umeliandama Alhuda tu? Na umenyamazia Mwanahalis, the sundy citzen? watu kama wewe ndio mnaoiletea sifa za udini jf na kuonekana ni kijiwe cha wakristo!
   
 12. A

  AbbyBonge Member

  #12
  May 28, 2009
  Joined: Apr 2, 2009
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unauhakika gani kama hii taarifa ni mwendelezo wa The Sunday Citizen ? na mbona huja hoji kilichoandikwa na Mwana halisi toleo la Mei 20??

  Wanachoongea Al-Huda kina ukweli maana hiyo ndo DINI-SIASA
   
 13. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,705
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kama unaona JF ni kijiwe cha wamisheni haulazimishwi kuwepo. Lakini usitake kutuletea uongo ili kupandikiza udini huo huo unaojifanya kuukemea!

  Amandla..........
   
 14. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #14
  May 29, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  .kijiwe cha wa misheni
  Wabaguzi
   
 15. A

  AbbyBonge Member

  #15
  May 29, 2009
  Joined: Apr 2, 2009
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haondoki mtu lakini ukweli ndio huo, mmeanza kuleta thread za kidini humu ndani!!

  Baada ya mtu kuongelea ukweli anatumia muda mwingi kuonyesha chuki zake binafsi na Al-Huda kisa haliandikwi na wamisheni... mtu mbaya sana huyu.....imetoka wapi mbegu hii mbona si ya kitanzania?
   
 16. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #16
  May 29, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kingekuwa cha wamisheni wewe ungapata nafasi ya kutuma hii post isiyo na kichwa wala miguu? Yaani kwa sababu mtu mmoja kaanzisha thread wewe lawama zako unazipeleka kwa MODS na wanaJF wote (wewe mwenyewe ukiwemo!). Lahaula la kwata..

  Mtu anayeongozwa na chuki, maarifa na busara humkimbia.
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  May 29, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kama The Citizen na Al Huda zote zimepotosha taarifa, huoni kuwa al Huda (gazeti la kidini) lina mchango na wajibu mkubwa zaidi wa kuleta taarifa sahihi kwa waumini wake? Je, hujui madhara ya upotoshaji yanayoweza kufanywa na gazeti la kidini? Msiwe mnapayuka bila kutafakari na kuleta sentensi za jumlajumla.
   
 18. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #18
  May 29, 2009
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mimi huwa sishangai baadhi ya uandishi katika baadhi ya magazeti !!
   
 19. C

  Chuma JF-Expert Member

  #19
  May 29, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Jifunze kuandika kwa Paragraph....Tafuta Kozi fupi usome!!!
   
 20. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #20
  May 29, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  .
  Haondoki mtu hapa! Tutawaeleza hata ukichukua! @Abdlhalim?? Wacha kujipendekeza. Yaliyo Vifuani.....
   
Loading...