Akina mama na matusi kwa watoto wao

Akina mama na matusi kwa watoto wao

Kila kitu kina msingi wake
Ukifuatilia hao kina mama hawakuwa na malezi mazuri ndio maana anaona kutukana mwanae na kama kumuonya asiendelee kufanya alichokuwa anakifanya bila kujua kuwa anamjaza mabaya mwanae na huyo mtoto akiwa na wenzake hutukana hivyo hivyo na yakishazoeleka anakuja kutukanana na mama yake hadharani.
Tuangalie malezi tuwapayo watoto wetu
 
Dah kweli kabisaa yani hapa ninajirani yangu anaongea balaa sasa mwanae amkere mama wee hiyo mitusi utaskia ku..ba..bako m..s..e..nge mkubwa wee! Dah hapo pengine baba mtu yupo ndani kimyaaa yani naonaga aibu kama nimetamka mimi vilee naingiaga ndani kimyakimya! Sasa mi huwa najiuliza incase huyo mtoto kakurudishia hiyo mitusi ama katukana wenzie utamchapa??

Then watoto huwa wanacopy sana na yeye akienda kucheza anayatoa matusi yale yale kwa watoto wenzie, sio tabia mnzuri kwa kweli wamama tubadilikeni.
 
Kwa kweli si tabia mnzuri kuna wamama wana midomo michafu kwa watoto wao yaani mpk unajiuliza kwani amezalia nn,kuna siku moja mama mmoja alimtukana mwanae wa kiume 'mbwa wee'yule mtoto alimjibu mama yake kama mm mbwa basi we jibwa , mzazi alikaa kimya kwa aibu

Kuna mitoto imekubuhu kwa mitusi aisee. dah.
 
Sasa ukimtusi huyo mtoto stress zitaisha?
Ni kuwatwisha mizigo isiyowastahili tu watoto na kuwafanya wakose staha nao.
Kuwa mama kunaambatana na mengi ikiwemo kuhakikisha stress zako za maisha haziwaathiri watoto.
A Real Mama speaking!
 
Ukiona mwanamke anamtukana mtoto jua hajitambui na uwepo wa mungu kwake hakuna na ukichunguza utakuta ndoa yake ina matatizo cos anaongea mbovu mbovu hat mbele ya mumewe..
 
Tabia hii ipo sana mikoa ya pwani hasa hasa uswazi.chanzo ni mimba za utoton,kuzaa m/watoto bila kuwa tayari. kibaya zaidi kuna maneno waambiwayo yanawaumba!
halafu sasa watu wenyewe wa uswazi huwezo wa kusoma michango kama hii ni anasa kwao.
 
Last edited by a moderator:
Sasa ukimtusi huyo mtoto stress zitaisha?
Ni kuwatwisha mizigo isiyowastahili tu watoto na kuwafanya wakose staha nao.
Kuwa mama kunaambatana na mengi ikiwemo kuhakikisha stress zako za maisha haziwaathiri watoto.

Asante sana kwa ujumbe mzuri

Hebu shushia na huu wimbo ..........

Last edited by a moderator:
Karucee mada safi sana hii...

Wajua wazazi tunawahusudu na kuwadhuru watoto kwa midomo yetu wenyewe utakuta mzazi anamwita mtoto wake maluuni au mshenzi unategemea mtoto awe vipi?

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
maji hufata mkondo wake...kama mama kakulia maeneo ambayo matusi ni mitajo ya kawaida tu,atamtukana na mwanae vile vile

hii tabia iko kila mahali
 
This weekend nimegundua dawa mpya ya hangover bana
 
Stress za maisha, unakuta moyo umejaa, sina hela, nadaiwa kodi gari mbovu matengenezo yake ni milioni mbili, term ya kwanza mtoto ndo imeisha akifungua nafaiwa ada, huku mkwe anaumwa kumuuguza, huku nyumba nnayojenga haijaisha, mlo wa kazini wa kubangaiza na kujidai unafanya diet kumbe hela huna wenzio kila siku wanakyla lynch za elf sita kwenda juu, sasa kichwa hiko halafu mtoto home anakwambia mama tumefunga shule lakini natakiwa hela ya tuition na hapo ripoti yake kafeli wee lazima wabwatuke, huku na huku house girl katoroka. Mie siwatetei as niko single ila nimewaza tuu wanayoyabeba vichwani mwao mmmhhh sjui kama ntaweza!! Hapo tena hujakutana na mmama mumewe hana kazi weeeh hiyo mineno inayorushwa ndani ya nyumba usiseme.

Looh, ndio umtukanie alikotoka kama strees c zako.!!! Tunapaswa kuwalea watoto vzr bila visingiziol
 
Kuna wanawake wana matusi jamani

Anamwachia mwanae tusi zito kali hadi roho inakusisimka

Halafu mwisho wa siku watoto wanaiga,

Ndo unakutana na katoto ka miaka 3 anakuachia tusi hadi unapata kizunguzungu

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Stress za maisha, unakuta moyo umejaa, sina hela, nadaiwa kodi gari mbovu matengenezo yake ni milioni mbili, term ya kwanza mtoto ndo imeisha akifungua nafaiwa ada, huku mkwe anaumwa kumuuguza, huku nyumba nnayojenga haijaisha, mlo wa kazini wa kubangaiza na kujidai unafanya diet kumbe hela huna wenzio kila siku wanakyla lynch za elf sita kwenda juu, sasa kichwa hiko halafu mtoto home anakwambia mama tumefunga shule lakini natakiwa hela ya tuition na hapo ripoti yake kafeli wee lazima wabwatuke, huku na huku house girl katoroka. Mie siwatetei as niko single ila nimewaza tuu wanayoyabeba vichwani mwao mmmhhh sjui kama ntaweza!! Hapo tena hujakutana na mmama mumewe hana kazi weeeh hiyo mineno inayorushwa ndani ya nyumba usiseme.
nakubaliana na wewe ila kuna sisi wa uswahilini hata hiyo gari au kusomesha wototo hakuna ila ni Mama Lishe aua muuza Genge la Samaki.
Chanzo ni hao watoto kwanini tunazaa wengi km ulishabugi na mume wa kwanza akaja wa pili makosa ni ya nani?
Kumtukana Mwanangu matusi mazito mbele ya kadamnasi ni lazima nayeye akikua atajua ni halali kabisa kuapayuka
Na kosa kubwa ni pale Mzazi mwenzio aliyekataa kuishi pamoja anapotaka kukusaidia mtoto kwa malezi ni lazima utawaharibu tu watoto km ni mtu wa matusi.
 
This weekend nimegundua dawa mpya ya hangover bana
Du Kaka umnikumbusha Karucee wangu leo kaja kivingine kabisa maana kawa mpole na kutukanya kabisa leo hana Hang-Over
Nakumbuka story zake za kuwa Konda wa Daladala au ile ya mjamaa kuupanda mnazi kule beach kwa ajili ya NDUMU
acha mchezo km unatumia kuna ma2 ikupande uwatukane mpaka wanao au ikupe HangOver week-end yote iishe KIPI BORA?
 
Last edited by a moderator:
Halafu kina baba wamekaa kimyaaa. Ama sijui hangovers hawajaamka? Ngoja niwaite one by one.
Ntuzu, Eiyer, Eliphaz the Temanite, dogo Excel, Eli79, OLESAIDIMU, kobun mtzmweusi

hizo ndizo mbegu wanazopanda akina mama kwa watoto wao!

watoto nao wanakua kulingana na mafunzo ya mama zao bila kujali ni mema ama mabaya..

mbegu nyingi hizo ndizo zinazofanya kazi mpaka sasa, mtoto mdogo tu anaishi maisha ya kiutu uzima kabisa mf. watoto wa kizaramo..
 
nilichogundua si kila anaeenda labour basi ni mzazi o mlezi wa mtoto, kulea mtoto ni zaid ya kwenda labour. Utakuta mtu anatukana kama wanatukanana mateja halafu nawe tukuite mkubwa kisa umezaa puuuuu. Halafu mtoto akiwa na matusi tunampiga kisa sie wakubwa. Nachukia hiyo tabia zaid ya neno lenyewe la kuchukia. Lets change kwa kweli
 
wakina mama wengi hawajitambui halafu hawajui kama maneno huumba mtoto ukimtukana hata tusi dogo la mfano mjinga na ukiwa unarudiarudia hata shuleni atakuwa jinga jinga tu
 
Back
Top Bottom