Akina dada, wanaelekea wapi? Tunaoa artificial women???

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Kwa siku za karibuni, tumekuwa tukishuhudia teknolojia ikikuwa kwa kasi ya ajabu na sasa inaonekana kuwaathiri dada zetu kwa kasi ya ajabu sana. Kuna dawa siku hizi zimeingia za kuwanenepesha wadada makalio (kuongeza hipsi), zipo za kupunguza/kuongeza matiti, zipo za kupunguza tumbo na sasa zimeingia sasa za kusimamisha matiti.

Nashawishika kufikiria beyond the box, endapo mi kijana nimepata mchumba mwenye makalio ya bandia (yametengenezwa na mchina/mganga wa kienyeji, matiti katengenezwa hapo sinza (au kwa cosmetic surgery) (machine ya kunyanyua titi yawa gumzo dar-gonga hapa), tumbo limekarabatiwa na Monalisa sliming belt (au dawa za kimasai), rangi ya ngozi ni ya bandia maana imekarabatiwa na cream za dubai/malaysia/china/USA etc! Sasa hapo nina mke kweli?

Swali langu ni je tunaelekewa wapi? Hivi tunajua madhara ya hizo kemikali na hizo sayansi za kubadili maumbile?
Na wanaume tutakuwa tunaoa nini, wadada wa kuchonga? Tutapona kweli na kansa? Na watoto tutakaowazaa je? Hawatakuwa na kasoro?

Nina waheshimu dada zangu sana na kuwapenda na si kusudio langu mada hii ieleweke tofauti, lengo ni kusikia maoni yenu juu ya sayansi hizi za kubadili maumbile na madhara yake kwa watoto wetu tutakaowaza!

Wenu,

HorsePower
 
HP akili za kuambiwa changanya na za kwako
Hapo macho yako yatumie vyema na kama ni miwani ongeza lensi kabisa uangalie kwa makini
Wenye akili wanajua mwanamke wa kuoa ni yupi
 
ndo maana mpapokuwa na uhusiano kuna kuchunguzana....
hamuamki asubuhi mkawa wachumba au mke na mume.....

kingine wakulaumu ni wewe mwenyewe.....
kama unapenda makalio hips sijui matiti itakula kwako.......

uzuri wa mwanamke ni tabia sio urembo........

ukitafuta mwenye tabia njema utampata na mkichunguzana vyema utampata asiyetumia hayo madawa/teknolojia ya urembo......ila ukikurupuka kutafuta wowowo na hips utapata wa kichina

 
Si ndio mnavyotaka wakina kaka, kwahiyo kila biashara lina soko lake. Ingekuwa mnatupenda hivi tulivyo original tusingefika huko.
 
sema nikupe binti zangu akina cantalisia, husniyo, mwali wote ni
orginal, kuanzia nywele hadi kwenye nyayo za kutembelea, achana
na hao wa kichina.
 
Nadhani ni ufinyu wa mawazo tu walionao baadhi ya wanawake. Wengi wao hawataki kujikubali vile walivyo. Nadhani hakuna mwanamke mbaya, isipokuwa ni kujitambua na kujikubali tu! Haijalishi wewe umepigwa pasi au mweusi, believe me kuna mwanaume atakupenda sana tu jamani. Maintain what God gave you! Sipendi kabisa wanawake wanaomkosoa Mungu aliyewaumba!Mwe HEBU MIKUBALI VILE MLIVYO NDO MTAPENDWA ZAIDI OTHERWISE WANAUME TUTAISHIA KUWAMEGA NA KUWAACHA!Katika kujenga familia wanaume hutafuta (mke) na sio (mwanamke).
 
jamani mbona mnachakachua thread? Lengo ni kuchambua sababu ya wadada kujibadilisha na madhara yatokanayo na hiyo tabia.
Thanks
 
ndugu, mungu atakupa wa kufanana na ww, ukiwa fake utapata fake ukiwa original mungu atakupa huyo huyo original!
 
ndugu, mungu atakupa wa kufanana na ww, ukiwa fake utapata fake ukiwa original mungu atakupa huyo huyo original!

Nimezungumzia kwa ujumla wake, sijamahanisha kuwa nina mke wa namna hii. Kikubwa nilipenda tujadili hasara za hizi teknolojia kunusuru vizazi vya sasa na baadaye.
 
Nimezungumzia kwa ujumla wake, sijamahanisha kuwa nina mke wa namna hii. Kikubwa nilipenda tujadili hasara za hizi teknolojia kunusuru vizazi vya sasa na baadaye.
utandawazi ndo unatusumbua na atuwezi zuia tekinologia ndani ya nchi yetu cha msingi kila mtu amuelimishe nduguye madhala ya artificial na kujikubali alivyo.
 
kazi kwenu wakaka mnaopenda fake........................... bado mengine yanakuja, lol!
 
Back
Top Bottom