Akina dada, mtafanya mauaji haya mpaka lini?

Ni ipi haki ya Fetus?

Kuzaa kama nguruwe ni dhambi kubwa na inagharimu sana jamii!

Ni heri kutoa mimba kuliko kuzaa mtoto akaishia kuwa YATIMA!
 
Aliye nizaa mimi alikua na miaka 15 that time,std7
pamoja na purukushani zote hakutoa mimba (ambayo ndo mimi huyu),...
alistrugle mwenyewe,jana kafikisha 39years na last year kachukua masterz yake!

Nimegundua humu kuna watu wametoa mimba nyingi sana,ili wapate peace ndani ya mioyo yao wana jaribu kutetea abortion!
Aisee..mama yako ni mwanamke wa shoka.Heshima mbele!
 
Yeye alifukuzwa kwao kabisaaaa,na hata limtu lilo mpa lilimfukuza!
Lakini mbona alivumilia?

Swala ni kuwa tayari kubeba matunda ya matendo yako,..
kubadilisha,...
tutaongea hapa hadi dunia iishe,lakini labda watakao badilika ni wachache wanao weza kusoma humu!
Huku duniani watu wana nyofoa watoto kama wanafumua nywele vile.

kuna mtu namfahamu,mwanachuo katoa zygotes mbili mwaka huu,...huyu nae kashindwa nini kutunza au?
anatoa kwa sababu anapewa ushauri na watu kama maty wasio penda kuona watoto wanaishi

Mimi nilipata kashkash kuliko alizopata mama yako na nina binti mkubwa tu na ninamfurahia binti yangu wa utotoni nimemtunza vizuri na anasoma vizuri tu. We unadhani tunachangia humu hatuna watoto tuna watoto tena wa mimba zisizotarajiwa
 
Ni ipi haki ya Fetus?

Kuzaa kama nguruwe ni dhambi kubwa na inagharimu sana jamii!

Ni heri kutoa mimba kuliko kuzaa mtoto akaishia kuwa YATIMA!

Mtoto kua yatima anajua Mungu peke yake na anajua ataishi vipi!
Hiyo sio sababu ya kutoa mimba kabisaaaaaa
 
Mimi nilipata kashkash kuliko alizopata mama yako na nina binti mkubwa tu na ninamfurahia binti yangu wa utotoni nimemtunza vizuri na anasoma vizuri tu. We unadhani tunachangia humu hatuna watoto tuna watoto tena wa mimba zisizotarajiwa

Itabidi nimtafute huyo mrembo,unaishi wapi mama mkwe wa muda?
 
Kabla ya kumega huwa natoa tahadhari mapema kuwa bwana usije ukaniambia una mimba yangu jukumu la kuzuia mimba hiyo ni lako mwenyewe kwa hiyo anaelewa mapema. Wadada wengi wanapata mimba kizembe zembe
Mkuu wewe huwa unachukua tahadhari kabla ya hatari lakini hata hivyo mwisho wa siku baada ya kugonga TBS kwa binti mtoto si ni wa kwako au ndio utataka uende kupima DNA kwa mkemia mkuu wa Serikali
 
Itabidi nimtafute huyo mrembo,unaishi wapi?

Nakushangaa unaongea tu ukidhani watu tunahalalisha utoaji mimba, tunakataa kunyoosheana vidole as if huyo mtoa mimba ndio ana makosa sana, na binti yangu ni mrembo hasa tena hasa na nilipigika kuliko maelezo mpaka sasa nimesimama sawa sawa we unazungumza nini? watu tumepata mateso sababu ya watoto kama kumtoa basi ningetoa ile mimba.

Sasa niko nafurahia maisha tukiongozana kama mtu na mdogo wake kila saa napenda kukaa nikimtazama tu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Naomba niwe mkwe wako basi mama,nimempenda binti yako (mrembo) ghafla!
 
Nakushangaa unaongea tu ukidhani watu tunahalalisha utoaji mimba, tunakataa kunyoosheana vidole as if huyo mtoa mimba ndio ana makosa sana, na binti yangu ni mrembo hasa tena hasa na nilipigika kuliko maelezo mpaka sasa nimesimama sawa sawa we unazungumza nini? watu tumepata mateso sababu ya watoto kama kumtoa basi ningetoa ile mimba.

Sasa niko nafurahia maisha tukiongozana kama mtu na mdogo wake kila saa napenda kukaa nikimtazama tu.

Hongera zako Mummy!
YouTube - Whitney Houston - Greatest love of all
 
Mamangu amenizaa akiwa na miaka 15,..
alikua hajapanga,na wakati wote wa mimba yake aliteswa kwa limtu lilo mdanganya na kumpa sababu ya umaskini wake.
alifukuzwa kwao....
alikuwa house gal na huko usumbufu ni uleule.....
alishauriwa kutoa aka kataaa,....
Mimba yangu ilikua haija pangwa,....
angetoa leo ningekua wapi?

Yawezekana hujapanga kumzaa mtoto,ila Mungu ana plan nae na ameona wewe unaetaka kutoa unafaa kumleta duniani!
Shiiiit,...

Dah, haya maneno yako kaka yameniliza.
Yamenikumbusha jambo fulani hivi.........
Ila, ni Neema tu inawezesha mama kama mama yako kuwa na moyo kama alioku/alionao lakini kwa kweli, hili swala ni gumu sana.
Kuna jirani yangu mmoja, binti yake alibeba mimba akiwa form two, binti ni mdogo kwa umri na kwa umbo pia, yani unaweza ukatamani ardhi ipasuke uingie ukiwa kama mzazi.......................Naomba tu nisesema sana kilichoendelea lakini yule mtoto anaendelea na shule na wala hakuzaa huyo mtoto........................sasa hebu tufikirie mazingira kama haya, na vitoto vyetu na tamaa za dunia hii ya utandawazi, na hawa Mafataki waliojaa kila kichochoro cha dunia hii.

Ni jambo ambalo ukilifikiria kwa mapana na marefu unaona kabisa ni changamoto isiyokuwa na majibu ya haraka haraka katika jamii yetu.
Kama alivyosema Mwanajamiione hapo hapo juuuu!!!!!!!!!!!
 
Speaker mimi na wewe tunazungumzia kitu kimoja kwa lugha na mitazamo tofauti...............nakubali kabisa si vizuri kutoa mimba, ni dhambi na tunapaswa kuishi kwa matendo yetu ........lakini itatusaidia nini kama tunaacha mazalia ya mimba zisizotakikana na kukemea utoaji wake? (Tuangalie maadili na namna ya kuyarudisha)

Unatolea mfano wa mama yes mama was very brave kwa hilo ana stahili pongezi lakini wangapi wenye ujasiri huo?? Binti wa miaka kumi na nne amepata mimba..mpaka amfikie mtu atakaye mshauri vema ameshapitia makundi mangapi ya wajuzi watakaomwonyesha njia rahisi ya kuepuka aibu na kukatishwa masomo?? Tuanze na kurekebisha mafiga kabla ya kusubiria sufuria itenguke ndo tukazane kuzuia chakula kisimwagike. Hilo ndilo neno langu
 
Dah,najenga picha hiyo!
Lakini in any way,...mimi si-support kutoa mimba labda kama mimba hiyo itasababisha mama matatizo kama kupoteza maisha ni reasonable kutoa!
 
Kweli kabisa usemayo MJ1, Kuna kiini ambacho kinatakiwa kufanyiwa kazi.............manake hiyo kutoa ni matokeo ya mambo mengi sana.

Na hatutakiwi ku-support hata kidogo.....
Lakini kuna changamoto iliyopo katika hili Speaker, Tuache kwanza sababu za kiroho.......ujasiri na neema ambayo mtu anaweza kuwa nayo wkati anapita katika hayo majaribu na akiweza kushinda anashinda.

Hebu jaribu kumsoma MJ hapo juu vizuri, halafu fikiria uhalisia wa swala zima la utoaji mimba, angalia makundi yote watoto, vijana, wanandoa wasio kuwa na ndoa, wanaobakwa, wanakataliwa.........tena hiyo hiyo historia ya mama yako unadhani ni kwa sababu mama aliweza kukuhifadhi tu? Hapana, mi naona hapa kuna mkono wa Mungu na Neema kubwa sana, USIOMBE kukataliwa na mimba kaka angu.........bila Neema huu wakati ni mgumu sana.
 
Uko wise sana,..
Sina maneno zaidi
 
Inashangaza na kushtusha kuona baadhi ya watu "wacha mungu", kwa namna moja ama nyingine kuunga mkono utoaji mimba.

Sidhani kama kuna mtu anayemcha Mungu anaunga mkono kutoa mimba........
Kusema tu Mungu hapendi kutoa mimba kwa wakati tulio nao sasa haitoshi kuzuia utoaji wa mimba........
Siku hizi injili inahubiriwa kila mahali, makanisa yamejaa kama nini ya majina tofauti tofauti achilia mbali Misikiti lakini bado tatizo la utoaji mimba lipo tena ni changamoto kubwa sana ktk jamii hii ya utandawazi. Kitoto cha miaka tisa, kumi na moja, na mbili wanapata mimba, mzazi wake ana uwezo, ana heshima yake katika jamii kinachofuata hapo wazazi/mzazi anampeleka kutoa/anamtoa hiyo mimba ili mwanae aendelee na shule.........

Achilia mbali hilo kama umemsoma MJ1 vizuri kuna sehemu anasema huyu mtoto wa miaka kumi na mbili anapopata mimba mpaka aje akutane na wewe utakaye mshauri kutoa mimba ni dhambi atakuwa amekutana na washauri wengine wangapi??????

Hili swala halipo rahisi kiivyo katika uhalisia wa jamii yetu, tunahubiri sana makanisani, lakini kila siku tunaona na kusikia utoaji wa mimba. Hata humu tunaona mtu anaweka thread eti, nilikuwa na DEMU/GIRL FRIEND wangu bila kinga na ilikuwa hivi na hivi je hii mimba anayosema itakuwa ya kwangu kweli????

Fikiria binti aliyekuwa na mtu anayeleta thread kama hii, hiyo mimba ataipeleka wapi, na mtu mwenyewe anamwambia sina uhakika na hiyo mimba???? Tusemeni yote lakini kusema tu MUNGU hapendi binafsi sioni kama tutakuwa tumetatua hili tatizo......................

Kuna kiini (Root) ambayo ni zaidi ya maisha ya kiroho..................
 
Tuwe wakweli, msituponde tu wanawake.
Binti wa form ii kapewa mimba, kesho yake hana mimba. Je ni nani kampa mimba? Je ni nani kampa hela ya kwenda kutoa?
Hivi kwanini baadhi ya nyie akina dada anaua watoto mliowatafuta kwa starehe zenu? Mtu unajiachia mwenye tena bila kinga yoyote, then ukipata mimba unatoa, je hamjui kuwa hapo anafanya mauji ya viumbe vya MUNGU? Kama hampo tayari kuzaa, kwanini mnajiachia bila kutumia hata lady pepeta? Wazazi wenu wangezitoa mimba zenu, nyie mngekuwepo hapa duniani? Inaniuma sana kwakweli!!!!!!!!!!!
 
Kweli kabisa usemayo MJ1, Kuna kiini ambacho kinatakiwa kufanyiwa kazi.............manake hiyo kutoa ni matokeo ya mambo mengi sana.

Na hatutakiwi ku-support hata kidogo.....
Lakini kuna changamoto iliyopo katika hili Speaker, Tuache kwanza sababu za kiroho.......ujasiri na neema ambayo mtu anaweza kuwa nayo wkati anapita katika hayo majaribu na akiweza kushinda anashinda.

Hebu jaribu kumsoma MJ hapo juu vizuri, halafu fikiria uhalisia wa swala zima la utoaji mimba, angalia makundi yote watoto, vijana, wanandoa wasio kuwa na ndoa, wanaobakwa, wanakataliwa.........tena hiyo hiyo historia ya mama yako unadhani ni kwa sababu mama aliweza kukuhifadhi tu? Hapana, mi naona hapa kuna mkono wa Mungu na Neema kubwa sana, USIOMBE kukataliwa na mimba kaka angu.........bila Neema huu wakati ni mgumu sana.

Unajua LD hili ni swala refu sana........I just wish watu wangeelewa kuwa its not just a matter ya kumnyooshea binti au msichana why unatoa mimba..............hivi do you really think kuwa watu hawajui kuwa kutoa mimba ni dhambi???? Watu wanajua sana but kuna sababu............sasa hizo sababu ndo sie tunatakiwa kuziaddress ndo tuweze kudeal na mimba but si kukemea utoaji wa mimba wakati mazingira ya upatikanaji mimba bado tunahalalisha........
 
  • Thanks
Reactions: LD

Similar Discussions

Back
Top Bottom