AKILI ZA MTU MWEUSI: Kuchangishana sherehe (kadi za mwaliko na magroup )

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,013
12,277
Hizi ni nyuzi special kuelezea akili za mtu mweusi, naanzia hapa.
Akili za mtu mweusi season1.
ep 01 :
Kuchangishana pesa kwenye raha binafsi za watu( hizi wanaita sherehe za harusi, ubatizo, birthday n.k )

* Kuna huu ujinga unaoendelea kwenye jamii zetu wa kuchangishana kwenye furaha binafsi za watu pesa kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao.

* Imefika hatua wajinga wanakusanya michango kama vile ana kudai, ni mwendo wa kukufuatilia kila uchwao ili tu umsaidie pesa ya kuendeshea huo upuuzi wake sijui ndoa, birthday na ujinga mwengine.

* Kuna watu wanavuka mstari mwekundu mpaka anakuunganisha kwenye magroup ya WhatsApp ili mpige zogo humo za namna gani mtapush upuuzi wake anao panga kuufanya.

* Kadi sasa hapa ndio kuna ujinga mwingi sana imekuwa kama kitambulisho cha taifa kwamba lazima uchukue na utie kiasi tajwa huu ni ufala wa level ya juu sana.

* Sherehe za harusi, ubatizo, birthday, vipaimara n.k hizi zote ni raha binafsi sio mchongo kutaka marafiki, ndugu, watu wa karibu, watu unao juana nao, majirani kukuchangia kwenye raha zako binafsi unazo taka fanya.

* Fanya vitu kwa uwezo wako usiwape shida jamii kuuwazia upuuzi wako namna gani ya kuupush.

NB: Hizi akili za namna hii kwa watu weusi inabidi zikome mara moja na najua kuna majitu humu huu uzi umewagusa kwa sababu ndizo akili hizi zimejaa vichwani mwao.
 
Mm sipati shida kuchangia hasa kama mtu namjua tumeshibana ila kinachonipa ukakasi iweje nichangie alafu kwenye furaha ya mtu mimi nipate karaha nishindwe kuwa huru. Unachangia sherehe ya mtu mkwanja mzuri tu ila unafika kwenye sherehe unaanza kuomba vinywaji chakula kimepoaaa haya mambo yananifanya sikuhizi mtu akinipa kadi naiangalia naiweka pembeni. Sikuchangisha mtu na sikuwa na mambo ya kamati na jambo langu lilienda kwanuwezo wangu ila kutaka kuonyesha dunia ufahari kwa michango ya mtu ni ufala wa kiwango cha lami
 
Kuna watu wakikupa kadi utajutaa

Kila baada ya masaa kazaa sms ya kawaida inaingia kukumbushia mchango..ukiwasha data Whatsapp nao ujumbe unaingia Kwa kawaida na Kwenye group la harusi napo anakumbushia Bado cm Kila baada ya cku mbilii aiseeeee n fedheaaa
 
Upuuzi nilishaachana nao miaka miwili iliyopita. Nikipewa kadi za send off, harusi na upuuzi mwingine unaofanana na huo sichangi hata shilingi. Kuoa mbona easy tu? Kwa nini usumbue watu wakuchangie wakati unaoa/kuolewa, wakati mnakutana na kukubaliana sisi tuliwaona? Mi mwenyewe nikioa sitasumbua watu wanichangie ni kusumbua watu na ni aibu. Kwa nini ufanye harusi kwa kutegemea mifuko ya watu? Unaweza kujikuta unaaibika bure kwa kuambulia fedha kidogo zisizoweza kufanya harusi ukaishia kulisha watu ugali dona kwa maharage au dagaa wakabaki kushangaa wakati ulitaka kufanya harusi ya bajeti kubwa kwa kutegemea michango
 
Nimetoka kulambwa km dola 100 mda si mrefu inauma balaa,sema tu namuheshimu huyo demu na mwanae anaeolewa ni mchepuko so nabembelezea niendelee kutafuna tu.
Wengine sitoi senti kumi na hata unialike bure siji vilevile
hata akiolewa potelea pwete😁.
 
Hizi ni nyuzi special kuelezea akili za mtu mweusi, naanzia hapa.
Akili za mtu mweusi season1.
ep 01 :
Kuchangishana pesa kwenye raha binafsi za watu( hizi wanaita sherehe za harusi, ubatizo, birthday n.k )

* Kuna huu ujinga unaoendelea kwenye jamii zetu wa kuchangishana kwenye furaha binafsi za watu pesa kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao.

* Imefika hatua wajinga wanakusanya michango kama vile ana kudai, ni mwendo wa kukufuatilia kila uchwao ili tu umsaidie pesa ya kuendeshea huo upuuzi wake sijui ndoa, birthday na ujinga mwengine.

* Kuna watu wanavuka mstari mwekundu mpaka anakuunganisha kwenye magroup ya WhatsApp ili mpige zogo humo za namna gani mtapush upuuzi wake anao panga kuufanya.

* Kadi sasa hapa ndio kuna ujinga mwingi sana imekuwa kama kitambulisho cha taifa kwamba lazima uchukue na utie kiasi tajwa huu ni ufala wa level ya juu sana.

* Sherehe za harusi, ubatizo, birthday, vipaimara n.k hizi zote ni raha binafsi sio mchongo kutaka marafiki, ndugu, watu wa karibu, watu unao juana nao, majirani kukuchangia kwenye raha zako binafsi unazo taka fanya.

* Fanya vitu kwa uwezo wako usiwape shida jamii kuuwazia upuuzi wako namna gani ya kuupush.

NB: Hizi akili za namna hii kwa watu weusi inabidi zikome mara moja na najua kuna majitu humu huu uzi umewagusa kwa sababu ndizo akili hizi zimejaa vichwani mwao.
Mimi sipendi huu upuuzi,ile mwanzoni magroup yanaanza,nikawa kwenye group la A level tuliosoma wote.Mweh zikaanza zile mtu kajifungua eti mchango. Nilitoka mbio.Mimi ninaamini kabisa yale maisha kabla ya mitandao, watu walimaliza A level,vyuo then kila mtu akawa na maisha yake huko. Leo tena kulazimishana kuchangiana mimi nipo Katavi wewe upo Dar.Mimi huo upumbavu siutaki.
 
Sure! Huu ujinga ni mwingi mno yaani daaah,,juzi juzi kuna mtu kafikia kuniadd group watsap kucheki ni la michango ya harusi nikampigia nikamwambia ntakuchangia ila naleft group,,,,"atasubiri sana"
 
Kila mtu na starehe yake, harusi zao sisi wageni tunakula, kunywa,kuserebuka na kuburudika plus social interaction ni sawa kuchangia tu. Nyinyi wazungu changianeni sex parties / orgies mshee wanawake na wanaume na ngono na wanyama beastiality.
 
Back
Top Bottom