Teknolojia ni mkombozi pekee wa maendeleo Tanzania

Edson Carrington

JF-Expert Member
Oct 30, 2022
216
634
Habari wakuu,

Twende moja kwa moja kwenye mada, maana muda ni mchache na mambo ni mengi sana. As Tanzania tumekuwa na tabia ya kuamini sana kwenye miujiza kuliko uhalisia wa mambo mbalimbali yanayotukumba. Pia kutokana na hili kila siku nchi yetu imekuwa nyuma kwenye masuala mbalimbali ilihali tuna kila nyenzo ya kusonga maendeleo.

Leo naomba niangazie kwenye suala zima la teknolojia nchini na barani kwa ujumla. Kwani kufikia karne hii Tanzania imekuwa moja ya nchi zinazotoa elimu mbalimbali kuhusiana na masuala ya teknolojia mfano uhandisi mbalimbali, habari na mawasiliano, afya nakadhalika.

Almost asilimia kubwa ya vijana wapatao nafasi ya kusoma masuala ya teknolojia wamekuwa wavivu kufikiri kuhusiana na matatizo mbalimbali yanayokumba jamii zetu na kutafutia ufumbuzi. Tunakumbwa na jamii ya vijana waliokosa uthubutu wa masuala mbalimbali ambao wengi wao wamekuwa wakitumia Elimu zao kama chombo cha kupata ajira na kuendesha maisha yao, na si elimu yao kukomboa jamii zetu.

Moja ya vichochezi muhimu vya maendeleo kwa afrika ni teknolojia kwani ndio nyenzo kubwa inayotutofautish na nchi zilizoendelea huko ughaibuni.
Hivyo basi sisi kama vijana hatuna budi kusimama kwenye nafasi yetu na kuipigania Afrika kwa kutumia elimu yetu.

Kuzorota kwa demokrasia, changamoto kwenye sekta mbalimbali, maradhi na majanga mengine mbalimbali ni moja ya matatizo yanayotukumba Afrika ambapo yanaweza kutumiwa kama fursa na pia kutatuliwa kwa teknolojia inayotokana na elimu yetu. Hili ni jukumu la kila kijana kuamua na kuifanyia kitu nchi kutokana na nafasi yake. Hii inaweza kuwa chachu ya maendeleo nchini.

Mimi kama mtaalamu wa masuala ya Teknolojia ya habari, naahidi kupambana kwa nafasi yangu hivyo pia naamini wewe kama kijana mwenzangu utapambana kwa nafasi yako kuipa nchi faida ya kuwa nawe.

Kutoka kwa Raisi mama Samia,
" Vijana ni nguvu kazi na tegemeo la taifa, japokuwa nguvu kazi hii kama itatumiwa vibaya itakuwa mzigo pia kwa taifa".

Pamoja kwenye Tanzania ya Teknolojia.

Teknolojia kwa maendeleo
 
Back
Top Bottom