Naomba msaada Ajira portal

Naomba msaada Ajira portal

sepema

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2019
Posts
603
Reaction score
1,011
salaam wakuu. Nimefungua akaunti ya ajira portal tangu mwaka jana, taarifa zote muhimu(CV)nimeweka na imekamilika kwa asilimia 98. Changamoto nipale ninapotaka ku apply nafasi za kazi inaniandikia *Failed" na maneno flani chini yake. Kuna mtaalamu nilimshirikisha akadai inatokana na mimi kuwa mwajiriwa wa serikali, japo baadhi ya nafasi hazizuii mtumishi wa umma kuomba.Sijui hili lina ukweli gani,na kama nihivyo naombeni msaada jinsi yakufanya ili inapotangazwa nafasi ninayoipenda(nikiwa na sifa) niweze kuomba.
 
Attachments

  • IMG_20260728_205409_824.png
    IMG_20260728_205409_824.png
    144.6 KB · Views: 6
salaam wakuu. Nimefungua akaunti ya ajira portal tangu mwaka jana, taarifa zote muhimu(CV)nimeweka na imekamilika kwa asilimia 98. Changamoto nipale ninapotaka ku apply nafasi za kazi inaniandikia *Failed" na maneno flani chini yake. Kuna mtaalamu nilimshirikisha akadai inatokana na mimi kuwa mwajiriwa wa serikali, japo baadhi ya nafasi hazizuii mtumishi wa umma kuomba.Sijui hili lina ukweli gani,na kama nihivyo naombeni msaada jinsi yakufanya ili inapotangazwa nafasi ninayoipenda(nikiwa na sifa) niweze kuomba.
Nicheki kwa namba 0743231877 nikusaidie
Yawezekani kwenye qualifications ulijaza vibaya , au hauna sifa ya kuomba kazi unayoapply
unaweza kuomba endapo barua yako itapitia kwa mkurugenzi wa ofisi yako..
 
changamoto nikwamba mfumo unakataa kwenye hatua za awali kabisa. Yan ile nikiminya tu neno "apply" inaniandikia Failed
 
Mkuu umeshaajiriwa serikalini yaan namaamisha una cheq number?
 
Fafanua vizuri mkuu, una fani mbili tofauti au??

Na lengo unataka kuhama taasisi moja ya zamani ili uapply kwenye taasisi nyingine??
 
Ndio mkuu. Nafasi ninazoomba ni zile ambazo wanaruhusu hata aliyeajiriwa kuomba kwa sharti la kupitishiwa barua na mwajiri wake
 
Fafanua vizuri mkuu, una fani mbili tofauti au??

Na lengo unataka kuhama taasisi moja ya zamani ili uapply kwenye taasisi nyingine??
Iko hivi, niliajiriwa serikalini na diploma. Nimeenda kusoma bachelor ya kitu kingine tofauti na ile diploma. Ninachotaka nikuhama taasisi ya zamani kwenda nyingine kupitia hii degree
 
Nicheki kwa namba 0743231877 nikusaidie
Yawezekani kwenye qualifications ulijaza vibaya , au hauna sifa ya kuomba kazi unayoapply
Kuhusu sifa huwa nakuwa nazo kulingana na kazi iliyotangazwa mkuu. Qualifications nimejaza zote kwa usahihi kwani kuna jamaa anautaalamu wa hizo mambo alizipitia na kujiridhisha kuwa zipo sawa.
 
Iko hivi, niliajiriwa serikalini na diploma. Nimeenda kusoma bachelor ya kitu kingine tofauti na ile diploma. Ninachotaka nikuhama taasisi ya zamani kwenda nyingine kupitia hii degree
Kama unahitaji kuhamia taasisi B kupitia shahada omba uhamisho kupitia mfumo wa hiyo taasisi B with recategorization,kuliko kuanza kuomba upya kupitia ajira portal.
 
Asante mkuu
 
Iko hivi, niliajiriwa serikalini na diploma. Nimeenda kusoma bachelor ya kitu kingine tofauti na ile diploma. Ninachotaka nikuhama taasisi ya zamani kwenda nyingine kupitia hii degree
Sasa hii huwezi kuhama kwa ku apply kupitia ajira portal mkuu,

Ingawa umechelewa, point ya kwanza ilitakiwa Uwashilikishe maafisa au katibu wako akupe ushauri kitu gani unaweza kusoma kabla hujala hasara.

Ndo maana tunasema kuwa ukiwa kwenye system unashauriwa kuendeleza masomo kulingana na cadre yako, ila kama Umesoma cadre tofauti kabisa( hasa masuala ya utawala) inabidi upeleke magamba Kwa maafisa wako waone wapi unafiti kisha wakupe kitengo. Tofauti na hapo, acha kazi serikalini nenda kwenye mashirika binafsi.... 🤝 🤝 🤝
 
Back
Top Bottom