Ajira na waganga wa kienyeji

Ajira na waganga wa kienyeji

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,618
Jana wakati nipo kwenye daladala natoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine mmoja wa abiria aliyekuwepo ndani ya daladalaalikuwa akiongea na mtu ambaye baadaye tulikuja kufahamu kuwa ni kaka yake.

Katika maongezi yao, huyo abiria alikuwa akimuomba huyo kaka yake hela na kaka yake akamchomolea basi baada ya kukata simu yule jamaa akawa anaongea na rafiki yake pembeni kitu ambacho ndiyo kimenifanya nilite hii maada, ALISEMA ''Huyu bro we muache tu, alihangaika sana kutafuta ajira, ametafuta zaidi ya miaka mitatu mimi ndiyo NILIMPELEKA KWA MGANGA mpaka akapata hiyo kazi lakini hana hata shukrani hajawahi kunipa hata shilingi moja''

Baada ya hayo maneno ndiyo nikafunguka kuwa kumbe kuna watu wanakesha kwa waganga wakitafuta kuwezeshwa wapate ajira.

Vipi wewe mwenzangu na mimi? Baba yako si lolote wala chochote, kichwani hauna kitu, Mungu haumuabudu, kwa waganga hauendi,
NI LINI UTAPATA AJIRA?

Namaliza kwa kusema MUNGU WA WOTE.
 
Kwa hiyo huyo mganga alimsaidiaje yani kupata hiyo ajira? Sometimes napenda sana kufahamu hizo kitu zina work vipi. Alimkonnect na mteja wake ambaye ni bosi akampatia hiyo ajira? alimwajiri yeye kama yeye? How? Mtu yeyote anayefahamu haya mambo atupe madesa tufahamu juu ya hii sayansi asee.
 
labda
Code:
mzizi mkavu
atakuwa anaelewa kidogo.....
 
Yani umenichekesha mpaka nimepaliwa manake nilikuwa nakunywa chai
 
kama huna qualifications huna tu. sasa kazi inahitaji mtu civil eng, experience 3 years, wewe BA History umegraduate mwaka jana unadhani mganga gani atakusaidia hapo?

tuachane na matapeli hawa vijana, tukazane na kuapply tu, kikubwa tuwe smart wakati wa kufanya application na tukiitwa interview.
 
That is the point. Unless unambie huyo mganga anakuja kufanya interview badala yako.
 
huyo mganga unakuta ana ndugu wana njaa na yeye mbona hajipi dawa akawe mganga wa watu wenye zao. Saa zingine mganga anakupaka mkaa na unakuwa na confidence tuu. MUNGU NDIO KILA KITU,shida ni kwale ambao hawapo kwa Mungu na KWa shetani.
 
kinachofanyika ni kupandishwa nyota yako,,yani wanao ku interview wanavutiwa na wewe hata kama umejibu hovyo,,kaeni tu hapo hapo mjini hapa,,,
 
Jana wakati nipo kwenye daladala natoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine mmoja wa abiria aliyekuwepo ndani ya daladalaalikuwa akiongea na mtu ambaye baadaye tulikuja kufahamu kuwa ni kaka yake.

Katika maongezi yao, huyo abiria alikuwa akimuomba huyo kaka yake hela na kaka yake akamchomolea basi baada ya kukata simu yule jamaa akawa anaongea na rafiki yake pembeni kitu ambacho ndiyo kimenifanya nilite hii maada, ALISEMA ''Huyu bro we muache tu, alihangaika sana kutafuta ajira, ametafuta zaidi ya miaka mitatu mimi ndiyo NILIMPELEKA KWA MGANGA mpaka akapata hiyo kazi lakini hana hata shukrani hajawahi kunipa hata shilingi moja''

Baada ya hayo maneno ndiyo nikafunguka kuwa kumbe kuna watu wanakesha kwa waganga wakitafuta kuwezeshwa wapate ajira.

Vipi wewe mwenzangu na mimi? Baba yako si lolote wala chochote, kichwani hauna kitu, Mungu haumuabudu, kwa waganga hauendi,
NI LINI UTAPATA AJIRA?

Namaliza kwa kusema MUNGU WA WOTE.

tusiokuwa na marefarii maofisini tuna kazi ngumu kwa kweli!

mimi nimeikimbia sector ya elimu ambayo in ajira ya moja kwa moja,

namuomba MWENYEZI MUNGU anifanikishe tu nipate kazi huku roho yangu iliko penda!

otherwise, sina ushirika na waganga wa kienyeji!
 
Kwa hiyo huyo mganga alimsaidiaje yani kupata hiyo ajira? Sometimes napenda sana kufahamu hizo kitu zina work vipi. Alimkonnect na mteja wake ambaye ni bosi akampatia hiyo ajira? alimwajiri yeye kama yeye? How? Mtu yeyote anayefahamu haya mambo atupe madesa tufahamu juu ya hii sayansi asee.

mkuu kuna huu uzi hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-biashara-na-uchumi/106954-biashara-ya-uchawi-tanzania.html nadhani utakuwa wa msaada mkubwa sana kwako!!

uko sticky jukwaa la biashara na uchumi..!

na kama uko sticky basi ujue lisemwalo limo!
 
kinachofanyika ni kupandishwa nyota yako,,yani wanao ku interview wanavutiwa na wewe hata kama umejibu hovyo,,kaeni tu hapo hapo mjini hapa,,,
Mkuu shalolizo Hebu funguka basii. Mfano mnapiga pepa written then hata ujibu utumbo mtoa marks anavutiwa na majibu yako (hayohayo ya kiutumbo) afu una qualify? Hebu funguka mkuu.
 
Last edited by a moderator:
sisi ofisini kwetu walikuwa wanawambia applicants wafungue bahasha zao reception,nilipodadisi waliniambia kuwa siku hizi applicants wanaweka manyoya,ungaunga na vitu vingine related na ushirikina. kwa hiyo ili kuepusha hayo hand delivery application zinafunguliwa na wenyewe! ila ikifika wakati wa kufungua za posta utashangaa maajabu ya dunia jinsi watu wanavyoamini ushirikina ktk ajira
 
mh inawezekana maana mbona wasanii pia wanaenda kwa waganga? maana AT alikiri kabisa kuwa alipeleka cd yake kwa mganga ili afanikiwe kupata tuzo za.kili awards so cha muhim ni watu waelewe ni kweli haya yanawezekana kweli? na inakua vip? mh God forbid!? Mzizi Mkavu baba sogea huku utoe elimu..
 
Waganga walikuwepo zamani wa sasa hv ni copy and pest
 
labda
Code:
mzizi mkavu
atakuwa anaelewa kidogo.....

Yeye ni mganga? Ngoja tumwit huku aje atupatie hili somo adhimu MziziMkavu njoo huku utupe somo.

mzizimkavu labda akwambie nyota yako ni ng'ombe mbuzi ama otherwise!

maybe anajua zaidi, siwezi sema moyowe!
Nyinyi munaishi ulimwengu upi? Kuna uchawi, utibabu na mengineyo mengi siwewzi

kusema hapa ni siri za Waganga kwa hiyo mtu kwenda kwa mganga ili aombewe Dua mambo yake yawe mazuri kwa mfano apate cheo

kazini au ashinde uchaguzi au biashara yake ifunguke apate wateja au mambo yake yawe mazuri afunguliwe nyota za bahati yake hayo

mambo yote yapo katika ulimwengu huu hata wazungu wanaroga kama tunavyoroga sisi hakuna kitu cha ajabu mtu kwenda kwa

mganga afanyiwe dua apate kazi kawazi kwenu mnaoamini au msio amini mchanga wa pwani huo mimi simo.
 
Back
Top Bottom