msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 839
- 1,472
- Thread starter
- #21
Rushwa, undugu na kujuana ndivyo vimetamalaki katika zoezi la ukusanyaji taarifa za walimu wanaojitolea hata majina yaliyotumwa tamisemi mengi yamejaa udanganyifu. Mathalani kuna watu wamejitolea kwa miezi kadhaa lakini kwenye ripoti wameandikiwa wamejitolea kwa mwaka mmoja na zaidi. Wengine baada ya kusikia kuna zoezi la ukusanyaji taarifa za walimu wa kujitolea wameenda kwa walimu wakuu na maafisa elimu kata kuongea nao kiutu uzima na majina yao yametumwa. Kwaiyo ata kama tamisemi wataamua kuajiri wanaojitolea wajue kabisa kuna ubatili mwingi umefanyika kwenye taarifa walizotumiwaHili suala wanapewa ajira kwa wanaojitolea tu ni rushwa hili mama angalia hili.inakuwaje mnasema ambao hawana ajira wajiajiri wenyewe.watu wamejiajiri wakisubiria ajira ,na sasa wanaambiwa ajira hakuna ila kwa wanaojitolea tu.hili suala litasababisha rushwa kufanyika.