Je, aliyekuwa Katibu Mkuu Chama cha Walimu Tanzania Deus Seif na Mweka Hazina Abubakari Alawi walifanya ajira za Kilaghai?

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
3,399
6,077
Novemba 2017 Aliyekuwa Katibu Mkuu Chama cha Walimu Tanzania Alhaji Yahya Bakari Kilo Msulwa alifariki dunia. Kwa Mujibu wa Katiba ya CWT toleo la sita 2014, nafasi ya katibu mkuu ilipaswa kujazwa na Baraza la taifa la chama hicho. Julai 2018 katika ukumbi wa LAPF Dodoma, Deus Seif kwa msaada toka kwa moja ya vigogo wa siasa nchini alishinda uchaguzi huo kilaghai dhidi ya mgombea mwenzake ndugu Simon Edwin Keha aliyepewa nafasi ya kukaimu ukatibu mkuu baada ya kifo cha katibu mkuu na ambaye inaaminike ndiye aliyeshinda lakini matokeo yakageuzwa.

Seif ambaye ni dhaifu kitaaluma, aliyefeli mtihani wa darasa la saba huko kwao Moreti wilaya ya Gairo alikwenda kurudia darasa la saba eneo la Kibakwe wilaya ya Mpwapwa akipata usaidizi kutoka kwa familia ya mmoja wa waziri mwandamizi wa serikali kwa sasa. Akafaulu, na kabla ya kuwa katibu mkuu CWT, alikua Afisa Elimu wa Geita DC, na aliyekuwa Afisa taaluma wake kwa sasa naye ni Waziri Mwandamizi wa Serikali.

Seif alipoingia ofisini alijifunza kwamba ni lazima watu wanaomzunguka ofisini wawe ni watu wake watakaomuunga mkono na kumsaidia kwa kila jambo ili kuficha udhaifu wake na madhambi yake na jingine ni kwamba ilikuwa ni lazima awaondoe makao makuu ya CWT maafisa waandamizi ambao aliamini wangekuwa kikwazo kwake kwa kuwashusha vyeo (demotion) ili aweke anaowahitaji. Aliwashusha vyeo wafuatao.
  1. Bi. Mwandile Benno Kiguhe aliyekuwa mkuu wa Idara ya Jinsia na walimu wanawake alimpeleka kuwa katibu wa Wilaya ya Hanang;
  2. Bw. Prosper Aloyce Lubuva aliyekuwa mkuu wa idara ya elimu na mafunzo alimpeleka kuwa katibu wa Wilaya ya Bukoba manispaa.
  3. Bw. Simon Edwin Keha aliyekuwa mkuu wa idara msaidizi elimu na mafunzo alipelekwa kuwa Katibu wa Wilaya ya Serengeti
  4. Bw. Dagobati Deogratius Tigaliyoma aliyekuwa msaidizi wa mkuu wa idara ya utetezi (mwanasheria) ambaye sasa ni marehemu kuwa katibu wa wilaya ya mkalama.
Deus kwa kutumia ulaghai kwa kamati ya utendaji ya taifa walimteua Stella Kiabo mjumbe wa kamati ya Utendaji ya taifa akiwakilisha mkoa wa Pwani kujaza nafasi iliyokuwa ya Prosper Lubuva na Stella Obedi Mamoto aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya taifa akiwakilisha walimu wanawake kujaza nafasi iliyokuwa ya Bi. Mwandile Kiguhe. Hapa maana yake ni kwamba Stella wote wawili walikua ni wajumbe wa kamati ya utendaji ya taifa. Kwenye kikao kilichofanyika Mwanza walishiriki kutoa hizo demotions na kwenye kikao hicho hicho wakateuliwa na wajumbe wenzao kujaza nafasi za waliofanyiwa demotions. Huu ulikua ni uharamia.

Kwa taratibu za CWT, wafanyakazi wa makao makuu huteuliwa kwa kutumia moja ya njia hizi mbili. (1). Kuitishwa usaili kwa kutumia vyombo vya habari. (2). Mfanyakazi kuteuliwa kutoka ngazi za chini yani wilaya au mkoa. Kina Stella hawakupitia njia hizo.

Sababu ya wafanyakazi waandamizi hao kushushwa vyeo ilielezwa kwenye barua zao kwamba ni ili kwenda kuimarisha chama kwenye ngazi za chini (Huu ulikuwa ni utapeli na kejeli) walipopeleka shauri lao CMA, Deus aliwazunguka mpaka leo haki zao hawajapata, mmoja wao amefariki na mwingine amestaafu.

Katika kuhakikisha kwamba Deus analeta watu wa kumuunga mkono makao makuu alihakikisha anawaleta wafuatao.
  1. Marieta Masanja (huyu aliajiriwa kwa nafasi ya uhasibu, alikua ni mhasibu wa Geita DC alipokuwa Deus alikuwa awe TC lakini alipata changamoto ya kikazi kwa muajiri wake, aliomba likizo bila malipo kwa miaka 3 lakini alipoingia ofisini Deus alimsainisha mkataba wa ajira ya kudumu kwa hiyo akawa na mikataba 2 hili ni kosa kisheria.
  2. Batholomeo Chilwa (huyu alikuwa ni afisa habari Geita DC, aliajiriwa kuwa afisa habari CWT makao makuu akitoka mshahara wa sh. 700,000 hadi mshahara wa sh. 1,800,000 kwa mwezi). Chilwa aliomba likizo bila malipo kwa miaka 3 kwa hiyo naye alikua na mikataba miwili ya ajira kwa wakati mmoja.
  3. Queen Augustino Luvanda (kwa sasa ni mkuu wa idara ya utetezi na mwanasheria wa CWT. Alitokea Geita na ana mkataba wa likizo bila malipo toka kwa muajiri wake na Deus alimpa mkataba wa ajira ya kudumu.
  4. Elina Simon Kanyuma (alitokea Geita kwenye Advocate ambayo ni private firm, kaka yake ni marehemu Kanyuma aliyekuwa afisa elimu wa Geita TC. Alipata promotion ya kwenda wizara ya elimu makao makuu na baadae alifariki. Deus akiwa Afisa Elimu Geita DC, Kanyuma alikua afisa elimu Geita TC kwa hiyo alimpa ajira mdogo wa swahiba. Elina Kanyuma hadi sasa ni mwanasheria wa CWT. Jambo jingine muhimu ni kwamba, Tangazo la ajira kwa wakati ule lilikuwa la kuajiri mawanasheria mmoja lakini Deus akalazimisha mwingine wa ziada.
  5. Buto Masele (huyu alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya upimaji ramani mkuranga kampuni hii ilikua inamilikiwa na aliyekuwa afisa elimu taaluma wa Geita ambaye kwa sasa ni waziri mwandamizi na aliajiriwa kama Real Estate Manager CWT)
  6. Ancila Protas Masawe (aliajiriwa kama katibu muhtasi wa Deus akitokea Geita. Mama yake ambaye kwa sasa ni marehemu ni mdogo wa kuzaliwa wa mke wa Deus Bi. Magreth Macha. . Kwa sasa mke wa Deus ni Afisa Elimu Msingi Geita DC
  7. Faraji Kanyama (huyu alikua ni dereva wa familia ya Deus na alipewa ajira ya mkataba kama dereva wa Katibu mkuu yani Deus. Baada ya Deus kuondoka mkataba wake uliisha na si mwajiriwa wa CWT.
  8. Alfred Stanley (huyu ni mtoto wa kaka yake Kornelio Magembe ambaye kwa sasa ni mkuu wa wilaya ya Geita na naibu katibu mkuu wa TUCTA aliyesaidiwa kupata nafasi hiyo kinyemela na Deus kwa kuwa hakuwa mwanachama wa CWT, pia aliwahi kuwa mkuu wa wilaya ya Ukerewe. Alfred Stanley aliajiriwa kama Cashier wa Chama na kwa sasa amehamishiwa Teachers Development Company Limited, Mwalimu House.
  9. Alfred Alexander (huyu alikua afisa elimu takwimu na vifaa Geita DC alipewa barua ya kuteuliwa kuwa katibu wa wilaya Bariadi na Deus bila kufanya usaili na baadae akampeleka Makao makuu CWT kama afisa idara ya utetezi na ndipo alipo hadi sasa. Deus kuwateua makatibu bila usaili imekua ni tabia yake na wengi amewaingiza kwenye nafasi za kazi kwenye chama kwa mtindo huo huo.
  10. Arnold Kisigiro (huyu ni mtoto wa rafiki yake Deus, alikua akifanya kazi kwenye moja ya kampuni za simu, aliajiriwa kama IT. Tangazo la ajira lilihitaji IT mmoja tu lakini Deus alimuongeza mtoto wa rafiki yake.
  11. Teddy Boniface Simbachawene aliyeajiriwa kama afisa masijala kazi ambayo haijawahi kutangazwa, huyu anatokea kule ambako Deus alikwenda kurudia darasa Kibakwe wilaya ya Mpwapwa.
Deus aliyafanya haya ili kuhakikisha kwamba anapata watu wa kumlinda kwenye uovu wake na udhaifu wake asigundulike na aendelee kuwaharass mahasimu wake kadiri ambavyo wangejitokeza. Angalia hapo juu, namna walivyojipanga kwenye idara. Gazeti la jamhuri la Januari 2019 lilifichua taarifa hii ya ajira za mchongo, baada ya Deus kuliona hilo alifanya mambo mawili. (1) Kwa wale walioazimwa kutoka kwa waajiri wao yani likizo bila malipo kwa miaka mitatu kama ulivyo utaratibu wa serikali huku wakiwa na mikataba ya ajira za kudumu CWT ambao ni Marietha Masanja, Queen Augustino Luvanda na Batholomeo Chilwa mikataba yao hiyo ilinyofolewa kwenye mafaili wakiogopa serikali na mamlaka zake kufuatilia jambo hili. Ikifuatiliwa kule walikotoka, mikataba hiyo iliyonyofolewa itaonekana. Sanjari na hilo (2) Barua za maombi ya kazi ya wafanyakazi walioomba kutokea Geita zilinyofolewa na wakaelekezwa waandike maombi ya kazi yenye barua zenye anuani zisizo za Geita. Kwa hiyo itaonekana kwamba hakuna aliyeomba kazi kutokea Geita. Lakini uhalisia ni kwamba karibu wote walitokea Geita na wote walikua na uhusiano na Deus kama ilivyoainishwa hapo juu.

Jambo lingine la kifikirisha ni kwamba Deus Seif, Buto Masele, Batholomeo Chilwa na Alfred Stanley wote hawa wamejenga majumba ya kutisha yaliyofuatana eneo la Michese Dodoma(majumba ya kimashindano), Sanjari na kununua magari ya kifahari katika kipindi kisichozidi miaka 5. Unajiuliza ni kwa mishahara ipi? Vipato vyao vikichunguzwa itatoa clue ya namna gani pesa za chama zimekua zikiibwa.

Kwa nini iliwezekana kuajiri watu wa Deus, kamati ya utendaji ya Taifa ndicho chombo cha uajiri wa wafanyakazi wa chama, wajumbe hawa Deus aliwaweka mkononi ili waajiri watu anaowataka yeye. Hebu fikiri, ajira za kazi zimetangazwa kitaifa, wazi kwa kila raia kwa nini waajiriwa wote hawa watokee Geita pekee? Wajumbe wa kamati ya utendaji, Deus amekuwa akiwahonga. Ili kuligundua hili ni vyema serikali na mamlaka zake waangalie maeneo matatu
  1. Malipo ya Posho za wajumbe kwenye vikao vya kamati ya utendaji kwa kuangalia viwango na idadi ya siku tangu Deus aingie madarakani
  2. Kuchunguza Akaunti zao zilizopo Mwalimu Commercial Bank Limited mtiririko wa malipo na uhalali wa malipo hayo tangu Deus aingie madarakani
  3. Kuchunguza akaunti zao nyingine kwenye benki Tofauti hasa NMB.
Serikali na mamlaka zake zinashauriwa kufanya ukaguzi yakinifu wa fedha (Forensic Audit) tangu Deus Seif na Abubakari Alawi wawepo madarakani, hakika itagundulika namna ambavyo Deus Seif na marafiki zake waliopo ndani ya chama na Serikalini na wanasiasa walivyokuwa wanaiba fedha na rasilimali za walimu.

Ufichuzi wa Madhila waliyopitia walimu kupitia chama chao yataendelea kuwekwa wazi na tunaamini Serikali na mamlaka zake zinaendelea kuyafanyia kazi.
 
Mtu akifeli darasa la saba ndio dhaifu kitaaluma?
Si alirudia na kufaulu vizuri.
Mbona watu mbalimbali bora kabisa kwenye sekta zao walifeli na kurudia na wakafanya vizuri sana.
Yote kwa yote maelezo mazuri inatakiwa uchunguzi wa hali ya juu CWT.
 
Mpenzile ni mke wa seif, hapana!

Mtoto wa waziri anawezaje kuwa ps, sio rahisi.
Majungu at work.
 
Kwahiyo Deus anaajiri tu hovyo hovyo ndugu zake yeye kama nani? Kwani si kuna utaratibu wa kuomba kazi, anafanikishaje yote hayo?
 
Hiyo CWT iwe na management yake wasiwe waalimu bali ifanyike recruitment nje ya walimu na ukaguzi wa akaunti zake ufanyike kwa kina kwa kipindi cha miaka mi5, na wabadhirifu waadhibiwe
 
Back
Top Bottom