Luqman Maloto: Waziri Ummy ajiepushe kufanya kazi mtandaoni

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,802
21,398
Muktadha ni mwanafunzi wa Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI), Hombolo, Dodoma, Lightness Shirima. Kitambulisho chake cha taifa kilizuiwa Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila kwa sababu ya deni.

Lightness alikuwa anamuuguza baba yake, ambaye alifariki dunia. Akaacha deni hospitali lenye kufikia Sh9 milioni. Mloganzila wakazuia kitambulisho cha Lightness ili wawe na uhakika deni lingelipwa.

Pamoja na kukaa na kitambulisho, Mloganzila walimpa Lightness agizo la kufanya malipo angalau Sh50,000 kila mwezi, mpaka atakapomaliza kulipa.

Tujadili malipo ya Sh50,000 kila mwezi kwa Sh9 milioni, maana yake angetumia miezi 180 kulipa deni lote. Miezi 180 ni sawa na miaka 15. Wakati huohuo uhai wa kitambulisho cha taifa ni miaka 10. Dhamana gani hii?

Kumbe sasa Lightness mwenye miaka 22 leo, kama angekuwa na nidhamu ya kulipa kila mwezi kama alivyopangiwa, angemaliza malipo akiwa na umri wa miaka 37. Kipindi chote hicho, angekosa huduma za msingi za kijamii kwa kutokuwa na kitambulisho cha taifa.

Kichekesho; Lightness angekuwa sio mwaminifu, angeweza kuwaachia kitambulisho Mloganzila na kwenda Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), kuripoti kupotelewa kitambulisho chake. Kwa maana hiyo angeweza kupata kitambulisho kingine na Mloganzila wangebaki na nakala ambayo ingetambuliwa na Nida kama iliyopotea.

Twende kwenye hoja; Gazeti la Mwananchi liliripoti habari ya Lightness. Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, aliiona habari, akasoma na kuchukua hatua za haraka. Pongezi kwa Waziri Ummy kwa kuwa mfuatiliaji na mwenye uamuzi wa haraka.

Ummy alimwagiza Lightness kupitia ukurasa wake wa Facebook, aende Mloganzila akachukue kitambulisho chake. Papo hapo aliomba watu wa karibu wampe mawasiliano ya mwanafunzi huyo. Akasema: “Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inajali wananchi wake.”

Nimetangulia kumpongeza Waziri Ummy kwa kitendo chake cha kiungwana. Hata hivyo, kuna ushauri wa kumpa. Ni kujua umuhimu wa kufanya kazi kwa mifumo na kuijua kasoro ya maonesho ya kiongozi mitandaoni au kwenye vyombo vya habari.

Nyakati za mwisho za uongozi wa Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump, mtangulizi wake, Rais wa 44, Barack Obama alimfananisha mrithi huyo wake na waigizaji wa mtindo wa maisha kwenye televisheni, yaani reality show.

Trump alikasirishwa sana na maneno ya Obama. Hata hivyo, msisitizo wa Obama ni kwamba ufanyaji kazi wa Trump, kujionesha zaidi mitandaoni na hata kujibishana na watu, alikuwa anakosea misingi ya uongozi wa Ofisi ya Rais, The Oval, badala yake aliamua kucheza reality show.

Huu ndio ushauri kwa Ummy. Suala la Lightnes ni zuri kwa namna alivyolifanyia kazi. Hata hivyo, lilibeba taswira ya maonesho ya mtandao zaidi kuliko kushughulikia kimfumo nfani ya ofisi yake.

Ummy ndiye bosi mkuu wa wizara. Alikuwa na nafasi ya kulifuatilia suala hilo hatua kwa hatua na kuunda suluhu ya kudumu. Kulisoma jambo na kulitolea uamuzi mtandaoni bila kushirikisha wasaidizi ndio mambo yaliyosababisha uongozi wa Trump uitwe reality show.

Hili ni tatizo lililoanza kuchukua nafasi pana kipindi cha uongozi wa Rais John Magufuli. Serikali ilifanya reality show kuanzia Ikulu mpaka ofisi za wakuu wa wilaya. Rasimu ya mchezo ilielekeza kumsifu zaidi mkuu wa nchi na kuonesha kuwa mbele yake majibu yote yapo.

Rais Samia ameshasema yeye hataki kujaziwa ‘misifa’. Anataka wasaidizi wake wafanye kazi. Mfano wa karibu ni hili la Lightnes, Waziri Ummy amesema Rais Samia anajali wananchi wake. Naomba nikubaliane naye kisha nihoji: “Mbona la Lightness limeibuka?”

Rais ni maono na dira, wanaotafsiri kwa vitendo ni wasaidizi wake. Rais hataki Mtanzania maskini adhalilike kwa kukosa pesa za matibabu. Ummy kwa nafasi yake ya kuwa msimamizi mkuu wa sekta ya afya, anapaswa kujenga mfumo unaotekeleza dira na maono ya Rais.

Inapotokea Mtanzania anapitia wakati mgumu kwa sababu ya kushindwa gharama za matibabu, mpaka ananyang’anywa kitambulisho cha taifa. Na kumbe Rais Samia hataki hayo yatokee. Maana yake Ummy ameshindwa kutafsiri kwa vitendo dira ya bosi wake.

Rais Samia hawezi kuingia Wizara ya Afya na kusuka mfumo utakaotasiri maono yake. Ni sawa na Ummy hataingia hospitali moja baada ya nyingine kusimika muundo autakao.

Mifumo ya utawala

Waziri kazi yake ni kuhakikisha dira ya Rais inatafsiriwa kimfumo, kuanzia hospitali ya taifa hadi zahanati ya kijiji.

Ushauri zaidi ni viongozi kujiepusha na presha za mitandaoni. Na hapohapo nasisitiza kwamba wasizichukulie poa hizo presha. Muhimu ni kuzipokea na kuzitafutia majibu katika namna ambayo mfumo mzima unajifunza.

Alichokifanya Ummy kinakaribisha watu wengine wenye kuumizwa na bili za hospitali lakini hawana uwezo wa kulipa, nao wakimbilie kwenye vyombo vya habari au mitandaoni.

Haitakuwa sawa. Wajibu wa Ummy sio kutatua changamoto kwenye mitandao, bali kupitia mifumo ya wizara anayoongoza.

Madhara ya Serikali kuendeshwa kama reality show ni kuibuka migongano ya mara kwa mara miongoni mwa mawaziri, makatibu wakuu na hata wakuu wa mikoa.

Rejea nyakati za mvutano wa mawaziri January Makamba na Hamisi Kigwangalla au Kigwangalla na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Kigwangalla pia alirushiana maneno na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Profesa Adolf Mkenda. Hivi sasa Mkenda ni Waziri wa Elimu. Usisahau mvutano wa Makonda na Waziri wa Habari, Nape Nnauye.

Serikali ikiendeshwa nje ya mifumo inayoeleweka migongano lazima itokee na mwananchi anakuwa njiapanda.

Hapa tunaamua kutojadili mivutano ya wakuu wa wilaya dhidi ya wakuu wa mikoa, vilevile wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri.

Serikali yenye kuendeshwa kama reality show, nidhamu ya mfumo wa kiutawala hutoweka. Kila mmoja hutaka kuonekana. Hali hiyo huunda familia ya kambare serikalini, kila mtu ana sharubu. Ubongo unaota pembe.

Uongozi wa kisasa ni lazima viongozi wawe mitandaoni. Hata hivyo, wajichunge. Mitandao isiwapelekeshe wakasahau kuwa Serikali inafanya kazi kwa mifumo. Sio maonesho ya mitandaoni. Serikali inataka uwajibikaji wa kimfumo. Sio reality show.

Chanzo: Mwananchi
 
Sekta ya afya kuna matatizo makubwa sana sema UMMY ana bahati sana hasemwi
 
Mleta mada uliongea vizuri sana na ninakuunga mkono.

Lakini tunawaomba kuanzia Rais mwenyewe pamoja na viongozi waandamizi wengine, washinde mitandaoni wakiperuzi, watapata mengi ya kufanyia kazi na kupunguza kero za wananchi kimya kimya bila ya kubebewa mabango ya uwajibikaji.
 
Alichokifanya waziri Ummy ni sawa na kufunga "bandeji" "jeraha" la "mshale"
Bila kwanza kuutoa ile ncha ya mshale,ambayo tayari iko ndani ya mwili!

Mawaziri wengi kwa sasa wanacheza na popularity ya kumsifia Rais,kwa maslahi yao binafsi.

#Ummymwalimu ni mmojawapo wa hao,alianza na Samia wakiwa Tanga!
Walipokwenda kusikilizia kitakachojiri Dar es Salaam!

Siku ileeee.....

Na Usiseme Samia hapendi sifa!
Hayo ni maneno yako wewe peno hasegawa!

Kama unanibishia....weka hapa link ya bandiko hata moja au video clip ukimkariri Rais Samia akikataa sifa!
 
Back
Top Bottom