ong'wafaza
JF-Expert Member
- Apr 30, 2012
- 243
- 100
Nimkuwa nikifuatilia kwa muda mrefu takwimu zinazotolewa na polisi kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na janga la Ajali za barabarani zikionyesha kuwa bodaboda ndo chanzo kikuu Cha Ajali hizo hasa mijini.
Pamoja na ukweli huo kudhihirika,Bado mamlaka zinazohusika hazichukui hatua madhubuti kudhibiti hali hiyo.
Pamoja na hatua kidogo ambazo mamlaka zinachukua Ili kupunguza Ajali hizi,Mimi napendekeza yafuatayo;-
1. Halimashauri na Serikali za mitaa zitunge Sheria ndogondogo za kuhakikisha kuwa Sheria za usalama barabarani zinafuatwa kikamilifu katika maeneo yao.
Kwa mfano,wamiliki wote wa bodaboda wasajiliwe na Serikali zao za mitaa/vijiji kwa masharti maalumu.
Ingependeza kama sharti la dereva kuwa na leseni liwe miongonii nwa masharti hayo.
2. Sheria ndogondogo hizo ziwabane madereva wa bodaboda pamoja na abiria wao kuhusu ukiukwaji wa Sheria hizo.
Kwa mfano,dereva akikamatwa Hana leseni na amepakia abiria,yeye na abiria wake wachukuliwe hatua Kali ikiwemo kutozwa faini .
Hii itawafanya abiria kudai leseni kwa dereva kabla hajapanda hiyo badaboda.
Na kwa hali hiyo,wamiliki na hata madereva wenye mapungufu mbalimbali watakosa abiria na hawatakuwa barabarani wakiendesha vyombo hivyo tena.
Mambo haya yakitekelezwa kikamilifu sio tu yatapunguza Ajali za barabarani zinazosababisha na bodaboda,Bali pia yataongeza mapato ya Serikali zetu za mitaa na vijiji kupitia faini watakazokuwa wanakusanya.
Swali;
Je, rushwa haitachukua mondo wake?
Naomba kuwasilisha.