Nini kifanyike bajaji na bodaboda kutosimama kwenye zebra?

Hakuna anayejali

JF-Expert Member
Jun 3, 2023
258
269
Habari, katika kutembea kwangu hapa na pale nimegundua tabia za madereva bajaji na bodaboda wengi hawatii sheria za barabarani, gari linasimama zebra lakini hao jamaa wanapita kushoto au kulia au hata wanapishana na mtembea kwa miguu katikati ya zebra.

Na wakati mwingine wanaona toka mbali mita mia mtembea kwa miguu ameonesha nia ya kuvuka wao wanapiga honi ya kumtisha asivuke. Je na wewe unaliona hili, nini kifanyike?
 
Habari, katika kutembea kwangu hapa na pale nimegundua tabia za madereva bajaji na bodaboda wengi hawatii sheria za barabarani, gari linasimama zebra lakini hao jamaa wanapita kushoto au kulia au hata wanapishana na mtembea kwa miguu katikati ya zebra.

Na wakati mwingine wanaona toka mbali mita mia mtembea kwa miguu ameonesha nia ya kuvuka wao wanapiga honi ya kumtisha asivuke. Je na wewe unaliona hili. nini kifanyike?
Polisi waambiwe na kupewa ruhusa kuwa hizo ni pesa za kiwi ....yaani waruhusiwe wakimkamata boda kafanya hivyo nusu ya pesa wanachukua na iliyo baki wanawekewa kwenye mfuko wa kukopesha polisi wote nchi nzima
 
MOJA YA KERO SUGU HII.
NA NDIO MAANA WAPATAPO AJALI, NYOYO ZA WENGI ZINASUUZIKA
Hii ni kero kubwa sana, specificaly hapa Arusha, eneo la Summit centre, kuna zebra inayoruhusu watu kuvuka kutokea summit kwenda kanisa la calvary, hapo watu wa hiace wamegeuza ndiyo parking yao, na madereva wa hiace Arusha wengi wao ni walevi sugu, cha kushangaza unakuta hiace imesimama hapo kuziba zebra, halafu dereva yupo hapo hapo anapiga story na askari traffic, yaani huwezi kutofautisha ujinga wa dereva na traffic.
 
Wakamatwe polisi wanaowafumbia macho! Trafiki hukaa barabarani si kwa usalama wa raia na vyombo vyao, bali kwa ajiri ya matumbo yao! Kwa vile wanajua boda hawana pesa ya kuwapa, basi hujifanya hawawaoni, macho yote yako kwa dala na madereva wa magari binafsi wakadai hongo! Hao ndo chanzo cha matatizo! Wakamatwe wao wajibu kwa nini wanajifanya hawawaoni!
 
elimu ndo shida.. hii ni elimu ya nyumbani kabisa elimu ya nidhamu wengi wao hatuna!. Unaweza ukadharau lkn lina athari kubwa sana ndio hiyohiyo elimu ambayo inatufanya tusijenge na kuijali nchi yetu!

Hata viongozi hawana nidhamu wanafuja tu pesa za umma!.. Ndio hiyohiyo elimu ambayo tumeikosa inayotufanya tupuuzie mambo ya msingi! Hata chaguzi hatuna time nazo. Hatuthamini ndio maana tunatupa taka hovyo tunachafua nchi yetu,so usishangae shida nishaonyesha ilipo.
 
Habari, katika kutembea kwangu hapa na pale nimegundua tabia za madereva bajaji na bodaboda wengi hawatii sheria za barabarani, gari linasimama zebra lakini hao jamaa wanapita kushoto au kulia au hata wanapishana na mtembea kwa miguu katikati ya zebra.

Na wakati mwingine wanaona toka mbali mita mia mtembea kwa miguu ameonesha nia ya kuvuka wao wanapiga honi ya kumtisha asivuke. Je na wewe unaliona hili. nini kifanyike?
Mada nzuri sana hii, binafsi hii tabia inaumiza sana na watu wengi wamekufa, kupata vilema na majeraha, RPC wapo, RTO wapo, Traffic police wapo, IGP yupo, inaumiza sana
 
Polisi waambiwe na kupewa ruhusa kuwa hizo ni pesa za kiwi ....yaani waruhusiwe wakimkamata boda kafanya hivyo nusu ya pesa wanachukua na iliyo baki wanawekewa kwenye mfuko wa kukopesha polisi wote nchi nzima
Fine on the spot yaani kila kosa msimbazi wa hapo hapo unabaki watarejesha heshima ya kufuata SHERIA za Nchi.
 
Boda boda akili amnaa, sasa angalia huyu kapakia ngedere mwenzie😄😄
Screenshot_20240310-210332_WhatsApp.jpg
 
Habari, katika kutembea kwangu hapa na pale nimegundua tabia za madereva bajaji na bodaboda wengi hawatii sheria za barabarani, gari linasimama zebra lakini hao jamaa wanapita kushoto au kulia au hata wanapishana na mtembea kwa miguu katikati ya zebra.

Na wakati mwingine wanaona toka mbali mita mia mtembea kwa miguu ameonesha nia ya kuvuka wao wanapiga honi ya kumtisha asivuke. Je na wewe unaliona hili. nini kifanyike?
Ushamba unawasumbua

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom