Ajali yaua watu watatu na kujeruhi 36 Tanga

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,117
1660493753729.png

Watu watatu wamefariki dunia kwenye ajali iliyohusisha Lori lililobeba wafanyabiashara waliokuwa safarini kwenda Handeni mkoani Tanga kwa ajili ya mnada.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Handeni, Dr. Hudi Shehdadi amethibitisha kupokea miili ya watu watatu na majeruhi 36 huku akieleza majeruhi 11 hali zao sio nzuri kutokana na majeraha waliyopata.

Kwa mujibu wa Rajabu Juma ambaye ni mmoja wa majeruhi, ajali imetokea eneo la Kwamagome baada ya Lori hilo kushindwa kukata kona.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Sofia Jongo hakupatikana kuzungumzia ajali hiyo, msaidizi wake ameeleza kuwa kamanda yupo kwenye msafara wa kumpokea Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ameanza ziara mkoani Tanga.
 
Watu watatu wamefariki dunia, huku 39

wakijeruhiwa, baada ya lori aina ya Fuso lenye namba usajili T 150 AGB, walilokuwa wakilitumia kwenda mnadani kuacha njia na kupinduka wilayani Handeni, mkoani Tanga.

Chanzo: ITV
 
Mi nataka kusafiri😱au bas nitasafiri ivoivo🙄.Wapumzike Kwa amani,na majeruhi wapone
 
Hizi fuso niliziona kilosa zinabeba mzigo wa mnada mzima na wafanyabiashara wote
 
Back
Top Bottom