Ajali yaua watu wanne wa familia moja Morogoro

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1673707025225.png
Watu wanne wamefariki dunia kufuatia ajali ya lori na gari dogo aina ya Toyota Spacio katika eneo la Kwambe Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro na kusababisha barabara kufungwa kwa saa kadhaa.

Akizungumza na Mwananchi Digital kwa simu leo Januari 14 Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Majid Mwanga amesema gari hilo ndogo lilikuwa na watu sita akiwemo dereva ambaye ni mtumishi wa Serikali.

Mwanga amesema kwa sasa wanaendelea kufanya mawasiliano kujua ni mtumishi wa idara gani.

Aidha amesema imetambulika kuwa waliokuwemo ndani ya gari hiyo woye ni familia moja, ambapo aliwataka madereva kuendelea kuwa makini wanapokuwa barabarani hasa kwa kipindi hiki cha Mvua.

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mtakatifu Joseph Dumila, Manyele Kapongo amesema wamepokea miili ya watu hao (marehemu) na majeruhi wawili.

Kapongo amesema kwa sasa wanaendelea na matibabu ya majeruhi hao wawili ambao ni mama na mtoto.

Aidha mashuhuda wa ajali hiyo wanasema kuwa magari hayo yaligongana uso kwa uso na ambapo gari ndogo imeharibika vibaya.

Shuhuda Julias Michael mkazi wa Dumila akizungumzia ajali hiyo amesema chanzo cha ajali hiyo ni kuendesha mwendokasi wa dereva wa gari ndogo kwa kushindwa kukwepa.

MWANANCHI
 
Hivi Spacio ni 7 seater? Aaaah itakua mtoto alikua amepakatwa.

Kumbe eneo la Dumila limetokana na jina la Mt. Joseph Dumila. Anaonekana alikua mtakatifu sana.

Mimi nikiwa dereva, nikiona gari inakuja mbele yangu, naikwepa. Haitonigonga.

Hivi gari za siku hizi zinaundwa kwa materials gani, mbona zikipataga ajali zinapondeka sana?
 
Yes ziko spacio zina 7 seats kuna kuwa na mbili nyuma za ziada unakunjua.
 
Hivi Spacio ni 7 seater? Aaaah itakua mtoto alikua amepakatwa.

Kumbe eneo la Dumila limetokana na jina la Mt. Joseph Dumila. Anaonekana alikua mtakatifu sana.

Mimi nikiwa dereva, nikiona gari inakuja mbele yangu, naikwepa. Haitonigonga.

Hivi gari za siku hizi zinaundwa kwa materials gani, mbona zikipataga ajali zinapondeka sana?
Gari za sikuhizi zinawekewa body laini na hazina chassis. Zina frame tu ambayo ndio inafungwa fungwa na machuma chuma yote ya chini.

Ndio maana gari ikishafumuliwa sehemu ya engine tu ambako ndio pagumu yote inakuwa inaisha kabisa na kuchanika chanika.
 
Back
Top Bottom