Ajali yatishia ndoto za bingwa wa olimpiki

Ajali yatishia ndoto za bingwa wa olimpiki

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
439
Reaction score
1,070
Bingwa wa Olimpiki wa mbio za kuruka mbali, Tara Davis amelazimika kusitisha msimu wake wa riadha wa mwaka 2026 kufuatia kupata mshtuko mkali wa ubongo uliosababishwa na ajali ya gari.

Uamuzi huo unamaanisha kuwa mwanariadha huyo Mmarekani mwenye umri wa miaka 27, hatashiriki katika Mashindano ya Riadha ya Dunia yanayofanyika wiki hii nchini Hungary, hatua inayopunguza nafasi yake ya kutetea mafanikio yake makubwa katika msimu huu.

Akielezea masikitiko yake kupitia mitandao ya kijamii, bingwa huyo wa dhahabu wa Olimpiki ya Paris 2024 na mashindano ya Dunia ya Tokyo, alikiri kuumia na kusikitishwa na tukio hilo huku akiahidi kwa mashabiki wake kuwa atapambana na kurejea tena uwanjani akiwa imara zaidi mara baada ya kupona kikamilifu.

1788855140660.png
 
Back
Top Bottom