Melubo Letema
JF-Expert Member
- Apr 1, 2020
- 416
- 413
Wakati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa mstari wa mbele kuhamasisha na kukuza Michezo Tanzania ukiwemo wa riadha ,
ila kuna Vizee vilivyopo kwenye Kamati ya Olimpiki Tanzania (Tanzania Olimpic Committee ~ TOC) vinaendekeza hila na uzandiki wa kufikia kumuita mwanariadha wa kimataifa Alphonce Simbu MUASI , hiyo haitoshi alikuwa anagombe Uenyekiti wa Kamisheni ya wachezaji ila hao wazee wakakata jina lake wazee hao ni Henry Tandau (makamu wa rais TOC) na Ghulam (Rais wa TOC) sambamba na Filbert Bayi (Katibu wa TOC) , kisa eti alikataa kukimbia akiwa amevaa mavazi ya kampuni ya ASICS kutumia kampuni ya XTEP
SOMA WALICHOANDIKA WADAU WA RIADHA:
Shida ya kwanza ameenguliwa kwa kwa kutuhumiwa kua kahamasisha mgomo wa kuvaa Xtep wakat ukweli ni kwamba Tandau aliwadanganya watanzania kua amesajili Asics wakati RT iliishasajili Xtep. Simbu kama mchezaji hakua na uwezo wa kukubali au kukataa vifaa wakati aneishaambiwa vifaa gani vimesajiliwa.
Hata tukiachana na kumkata kwanini Tandau amdhalilishe Simbu kwa kumwita Muasi? Simbu ameipambania sana hii nchi kwenye mashindano mbali mbali ya IOC, Common Wealth Games Commitee, Ya Shirikisho, Ya Majeshi kote amepeperusha bendera ya nchi kwa miaka mingi tangu alipoanza kwenda kimataifa.
Leo mtu anaamua kumwita Muasi mbele ya hadhara ya wanamichezo mbalimbali. Hii sio haki kabisa. Nafikiri Wanamichezo wote tuna deni kwa Simbu na tunapaswa kumpigania kwa nguvu zote katika hili kama
Ambavyo yeye amekua akitupigania kimataifa.
Simbu kashiriki mashindano ya kuibeba nchi kwa miaka ya mfululizo bila kuchoka. Hivi karibuni amelazimika kucheza marathon mbili ndani ya siku saba kwajili ya nchi yake. Amecheza Majeshi Naijeria jumapili moja na akapata Gold, na jumapili
Iliofuata kaenda kucheza Valencia na akapata Shaba. Tutakua tumemsaliti kama
Tutakaa kimya na kuacha lipite hivi hivi.
UDHALILISHAJI WA MWANARIADHA:
Simbu ni mwanajeshi, Simbu ni mwanariadha wa kimataifa, Simbu ni Kapteni wa timu ya Taifa ya Riadha, 2022 alikua kapteni wa timu ya Taifa ya Tanzania ilioshiriki Birmingham Common Wealth Games na akaleta medali ya fedha, Simbu ni icon ya Taifa katika michezo.
Huyo Henry Tandau August 2021 baada ya Tokyo Olympic alienda Ikulu kwaajili ya Simbu, leo hawezi kumwita Simbu Muasi alafu ikaisha hivi hivi, lazima pafanyike jambo.