Ajali ya Mh Regia - tuna tatizo

Wayne

JF-Expert Member
May 27, 2009
659
201
Wakulu

Nimesukumwa kuandika haya baada ya kufuatilia tukio zima la ajali ya Mh. Mbunge ambaye sasa ni marehemu.

Mh. Regia alikuwa mlemavu wa mguu wa kulia. Gari aliyokuwa anaendesha kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi lilikuwa halijafanyiwa -modification kwamba ni gari maalumu kwa ajili ya walemavu.

Sasa swali, ni mamlaka gani ilitoa leseni kwa Marehemu? wakati anajulikana kwamba ni mlemavu...... (ukizingatia kwamba kwa mujibu wa sheria zilizopo, hata ukiwa na makengeza huruhusiwi kupewa leseni)

Nauliza hili kwa uchungu tukizingatia kwamba Regia alikuwa ni hazina ya taifa...... mpaka lini tutaendelea kupoteza vijana wenye uwezo mkubwa wa kulisaidia taifa hili ... kwa kuruhusu uzembe, kutoheshimu sheria na mambo yanayofanana na hayo?

Ilikuwaje mfumo mzima kuanzia serikali kupitia vyombo vyake vya TRA, Trafiki polisi, ndugu, chama chake, marafiki zake, abiria aliokuwa nao kwenye gari kwa nyakati mbalimbali hawakuliona hili kwamba ni tatizo kwa marehemu kuendesha gari wakati yu mlemavu ? kwa nini hawakumkemea, hawakumshauri ....n.k

Sheria, kanuni na taratibu zipo kutulinda ..... naamini TUNA TATIZO KUBWA KULIKO TUNAVYODHANI.....

Naomba tujadili objectively...bila jazba...
 
Kila mtanzania ni hazina ya Taifa, wazima na walemavu

Mbona huulizi walemavu wanahudumiwa vipi kwenye hii nchi?

usisahau kuwa nchi yetu ulikuwa inaongozakwa kua ALBINO sasa jiulize wenye ulemavu mwingine wakoje hali zao?
 
Haya bwana ajali zote nchi hii zinasababishwa na madereva walemavu sio? Haya bwana ajali zote nchi hii zinasababishwa na madereva walemavu sio?
 
mi bado sijaelewa logic unayojenga hapa ni nini??

je unauliza swali mamlaka gani iluruhusu yeye kuendesha gari???

au unataka kutuambia kuwa ni uzembe wake???

au unailaumu serikari???

anywai ni hivi 'MHESHIMIWA MBUNGE ALIYEKUWA NA ULEMAVU WA MGUU ALIPATA AJALI YA GARI ALILOKUWA ANALIENDESHA MWENYEWE, NA ALIFARIKI DUNIA HAPO HAPO! (Sasa hayo mengine yaache kama yalivyo, kama ni uzembe wake au serikali au dreva wake poa, mungu amuweke mahari pema peponi)
 
Hakuwa na leseni. Ni ubishi wake wakifahari ndio ulimfanya aendeshe gari mwenyewe! Mbona unatafuta mtu wa kumpa lawama? Hili ni kosa la REGIA mwenyewe! Hayo ya hazina unayajua wewe!
 
Tulishajadili hili toka jumamosi.........mwacheni apumzike na ile ilikuwa ni ajali tu......hata Sokoine alikufa kwa ajali japo hakuwa na ulemavu
 
Kuna tatizo mahali nakubaliana na wewe,
ajali zinaongezeka na sababu zinaongezea,
mamlaka zetu zilizoajiri ndugu zetu, tunaogopa kuzihukumu, kwani wantanzania ni ndugu na tunapendana, bila kujua kuwa kupendana sio kulindiana maovu.
 
kamanda mwenyezimungu anapoamua kuchukua kiumbe chake ameamua hata kama angekuwa haendeshi yeye kama wakati wake ulikuwa umefika asingekwepa,pamoja na ulemavu wake alimudu kuendesha gari hilo,ukitafuta ni nani mwenye makosa unakosea na tena unamkufuru mungu ambaye ndie anaetoa uhai na kuuchukua kwa wakati apendao,regia ametangulia nasi tuko nyuma yake kwani ni njia ya wote hiyo kikubwa tumuombee mh wetu mungu ailaze roho yake mahali pema peponi AMIN.
 
nyinyi mlijadili!!! sisi hatujajadili na ndo tunajadili

Kwa tija ipi? kwamba alikuwa mlemavu basi asiendeshe gari? Alipataje leseni?........tusitafute kuanzisha maneno yasiyo saidia kwa mtu amabaye tumeshamzika
 
Wakati nachangia kwenye thread za kifo chake, niligusia suala hili japokuwa sikusema juu ya mamlaka. Nilisema yeye mwenyewe kasababisha kifo chake, kwani ni mlemavu halafu anaendesha gari MANUAL, ambayo inahitaji kutumia viuongo mbalimbali vya mwili kuliendesha.

pili nilizungumza kuwa, kitendo cha yeye kutokuwa na dereva kwa safari hiyo wakati tayari serikali inamlipa hela ya dereva tena wa daraja la juu la kuendesha viongozi wa serikali, nao ni ufisadi. kunyima vijana wenye daraja lessen C, kumemgharimu maisha, kumetugharimu watanzania kwani tulikuwa bado tunamhitaji tuendelee kupambana.

Mwisho nilisisitiza vyombo vilivyopewa mamlaka kusimamia sheria visiangalia sura ya mtu katika kusimamia sheria, japokuwa vinalalmikiwa lakini wasimame kama taasisi wawashitaki wale wanaotumia fedha za walipakodi kujinufaisha. Na waanze na wabunge ambao mpaka sasa wamekataa kuajiri madereva wenye sifa kuwaongoza safarini, huu ni ufisadi kwa wabunge
 
Kwa tija ipi? kwamba alikuwa mlemavu basi asiendeshe gari? Alipataje leseni?........tusitafute kuanzisha maneno yasiyo saidia kwa mtu amabaye tumeshamzika

kila kitu huwa kina funzo ndani yake. mbunge hatakiwi kujiendesha kwa namna yoyote ile, huo ni ufisadi tu
 
Hakuwa na leseni. Ni ubishi wake wakifahari ndio ulimfanya aendeshe gari mwenyewe! Mbona unatafuta mtu wa kumpa lawama? Hili ni kosa la REGIA mwenyewe! Hayo ya hazina unayajua wewe!

acha kupayuka wewe kiumbe uliekosa heshima kwa Mungu wako
 
pengine umekaa ukahisi wewe utakuwa umeuliza swali la maana kweli na bahati mbaya familia yenu ndio wanakutegemea anyway
akuna jipya atizo mnaingia huku mpaka mpate viji 500/1000 jitahdi uwe unaingia mara kwa mara utakuta mkeo kauzwa ujui..kuna waliuliza wakajibiwa sioni jipya ulilouliza
all the best
 
kila kitu huwa kina funzo ndani yake. mbunge hatakiwi kujiendesha kwa namna yoyote ile, huo ni ufisadi tu

Una hakika?......mimi kila weekend napishana na Dr Mwinyi akiendesha gari lake binafsi.....mbona trafiki hawamkamati? wakati mwingine binadamu huhitaji privacy bila uwepo wa devera hata kama umuhimu upo.....sasa ufisadi unatoka wapi?
 
Kwa tija ipi? kwamba alikuwa mlemavu basi asiendeshe gari? Alipataje leseni?........tusitafute kuanzisha maneno yasiyo saidia kwa mtu amabaye tumeshamzika
Nadhani hata tuliobaki tunaweza kupata somo kutokana na yale yaliyotokea. Kwa hiyo nadhani ni muhimu tukajadili hili kwa kina, si kwa maana ya kumshushia lawama marehemu, bali kupata funzo la nini kilifanywa vuisivyo na kuwa uwezekano wa chanzo cha ajali ile ili sisi tuliobaki tujiepushe kufanya kama hivyo.
 
Nadhani kunaswala kubwa hapa zaidi ya Marehemu Regia, tunaongealea miundo mbinu na mazingira yaliyopo Tanzania iwapo yanawawezesha watu waishio na ulemavu kuwa na haki na uhuru wa kuendesha magari. Itambulike ni haki kwa mlemavu ambaye anauwezo wa kuendesha gari inayolinda usalama wake kuendesha gari. Ni wajibu wa mamlaka tofauti kuhakikisha upatikanaji wa vifaa hivyo ama magari hayo ya walemavu, na kuhakikisha wanatimiza masharti hayo ya uendeshaji salama. Kwa watu waishio na ulemavu ni wajibu kutambua na kutimiza masharti ya nchi katika uendeshaji salama
 
......mapungufu yaliyomo kwenye mamlaka zetu nchini yanajulikana, na kibaya zaidi watanzania kwa ujumla huwa hatuangalii mbele zaidi zaidi tunafuata matukio, ni wakati sasa wa kubadilika vinginevyo tutawapoteza wengi.
 
Nadhani hata tuliobaki tunaweza kupata somo kutokana na yale yaliyotokea. Kwa hiyo nadhani ni muhimu tukajadili hili kwa kina, si kwa maana ya kumshushia lawama marehemu, bali kupata funzo la nini kilifanywa vuisivyo na kuwa uwezekano wa chanzo cha ajali ile ili sisi tuliobaki tujiepushe kufanya kama hivyo.

Kwani tumezuiwa kufanya hivyo mpaka tumtumie marehemu kama reference? Ajali ngapi zimeua watu na mbona wasitumike kama reference hapa? Polisi hawajatoa ripoti rasmi ya chanzo ajali sasa tunajifunza kutokana hadidu rejea ipi?
 
Kuna tatizo mahali nakubaliana na wewe,
ajali zinaongezeka na sababu zinaongezea,
mamlaka zetu zilizoajiri ndugu zetu, tunaogopa kuzihukumu, kwani wantanzania ni ndugu na tunapendana, bila kujua kuwa kupendana sio kulindiana maovu.

Haika

Nashukuru kwamba umeweza kuliona tatizo...lkn bado tunahitaji ufafanuzi wako...nahisi kwamba labda naliangalia hili kwa mtazamo tofauti...
 
Back
Top Bottom