Congo
JF-Expert Member
- Mar 13, 2008
- 2,064
- 2,301
Wakulu
Nimesukumwa kuandika haya baada ya kufuatilia tukio zima la ajali ya Mh. Mbunge ambaye sasa ni marehemu.
Mh. Regia alikuwa mlemavu wa mguu wa kulia.Gari aliyokuwa anaendesha kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi lilikuwa halijafanyiwa -modification kwamba ni gari maalumu kwa ajili ya walemavu.
Sasa swali, ni mamlaka gani ilitoa leseni kwa Marehemu? wakati anajulikana kwamba ni mlemavu...... (ukizingatia kwamba kwa mujibu wa sheria zilizopo, hata ukiwa na makengeza huruhusiwi kupewa leseni)
Nauliza hili kwa uchungu tukizingatia kwamba Regia alikuwa ni hazina ya taifa...... mpaka lini tutaendelea kupoteza vijana wenye uwezo mkubwa wa kulisaidia taifa hili ...kwa kuruhusu uzembe,kutoheshimu sheria na mambo yanayofanana na hayo?
Ilikuwaje mfumo mzima kuanzia serikali kupitia vyombo vyake vya TRA, Trafiki polisi, ndugu, chama chake, marafiki zake, abiria aliokuwa nao kwenye gari kwa nyakati mbalimbali hawakuliona hili kwamba ni tatizo kwa marehemu kuendesha gari wakati yu mlemavu ? kwa nini hawakumkemea, hawakumshauri ....n.k
Sheria , kanuni na taratibu zipo kutulinda.....naamini TUNA TATIZO KUBWA KULIKO TUNAVYODHANI.....
Naomba tujadili objectively...bila jazba...
Nimesoma maoni mengi kuhusu mada uliyoanzisha.Wengi sana wamekuponda lakini hata mie nilikuwa na wazo la kunzisha mada kama hii, bahati nzuri nimeikita yako. Ukweli unabaki ukweli kuwa linapokuja suala la ajali kuna ajali ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. Sasa ukiangalia mazingira yenyewe kuwa alitaka kulipita gari lililokuwa mbele yake akakutana na gari lililokuwa linakuja upande mwingine. Akaingia porini. Gari likapinduka mara (wanasema) saba. Kama gari lilipinduka mara saba ina maana alikuwa mwendo kasi, jambo linalokemewa na trafiki kila leo. Hapo mambo mawili yanajitokeza. Hakuhakikisha kama hakuna gari mbele na alikuwa mwendo kasi. Hivi ni vitu viwili havina uhusiano na ulemavu wake na VINGEWEZA KUEPUKIKA. Suala la ulemavu na uendeshaji wa gari ni suala lamjadala pia ukizingatia hali ya ulemavu wake. Mamlaka zetu unazijua zaweza kumpa mhasibu kazi ya kujenga barabara.