Ajali ya Mh Regia - tuna tatizo

Uache uongozi wa chadema, wao wanashughulikia masuala makubwa kama Ufisadi na maandamano, usalama wa uhai wa mtu kama marehemu Regia kwao sio muhimu, ingekua muhimu wangemshauri awe na dereva japo kwa safari ndefu kama hizo.
 
......mapungufu yaliyomo kwenye mamlaka zetu nchini yanajulikana, na kibaya zaidi watanzania kwa ujumla huwa hatuangalii mbele zaidi zaidi tunafuata matukio, ni wakati sasa wa kubadilika vinginevyo tutawapoteza wengi.

Mkulu

Heshima kubwa kwako...naomba tuendelee kujadili
 
Uache uongozi wa chadema, wao wanashughulikia masuala makubwa kama Ufisadi na maandamano, usalama wa uhai wa mtu kama marehemu Regia kwao sio muhimu, ingekua muhimu wangemshauri awe na dereva japo kwa safari ndefu kama hizo.

Jamani mnatumia vichwa kweli kufikiri ? Yaani chama kikae kulazimisha hata masuala binafsi ya mtu ? Kwa hiyo ajali ile walaumiwe CHADEMA? kazi ipo......je kama yeye mwenyewe hakutaka hiyo safari aende na dereva?
 
Nadhani kunaswala kubwa hapa zaidi ya Marehemu Regia, tunaongealea miundo mbinu na mazingira yaliyopo Tanzania iwapo yanawawezesha watu waishio na ulemavu kuwa na haki na uhuru wa kuendesha magari. Itambulike ni haki kwa mlemavu ambaye anauwezo wa kuendesha gari inayolinda usalama wake kuendesha gari. Ni wajibu wa mamlaka tofauti kuhakikisha upatikanaji wa vifaa hivyo ama magari hayo ya walemavu, na kuhakikisha wanatimiza masharti hayo ya uendeshaji salama. Kwa watu waishio na ulemavu ni wajibu kutambua na kutimiza masharti ya nchi katika uendeshaji salama

Hiki ndicho nilichotarajia tujadili ...asante...tuendelee
 
pengine umekaa ukahisi wewe utakuwa umeuliza swali la maana kweli na bahati mbaya familia yenu ndio wanakutegemea anyway
akuna jipya atizo mnaingia huku mpaka mpate viji 500/1000 jitahdi uwe unaingia mara kwa mara utakuta mkeo kauzwa ujui..kuna waliuliza wakajibiwa sioni jipya ulilouliza
all the best

Nawe pia nakushukuru kwa uchambuzi wako..asante...
 
WakuluNimesukumwa kuandika haya baada ya kufuatilia tukio zima la ajali ya Mh. Mbunge ambaye sasa ni marehemu.Mh. Regia alikuwa mlemavu wa mguu wa kulia.Gari aliyokuwa anaendesha kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi lilikuwa halijafanyiwa -modification kwamba ni gari maalumu kwa ajili ya walemavu.Sasa swali, ni mamlaka gani ilitoa leseni kwa Marehemu? wakati anajulikana kwamba ni mlemavu...... (ukizingatia kwamba kwa mujibu wa sheria zilizopo, hata ukiwa na makengeza huruhusiwi kupewa leseni) Nauliza hili kwa uchungu tukizingatia kwamba Regia alikuwa ni hazina ya taifa...... mpaka lini tutaendelea kupoteza vijana wenye uwezo mkubwa wa kulisaidia taifa hili ...kwa kuruhusu uzembe,kutoheshimu sheria na mambo yanayofanana na hayo? Ilikuwaje mfumo mzima kuanzia serikali kupitia vyombo vyake vya TRA, Trafiki polisi, ndugu, chama chake, marafiki zake, abiria aliokuwa nao kwenye gari kwa nyakati mbalimbali hawakuliona hili kwamba ni tatizo kwa marehemu kuendesha gari wakati yu mlemavu ? kwa nini hawakumkemea, hawakumshauri ....n.kSheria , kanuni na taratibu zipo kutulinda.....naamini TUNA TATIZO KUBWA KULIKO TUNAVYODHANI.....Naomba tujadili objectively...bila jazba...

Mkuu Wayne Heshima Mbele

Nadhani ulikuwa na hoja nzuri lakini ukuifanya kikamilifu kwa kuweka ushahidi wa baadhi ya lawama/Shauku zako

1) Swali lako la pili unauliza ni mamlaka gani iliyotoa leseni kwa Marehemu
Nadhani kwanza ungetuwekea hiyo leseni ya Marehemu na tukaiona imetolewa ikiwa kwenye Category gani, maana najua leseni zote zinakuwa na sehemu ya kuonyesha mwenye leseni ana ugumu gani wa kuendesha gari, (Mlemavu, anavaa miwani nk)

2) umesema Polisi walilikagua gari na kuthibitisha kuwa halikufanyiwa marekebisho ya kuendana na mlemavu
hapa point kumbe sio tatizo kwa mlemavu kuendesha gari (na ndio maana wana leseni za kuendeshea), maana hata polisi wanalijua hilo na Marehemu sio Mlemavu wa kwanza kuendesha gari, kumbe tatizo ni gari alikuwa kwenye kiwango staili kwa mlemavu

Mimi nakubaliana na wewe kuwa ukiukwaji wa kanuni na sheria ulifanywa na MArehemu, kwa kutumia leseni yake kuendesha asichoruhusiwa, ni uvunjwaji wa sheria unaoonekana ni wa kawaida machoni pa watu, ni kama mtu mwenye leseni ya gari ndogo kuitumia kuendeshea malori nk

Pamoja na hayo yote, kwa mujibu wa waliopona hiyo ajali, ni kuwa hiyo ajali haihusiani na ulemavu hata kidogo, kama alikuwa anataka kuovertake na likatokea gari lingine mbele, hapo hata kama hakuwa mlemavu hali ingekuwa ni hiyohiyo tu,

Pamoja na kuwa na hoja ya kuwa kwa nini watu wa kwenye gari hawakumkemea kwa kuendesha gari, lakini nadhani wangemkemea zaidi kwa speeding, umakini wa kuangalia kabla ya kuovertake na vitu kama hivyo
 
Duh...

Kwa wakati fulani, nililifikiria hili.... nikasema RIP Regia
 
Haika

Nashukuru kwamba umeweza kuliona tatizo...lkn bado tunahitaji ufafanuzi wako...nahisi kwamba labda naliangalia hili kwa mtazamo tofauti...
Labda kwa kuongeza ufafanuzi, na sie wenyewe hatupendi kuhukumiwa, na tuna nafasi ya kutokuhukumiwa, tuna nafasi ya kufanya shortcut ya mambo mengi tu including ya hatari kwetu na kwa wenzetu.
Nadhani nataka kuelekea kwenye law enforcement Tanzania ni ndogo, kwetu personally na kwa institutions zetu.
lakini kabla ya yote, kuilink hii na kifo cha dada yetu mpendwa, ningependa taarifa ya tukio. Ila inawezekana pia isipatikane kwa kuwa tunapendana.
 
hii tabia kila mara itokeapo ajali ama majanga tunaishia kusema kazi ya mungu aina makosa itatusumbua sana; kinachopaswa kuangalia ama kujadili ni je mambo gani yanasababisha ajali hizi?je?kwa mfano barabara aliyopatia ajali regia ingekua na upana wa kutosha na yeye mwenyewe kufata sheria za barabarani vema
 
hapa kuna hoja ya msingi, tusichukie kwa kuwa inamhusu mpendwa wetu. Kuna mengi ya kujifunza kwetu sisi na kwa serikali ili kuepusha au kupunguza ajali kama hizo na kuzidi kuwapoteza wapendwa wetu.
 
wakulu

nimesukumwa kuandika haya baada ya kufuatilia tukio zima la ajali ya mh. Mbunge ambaye sasa ni marehemu.

Mh. Regia alikuwa mlemavu wa mguu wa kulia.gari aliyokuwa anaendesha kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi lilikuwa halijafanyiwa -modification kwamba ni gari maalumu kwa ajili ya walemavu.

Sasa swali, ni mamlaka gani ilitoa leseni kwa marehemu? Wakati anajulikana kwamba ni mlemavu...... (ukizingatia kwamba kwa mujibu wa sheria zilizopo, hata ukiwa na makengeza huruhusiwi kupewa leseni)

nauliza hili kwa uchungu tukizingatia kwamba regia alikuwa ni hazina ya taifa...... Mpaka lini tutaendelea kupoteza vijana wenye uwezo mkubwa wa kulisaidia taifa hili ...kwa kuruhusu uzembe,kutoheshimu sheria na mambo yanayofanana na hayo?

Ilikuwaje mfumo mzima kuanzia serikali kupitia vyombo vyake vya tra, trafiki polisi, ndugu, chama chake, marafiki zake, abiria aliokuwa nao kwenye gari kwa nyakati mbalimbali hawakuliona hili kwamba ni tatizo kwa marehemu kuendesha gari wakati yu mlemavu ? Kwa nini hawakumkemea, hawakumshauri ....n.k

sheria , kanuni na taratibu zipo kutulinda.....naamini tuna tatizo kubwa kuliko tunavyodhani.....

Naomba tujadili objectively...bila jazba...

hii mada ilishajadiliwa kwenye habari mchanganyiko tangu juzi,ukitaka majibu mazuri nenda huko utayapata
 
mi bado sijaelewa logic unayojenga hapa ni nini??

je unauliza swali mamlaka gani iluruhusu yeye kuendesha gari???

au unataka kutuambia kuwa ni uzembe wake???

au unailaumu serikari???

anywai ni hivi 'MHESHIMIWA MBUNGE ALIYEKUWA NA ULEMAVU WA MGUU ALIPATA AJALI YA GARI ALILOKUWA ANALIENDESHA MWENYEWE, NA ALIFARIKI DUNIA HAPO HAPO! (Sasa hayo mengine yaache kama yalivyo, kama ni uzembe wake au serikali au dreva wake poa, mungu amuweke mahari pema peponi)

Hili ni tatizo, kwanini tu - ignore kila kitu; Kutokana na hili matatizo hayatatuisha. Muuliza swali ana hoja ya msingi sana. Katika hili iko kesi kabisa ya kupeleka mahakamani, ningeshauri wanaharakati wa mambo ya haki za binadamu kulipeleka hili mahakamani. Nafikiri kuna sehemu sheria ilipindishwa kwa makusudi.
 
Kwangu issue yenye mantiki ni namna ya kupunguza ajari za barabarani.Mtu akishatangulia mbele za haki ndo hivyo amekwenda na kamwe hatarudi. My main concern is to ensure we reduce to ZERO the level of public accidents that we have on roads.
 
Chukulieni hii issue positive! Watanzania tulio wengi huwa hatupendi kukosolewa au kuambiwa ukweli! tu wanafiki! Marehemu alikuwa na dereva wake ndani ya gari (Rodger), sasa kwa nini huyu kijana hakuendesha gari? hapa hatuangalii masuala ya ajari maana ajari ni ajari vyovyote yaweza kutokea!

swala hapa ni je, watu wote ndani ya gari walishindwa kumwambia ukweli? kwamba hapana na wakagoma usiendeshe hili gari? hata mama ake mzazi? na hakufunga mkanda why na watu mpo saba ndani ya gari? au ndio mlikuwa mnasubiri muone trafic ndio mumwambie usiendeshe au funga mkanda? ni lini watanzania tutakuwa strictly kama wazungu kuwa no ni no regardless ya kuwa utaonekana mbaya!

bongo mtu akiwa na principles mnasema mnoko! anajidai!. Hizi tabia ndizo zinatupelekea hadi maofisini mpaka serikalini tunabaki tunalalamika oh jk, oh jairo, oh lowasa. mpaka lini?

Tatizo ni sisi wenyewe na wala sio jk wala el wala nani maana hata ww ukikaa pale utafanya hayo hayo, jamani ni watanzania wangapi wanangangamala kupata mshahara mkubwa ili afanye kazi 100%? majority anataka alipwe chochote ili mradi aingiea akaibe!!

Tujifunze kuwa na principles na kufata sheria! Swali kwa nini watz tukiwa nchi za watu e.g ulaya tunafata sheria ila kwetu hatufuati?


Rest in Peace Regia.
 
Wakulu

Nimesukumwa kuandika haya baada ya kufuatilia tukio zima la ajali ya Mh. Mbunge ambaye sasa ni marehemu.

Mh. Regia alikuwa mlemavu wa mguu wa kulia.Gari aliyokuwa anaendesha kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi lilikuwa halijafanyiwa -modification kwamba ni gari maalumu kwa ajili ya walemavu.

Sasa swali, ni mamlaka gani ilitoa leseni kwa Marehemu? wakati anajulikana kwamba ni mlemavu...... (ukizingatia kwamba kwa mujibu wa sheria zilizopo, hata ukiwa na makengeza huruhusiwi kupewa leseni)

Nauliza hili kwa uchungu tukizingatia kwamba Regia alikuwa ni hazina ya taifa...... mpaka lini tutaendelea kupoteza vijana wenye uwezo mkubwa wa kulisaidia taifa hili ...kwa kuruhusu uzembe,kutoheshimu sheria na mambo yanayofanana na hayo?

Ilikuwaje mfumo mzima kuanzia serikali kupitia vyombo vyake vya TRA, Trafiki polisi, ndugu, chama chake, marafiki zake, abiria aliokuwa nao kwenye gari kwa nyakati mbalimbali hawakuliona hili kwamba ni tatizo kwa marehemu kuendesha gari wakati yu mlemavu ? kwa nini hawakumkemea, hawakumshauri ....n.k

Sheria , kanuni na taratibu zipo kutulinda.....naamini TUNA TATIZO KUBWA KULIKO TUNAVYODHANI.....

Naomba tujadili objectively...bila jazba...

Mawazo yako yanaweza kuwa ni ya kibaguzi sana hususan kwa walemavu. Kumbuka pia nao wana haki kamili ya kuweza kuendesha magari. Cha msingi ni aina ya gari hapa tunahusisha modification za kuweza kurahisisha na wao waweze kujiendesha.

Labda ni vizuri nikuweke sawa hapo.

1. Kwanini Mh aliruhusiwa kuendesha gari kwenda mwendo mrefu (yaani nje ya mji). kwani alihitajika kuwa na professional driver.

2. Pili Mh alitakiwa kufuata sheria za usalama barabarani yaani kufunga mkanda (safety belt) wakti chombo kinakwenda na kujizuilia na mwendo kasi.

Ukitazama picha ya gari lake inajionyesha wazi hakuwa amefunga mkanda. Na pasi na shaka yoyote abiria wote aliokuwa nao kwenye gari walikuwa wamefunga mikanda.

3. Viongozi kuwa wa kwanza kufuata sheria na sio kuvunja sheria .

Huo ni mtazamo wangu.

 
Nadhani ajali ni ajali tu. Mama wa kaya aliwahi kugonga mtu na msafara wake. Mumewe aliwekewa Mafuta machafu huko kaskazini. Then Gari lake tairi zilibuma huku Dar. Mwakyembe je Si alikuwa na qualified driver akala mzinga?
Kuna Mzee mwingine alikufa kwa ajali ya ndege Mbeya Kama sijakosea.
Hiyo ni mifano michache tu. Mchango wako haujengi. Angekuwa hajui kudrive asingefika hata huko Ruvu. Tumwache apumzike kwa Amani jamani.
 
Back
Top Bottom