Ajali ya Meli: Maoni na mtazamo wa wananchi kwa yaliyojiri

Nawatakia Lundenga na Rwehumbiza mashindano bora na yenye mafanikio. Narudia kusema Zanzibar sio Tanganyika ni nchi kama ilivyo Comoro ama Sychelles. Msiba wao unatugusa kwani ni binadamu wamekufa lakini hakuna haja ya kuahirisha mashindano kwa sababu ya msiba huo.

Wazanzibar wako karibu na Waoman kuliko Watanganyika hivyo mambo yao yawe ya shida ama raha hayatuhusu kivile.

Tukio la msiba huu liwe chachu ya kuvunja muungano rasmi maana kimsingi ulishavunjika.
 
...........Katika kile ambacho watanzania wanaweza kuanza kuona ni tukio geni kwa raisi wao JK ameahirisha safari yake ya CANADA aliyokuwa amealikwa na Gavana wa nchi hiyo.Hii inatokana na msiba wa kitaifa ulitokea huko Zenji na kuua watu wanakadiriwa ni zaidi ya 200....Nadhani anaumia sana kuikosa hii safari Bwana Vasco Da Gama......
 
haya mavyombo yetu ni kama miredio ya mbao tu hila kama maalim seif angekuja kufungua kisima mwananyamala ungeona waandish wetu wanafki wapo bize kama kuna tukio muhimu au sijui jk kaenda ngomani msoga. Aubu tupu.
 
Wakati MV Bukoba ilipozama na kuua maelfu ya watu nilitegemea kuwa serikali itajifunza na kuanza kuwekeza kwenye idara za dharura zilizo chini yake lkn kwa ajali hii ya sasa ya Nungwi ambako mamia ya watu wamekufa hasa kwa kukosa huduma nzuri za uokozi mapema kunaonyesha wazi kuwa serikali ya CCM haijui vipaumbele gani viwe vya kwanza kwenye kuiendesha serikali!

Kwenye tawala zao tumeshuhudia jinsi mabilion ya pesa za walipa kodi zinavyochezewa kwenye vitu ambavyo sio muhimu kulinganisha na uhai wa raia wake.Kulikuwa na ulazima gani wa kununua gari la upupu kwa polisi kwa mamilion ya pesa ili kudhibiti waandamanaji pasipo kuwezesha kwanza majeshi yetu na idara za dharura kuipa vifaa vya kutosha yakitokea majanga kama haya?

Kulikuwa na ulazima upi kwa Bunge kuhamia kwenye jengo jipya na viyoyozi vya kisasa pasipo kupeleka pesa hizo kwenye idara ya maafa ili waweze kukabiliana na majanga yakitokea?Kwa nini tulinunua ndege ya Rais kwa bei kubwa wakati idara za uokoaji hazina vifaa?Tutazidi kufa kwa uzembe kama huu hadi lini?

Nape najua wewe ni mwenzetu hapa naomba tueleze kuhusu hili tafadhali maana serikali isiyo wajali raia wake kwa kuweka vipaumbele vya ajabu mbele haifai kuwepo madarakani!

Sijui hata kauli yenu ya"tumethubutu,tumeweza na tunasonga mbele"kama ina maana yeyote kwa raia wa kawaida wa TZ wasio na uhakika wa kuokolewa kama watapata ajali;Miaka 50 baada ya Uhuru bado tunaiendesha nchi kibabaishaji kiasi hiki?
 
Tunaangamia kwa kukosa maarifa.
Hatujajifunza kitu. Ajali ya Mv. Bukoba ilikuwa ni shule, tumefeli sasa tumepiga sup.
Na hii tukifeli, tutaendelea kufia majini.
 
Nilikuwa nasoma habari ya ajali ya kuzama meli huko Unguja na Pemba, BBC kama tulivyo watanzania wengi nao wameshindwa kuelezea ajali ilipotokea.
Habari yao inachanganya na kuibua maswali Tanzania ni nchi gani? Je Zanzibar ni Nchi au Kisiwa? Je Pemba ni sehemu ya Zanzibar? Unguja ni wapi kwenye ramani ya dunia?
Angalia hii habari na ramani iliyowekwa na BBC BBC News - Zanzibar ferry disaster: Scores die, many more missing.
nadhani tunahitaji kuweka mambo clear kutambua nchi zinazotengegeza muungano wa Tanzania.
"At least 187 people have died after an overloaded ferry sank off the Tanzanian island of Zanzibar with at least 800 people on board".... mbona wameeleza vizuri tu mkuu..ama sijui kiingereza...nilivyoelewa ni kwamba " kwa uchache watu 187 wamekufa kufuatia boti iliyojaza kupita kiasi kuzama katika kisiwa cha zanzibar kilichoko tanzania.
 
Alipokufa Nyerere, redio stations zote na kumbi za starehe zilifungwa kwa mwezi mzima, leo wapendwa wetu Unguja na Pemba wameangamia baharini, starehe zimeshika mkondo kama kawa.
Huku Miss Tanzania, huku Yanga ina draw, huku rhumba kama kawa.
Jamani serikali yetu mbona haithamini watu wake? Kama ilivyofanya alipokufa Nyerere tunaomba ifanye na sasa
 
Kaiahirisha kwa muda ni lazima aende nyie hamumjui Vasco Da Gama nyie. Subirini hizo siku 3 zipite kama hamjamsikia yuko Ottawa
 
Heri yake sasa ameanza kufahamu kuwa watz hawataki upuuzi wake ambao amekuwa akiufanya hata hivyo haitamuongozea lolote watu wesha mchoka
 
Nyerere alikuwa Mtanganyika na Tv za Tanganyika na mengineyo ndo vilisimama. Hilo tukio limetokea Zanzibar na si Tanganyika. Mbona unaisemea nchi nyingine??
 
kuna watu wametoa maoni mahala fulani kuwa vodacom miss tanzania haina miss zanzibar hivyo kuisitisha au kuiahirisha wakati haiwahusu ni kutolitendea haki onyesho hilo. Dakika moja ya kuwakumbuka itatosha, hata hivyo zanzibar ni nchi jirani tu kama zilivyo zambia, burundi, uganda, n.k.
Hata hivyo ni janga la kusikitisha kwa kweli.

miss tanzania haiko katika mambo ya muungano. Ndo tutaambiwa hivyo. Kiukweli huu ni msiba mkubwa inabidi matukio yote ya burudani yasitishwe hadi baada ya maombolezo.
 

Baada ya Tukio la MV Bukoba katika ziwa VICTORIA na kama idadi ya watu wanaohofiwa kupoteza maisha ikawa hiyo inayodhaniwa kati ya 1500 - 2000 itakuwa ni ajali ya majini kubwa kuliko zote katika historia ya Taifa hili. Huu ni msiba usioelezeka (endapo idadi itakuwa hiyo ama kuvuka)

Kwa mintarafu hiyo Uncle Lundenga na Ndugu yangu George Rwehumbiza hamna sababu yoyote ya kuwaweka Watanzania pale Mlimani City wakimkufuru Mungu huku wengine wanaomboleza. Najua mnaweza kutia pamba masikio na mkaamua kuobserve silence kwa dakika 1, lakini dhambi hii haitawatoka kamwe kama mtapuuza maono haya.

Kama kawaida yetu tutasema unajua tumekodi na kulipa gharama kubwa kwa wataalam kutoka maeneo mbalimbali ndani na Nje ya Tanzania kwa hiyo hatuwezi kupoteza fedha hizi na hakuna wa kuzilipa tena kuandaa Tamasha, Aaah nyie watu hizi fedha za nani kama si wauza vitumbua na karanga wa msata hadi mahenge ambao hawalali wakikesha kutuma meseji na kushiriki bahati nasibu wasiyoshinda hata siku moja huku shilingi zao zikiteketea kama fupa katika domo la fisi.

Ndugu zetu wapendwa wa VODACOM na LINO AGENCY INTERNATIONAL kaeni meza moja na mtafakari hili msiba huu leo ni mkubwa kwa Taifa, hatuna haja ya kusherekea kupitia matangazo ya LIVE katika Luninga kwa mabinti zetu kupita wakiwa Nusu Uchi huku mamia ya ndugu zao bado wapo majini miili yao ikiwa inasakwa na huzuni kubwa imeligubika Taifa.

Kila jambo ni mapenzi ya Mungu na kwa moyo wa Unyenyekevu kabisa natoa pole kwa familia zilizoguswa na msiba huu kwa niaba ya wana JF wenzangu.

Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa...Jina lake lihimidiwe

Ina lilah waina ilaih rajuun

View attachment 36955

Kaka Mkubwa amerejea katikati ya Sintofahamu Nyingi...Inakadiriwa waliopoteza maisha ni 192 kwa mujibu wa REUTERS, Zanzibar Yatangaza Maombolezo ya Siku 3, BLOG ZOTE ZASUSIA Highlight za Tamasha ambazo miaka yote hutoa dondoo za awali...MOYO WA UZALENDO (MICHUZI, Sufiani Mafoto, Full Shangwe, G Sengo na Wengine)


ADIOS
mzee wa magogoni kachukia ajali imemkatishia miadi yake.
 
Back
Top Bottom