Ajali ya Meli: Maoni na mtazamo wa wananchi kwa yaliyojiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali ya Meli: Maoni na mtazamo wa wananchi kwa yaliyojiri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GHOST RYDER, Sep 10, 2011.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135

  Baada ya Tukio la MV Bukoba katika ziwa VICTORIA na kama idadi ya watu wanaohofiwa kupoteza maisha ikawa hiyo inayodhaniwa kati ya 1500 - 2000 itakuwa ni ajali ya majini kubwa kuliko zote katika historia ya Taifa hili. Huu ni msiba usioelezeka (endapo idadi itakuwa hiyo ama kuvuka)

  Kwa mintarafu hiyo Uncle Lundenga na Ndugu yangu George Rwehumbiza hamna sababu yoyote ya kuwaweka Watanzania pale Mlimani City wakimkufuru Mungu huku wengine wanaomboleza. Najua mnaweza kutia pamba masikio na mkaamua kuobserve silence kwa dakika 1, lakini dhambi hii haitawatoka kamwe kama mtapuuza maono haya.

  Kama kawaida yetu tutasema unajua tumekodi na kulipa gharama kubwa kwa wataalam kutoka maeneo mbalimbali ndani na Nje ya Tanzania kwa hiyo hatuwezi kupoteza fedha hizi na hakuna wa kuzilipa tena kuandaa Tamasha, Aaah nyie watu hizi fedha za nani kama si wauza vitumbua na karanga wa msata hadi mahenge ambao hawalali wakikesha kutuma meseji na kushiriki bahati nasibu wasiyoshinda hata siku moja huku shilingi zao zikiteketea kama fupa katika domo la fisi.

  Ndugu zetu wapendwa wa VODACOM na LINO AGENCY INTERNATIONAL kaeni meza moja na mtafakari hili msiba huu leo ni mkubwa kwa Taifa, hatuna haja ya kusherekea kupitia matangazo ya LIVE katika Luninga kwa mabinti zetu kupita wakiwa Nusu Uchi huku mamia ya ndugu zao bado wapo majini miili yao ikiwa inasakwa na huzuni kubwa imeligubika Taifa.

  Kila jambo ni mapenzi ya Mungu na kwa moyo wa Unyenyekevu kabisa natoa pole kwa familia zilizoguswa na msiba huu kwa niaba ya wana JF wenzangu.

  Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa...Jina lake lihimidiwe

  Ina lilah waina ilaih rajuun

  sfsf.jpg

  Kaka Mkubwa amerejea katikati ya Sintofahamu Nyingi...Inakadiriwa waliopoteza maisha ni 192 kwa mujibu wa REUTERS, Zanzibar Yatangaza Maombolezo ya Siku 3, BLOG ZOTE ZASUSIA Highlight za Tamasha ambazo miaka yote hutoa dondoo za awali...MOYO WA UZALENDO (MICHUZI, Sufiani Mafoto, Full Shangwe, G Sengo na Wengine)


  ADIOS
   
 2. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Nilikuwa sina taarifa hii naangalia news CNN nikaona wanabreak news about Tanzania nikaona niweke TV ya Taifa, nakutana na watoto wanaimba kwaya

  Hivi hii TV ya taifa inayoendeshwa na my PAYE ina faida gani jamani ?

  Poleni wafiwa, its national mourning and I hope the pageant(sp) will be postponed
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Tumefiwa na wapendwa wetu kweli ila shughuli zingine ni lazima ziendelee. Maisha ni lazima yasonge mbele.
   
 4. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 3,999
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Hii kitu ukiitazama kwa juu ni kama iko pouwa tu..ila ukiitazama kwa undani ni kama unaweza kushangaa
  Usiku wa jana ...huko Zanzibar au Tanzania Visiwani..wamepatwa na msiba mkubwa sana..wakupoteza watu wengi kwa ajari ya meli

  Leo jumamosi..Tanzania Bara tunafanya shindano kubwa la urembo ..Vodacom Miss Tanzania..kumbuka Miss Tanzania haina mshiriki toka Zanznibar(Tanzania Visiwani)...

  Je hii haiwezi kuzua mjadala...kwa wazanzibari

  Ni wangu mtazamo
   
 5. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #5
  Sep 10, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Wakuu nimestaajabishwa sana na hili hasa kwa upande wa TV stations ikiwa za nje zimeweza kuujuza ulimwengu kwanini TV stations zetu hawana updates/wamechelewa kutuletea updates zaidi ya kutuonyesha cartoons na maandishi kupita kwa chini? Au wapo busy na Miss Tanzania? Inasikitisha sana.
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Sep 10, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Kama wana busara wataahirisha hayo mashindano yao ya umiss..
   
 7. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #7
  Sep 10, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Zanzibar ni wilaya ndani ya JMT.Zipo wilaya nyingi ambazo hazina uwakilishi kwenye mashindano ya Miss Tanzania Zanzibar ni mojawapo wa wilaya zilizokosa uwakilishi nini cha ajabu !.

   
 8. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #8
  Sep 10, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Meli iliyozama Zanzibar
   
 9. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #9
  Sep 10, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 3,999
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  mkuu Ngongo umeua kabisa...kwahiyo sio kesi wao kukosa mwakilishi miss tanzania...hahahahahaahaha..twende tukawape pole..
  na pia Invisible atoe taarifa ya rambi rambi kwa msiba huo..kwa niaba ya wanajf wote
   
 10. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #10
  Sep 10, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 3,999
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  shossi ..unazungumzia hizi media zetu makanjanja?....mie natoka pale itv saa hz ndio wanapeleka mtu znz...mpk arudi Aljazeera washamaliza kila kitu katika habari...wacha tu subiri saa mbili tuliyozea
   
 11. yegella

  yegella JF-Expert Member

  #11
  Sep 10, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  wanasubiri maelekezo wasema watu wangapi wamekufa.....
   
 12. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #12
  Sep 10, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hakika isipohairishwa leo kweli VODACOM japo hakuna sehemu yoyote wanafungwa kwa hilo lakini kama wanajali wanuwezo mkubwa sana kuhairishwa tamasha hilo [Event].

  Ni kwa faida yao na kwa jamii kuwa wanajali na kuwa wao ni sehemu ya Watanzania kama corporate social responsibility kwao kuwa wanajuha kuwa jamii ya Watanzania leo imeondokewa na mamia ya Watanzania kwa ajali ya Meli huko Zanzanzibar.

  Kwenye mikataba yao na makampuni waliyo outsource shughuri hiyo nadhani kuna vipengele vya demage caused by nature disaster.[Force M] wanaweza kutumia kuhairisha kwa muda.

  Nia kwa nia njema ya kutengenezaa positive impression juu ya macho ya Watanzania na kuonyesha kuwa mnajali hata wakati wa matatizo nyie ni sehmu ya jamii.
   
 13. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #13
  Sep 10, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Tumekwisha
   
 14. Avatar

  Avatar JF Gold Member

  #14
  Sep 10, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 676
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 35
  Siungi mkono hoja!
   
 15. p

  plawala JF-Expert Member

  #15
  Sep 10, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inategemea ukubwa wa msiba au janga mkuu
  Kupoteza watu zaidi ya 200(idadi kamili bado kuthibitishwa?) siyo msiba mdogo
   
 16. m

  mozze Senior Member

  #16
  Sep 10, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 185
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa nasoma habari ya ajali ya kuzama meli huko Unguja na Pemba, BBC kama tulivyo watanzania wengi nao wameshindwa kuelezea ajali ilipotokea.
  Habari yao inachanganya na kuibua maswali Tanzania ni nchi gani? Je Zanzibar ni Nchi au Kisiwa? Je Pemba ni sehemu ya Zanzibar? Unguja ni wapi kwenye ramani ya dunia?
  Angalia hii habari na ramani iliyowekwa na BBC BBC News - Zanzibar ferry disaster: Scores die, many more missing.
  nadhani tunahitaji kuweka mambo clear kutambua nchi zinazotengegeza muungano wa Tanzania.
   
 17. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #17
  Sep 10, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 3,999
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  sasa wakisubiri taarifa ya polisi..watakuwa wameenda kutafuta habari au kuchukua habari?...media zetu bana..uwiiiiii
   
 18. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #18
  Sep 10, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Shossi vyombo vyetu vya habari ikifika usiku sisi tukilala navyo vinalala vinaamka saa 12 asubuhi.
   
 19. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #19
  Sep 10, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Umeongea maneno ya msingi na yenye ukweli usiopingika tena wanatuona mafala wote wanatukusanya saa mbili usiku tunakuwa wajingaaa tukiahamishahamisha stations
   
 20. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #20
  Sep 10, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Rafiki yangu yeye hakujizuia hisia yake amesema kwenye facebook
  [h=6]Saleh Mahdi

  kama mzanzibari sitaitazama tena TBC kwa upuuzi waliotuonesha yaani watu wako na huzuni eti wao wanaonesha katuni na kila mzanzibari mwenye uchungu na nduguzetu walopotea lazma itawagusa allah awape jannah waliokufa shahid baharini[/h]
   
Loading...