Ajali ya Meli: Maoni na mtazamo wa wananchi kwa yaliyojiri

Media zetu zinakua legelege kama serikali yetu je ktk hili tutaendelea kweli labda mungu ashushe baraka zake tu
 
Mungu awarehemu marehem wote nadhani Uncle Lunde na VTL wataliangalia hili kwa uzito mkubwa. Mkwele yeye nae atatulia hapa nyumbani?
 
[h=6]according to the official news till the moment, 338 people survived, while 160 people died from the accident that saw mv.spice (ship) sunk around nungwi in zanzibar !! Yet an investigation goes on. What a sad day !! Let's pray for the dead people and hope safety for all.[/h]
 
Nadhani watakuwa busy kufuatilia kwa karibu vyama vya CCM na Chadema vikifuana kwenye uchaguzi mdogo wa Igunga
 
Endelea kushabikia Moto kwa Jirani huku kwako nako kunafuka MOSHI. Unaingiza propaganda za Jukwaa la Siasa kwenye maisha ya Watu na Msiba mkubwa kama huu?

Hakuna ushabiki hapa. Hakuna kipimo cha msiba mkubwa. Wanaweza wakafa watu 100 isiniume sana kama akifa mtu mmoja anayenihusu. Wasimame dk 1 kuwakumbuka binadamu wenzetu waliopoteza maisha, basi inatosha.

Mwenye uchungu atakaa nyumbani
hataenda Miss Tanzania. Kwani VODA watawafuata watu majumbani kwao kuwalazimisha? Wache wasio na uchungu (na sio kosa) waendelee na maisha.

Iko siku na wao watakua na machungu yao, na wewe wakati huo utakua kwenye furaha fulani. Haya ndo maisha ndugu yangu. Dunia haisimami hata mkifa treni nzima
 
Wakuu nimestaajabishwa sana na hili hasa kwa upande wa TV stations ikiwa za nje zimeweza kuujuza ulimwengu kwanini TV stations zetu hawana updates/wamechelewa kutuletea updates zaidi ya kutuonyesha cartoons na maandishi kupita kwa chini? Au wapo busy na Miss Tanzania? Inasikitisha sana.

Mku hapa nipo naangali tbc lakini hawana mpango wowote wa kutuletea taarifa,kuna kipindi cha taarabu inaendelea
 
Jamani mbona kuna watu mna kauli chafu na misiba ya wenzenu namna hiyo!? Mambo ya muungano na siasa mnaingiza kwenye misiba hebu acheni masikhara nyinyi nadhani sasa kwenye hili jukwaa mmeingia kimakosa.
 
Nakumbuka MV Bukoba bendera ilishushwa nusu mlingoti na TV zilionyesha vipindi vya live japo kuwasiliana kwa simu na eneo latukio. Hii ya Zanzibar imechukuliwa poa na vyombo vyetu vya habari mfano leo vyombo vyetu asubuhi wakionyesha katuni BBC na Al Jazeera walikuwa wakitoa exclusive news kutoka eneo la tukio inasikitisha sana wakuu.
 
wasisimamishe ila wafanye maombelezo kwa mda mfupi then waendelee yameshatokea teyari kusimamisha shughili zingine ni kuongeza matatizo...
 
Mashindano yaendelee tu. Zanzibar ni nchi ya ng'ambo haituhusu. Mambo ya Wazanzibar tuwaachie wenyewe kama tunavyowaachia Washelisheli mambo yao.
 
Zanzibar ni majiran wa tanganyika kama ilivyo rwanda, kenya na uganda. 2004 abanyagwanda walichinjana na kilisha samaki wetu wa mto kagera na watanzania waliendelea kucheza kiduku. Kenya-after erection riots zilizalisha maiti nyingi wakati wa TZ wakiendelea kunya kahawa-zanzibar siyo tanzania.
duh....edit basi post yako kidogo
 
Kwa kweli ni jambo la msingi kuhuzunika na wenzetu ambao msiba huu umewagusa moja kwa moja kwa kupoteza ndugu wa damu au wa karibu sana. Natoa rambirambi zangu katika hilo.

Lakini swala la kuhairisha shughuli zingine kwa tukio hilo tu inabidi litazamwe kwa jicho la tatu kuliko kulijadili kwa jazba. Tuangalie tumejiandaaje kushiriki huzuni hiyo, je tutawafariji vipi wafiwa....tukihairisha tutapata wasaa wa kushiriki nao hata kwa kutuma rambirambi au tunahairisha tu....! hilo ni moja, La pili Watanzania tujenge hoja katika kujadili jambo kuliko kutoa lawama tu kwa mtoa hoja..kila mtu ana uhuru wa kuwasilisha mawazo yake!
 
Baada ya Tukio la MV Bukoba katika ziwa VICTORIA na kama idadi ya watu wanaohofiwa kupoteza maisha ikawa hiyo inayodhaniwa kati ya 1500 - 2000 itakuwa ni ajali ya majini kubwa kuliko zote katika historia ya Taifa hili. Huu ni msiba usioelezeka (endapo idadi itakuwa hiyo ama kuvuka)

Kwa mintarafu hiyo Uncle Lundenga na Ndugu yangu George Rwehumbiza hamna sababu yoyote ya kuwaweka Watanzania pale Mlimani City wakimkufuru Mungu huku wengine wanaomboleza. Najua mnaweza kutia pamba masikio na mkaamua kuobserve silence kwa dakika 1, lakini dhambi hii haitawatoka kamwe kama mtapuuza maono haya.

Kama kawaida yetu tutasema unajua tumekodi na kulipa gharama kubwa kwa wataalam kutoka maeneo mbalimbali ndani na Nje ya Tanzania kwa hiyo hatuwezi kupoteza fedha hizi na hakuna wa kuzilipa tena kuandaa Tamasha, Aaah nyie watu hizi fedha za nani kama si wauza vitumbua na karanga wa msata hadi mahenge ambao hawalali wakikesha kutuma meseji na kushiriki bahati nasibu wasiyoshinda hata siku moja huku shilingi zao zikiteketea kama fupa katika domo la fisi.

Ndugu zetu wapendwa wa VODACOM na LINO AGENCY INTERNATIONAL kaeni meza moja na mtafakari hili msiba huu leo ni mkubwa kwa Taifa, hatuna haja ya kusherekea kupitia matangazo ya LIVE katika Luninga kwa mabinti zetu kupita wakiwa Nusu Uchi huku mamia ya ndugu zao bado wapo majini miili yao ikiwa inasakwa na huzuni kubwa imeligubika Taifa.

Kila jambo ni mapenzi ya Mungu na kwa moyo wa Unyenyekevu kabisa natoa pole kwa familia zilizoguswa na msiba huu kwa niaba ya wana JF wenzangu.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa...Jina lake lihimidiwe
Ina lilah waina ilaih rajuun

Kuna watu kula yao ya kesho inategemea shindano hilo, kuna watoto ili j3 waende shule inategemea shindano hilo kufanyika, kuna wagonjwa wapo mahospitalini ili watibiwe haraka wanategemea shindano hilo,kuna mambo mengi mengi yayotegemea shindano hilo ili yaendelee kufanyika.

Uzembe wa watu wachache usilifanye taifa kufa ganzi na kusitisha mtiririko wote wa shughuli za kawaida za maendeleo. Hizo norms ndio zimelifikisha taifa hili hapa tulipo (choka mbaya).tuendelee kuwafariji wote ndugu, jamaa na marafiki wa karibu wa waliokufa lakini shughuli za kibiashara tuache ziendelee

I sympathize with all who have lost their love ones.
 
Muungano una lega lega ukitaka ukweli kamuulize waziri wa zamani wa Zanzibar katika utawala uliopita, aliyekuwa na dhamana ya wizara zote Mh Hamid
 
Back
Top Bottom