Ajali za Kisiasa za kutengenezeana zinavyoua ndoto za Viongozi wetu bora

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
20240217_203925.jpg


๐Ÿ™๐Ÿฟ Neno "AJALI" limetumika sana tangu Lowassa afariki.

๐Ÿ™๐Ÿฟ Neno hilo limetumika kuelezea majanga ya kutengenezwa yaliyomkuta Lowassa.

๐Ÿ™๐Ÿฟ Kwa mujibu wa Raphael Chegeni, ajali hizo ndizo zilizoharakisha kifo cha Lowassa.

๐Ÿ™๐Ÿฟ Kilichomsononesha zaidi Lowassa ni kuwa ajali hizo zilitengenezwa na waliovaa ngozi ya Urafiki.

๐Ÿ™๐Ÿฟ Ajali kubwa zaidi ni ile ya Mwaka 2008 iliyogharimu nafasi yake ya Uwaziri Mkuu.

๐Ÿ™๐Ÿฟ Mtengenezaji wa ajali hiyo hatimaye amejulikana wakati wa msiba wa Lowassa

๐Ÿ™๐Ÿฟ Licha ya kujinasibu kuwa "Rafiki Mkubwa" wa Lowassa, siyo ndugu au rafiki yeyote wa Lowassa aliyetamka kuwa Mheshimiwa huyo alishiriki kwenye kumuuguza au kuifariji familia.

๐Ÿ™๐Ÿฟ Hakuna hotuba yeyote iliyoonesha ukaribu wa Mheshimiwa huyo na Hayati Lowassa.

๐Ÿ™๐Ÿฟ Hata yeye mwenyewe wakati wa kuaga mwili wa Lowassa hakupeana mkono wala kuzungumza na mwanafamilia yeyote wa Lowassa.

๐Ÿ™๐Ÿฟ Pale Masaki hakuingia ndani kuwapa pole wafiwa baada ya kusaini kitabu cha maombolezo.

๐Ÿ™๐Ÿฟ Pale Monduli, wengine walienda kuiaga familia kwa ukaribu, yeye akapotea kama mvuke.

๐Ÿ™๐Ÿฟ Neno letu kwa watengeneza ajali wote: Acheni tabia hiyo chafu.

๐Ÿ™๐ŸฟMnatupora viongozi wetu na mnasononesha mioyo ya watu na kuacha mama zetu Wajane.

๐Ÿ™๐Ÿฟ Msipoacha mtakufa KIBUDU

LALA SALAMA SHUJAA. TUTAONANA BAADAE
 
Hivi kweli hakuingia ndani kumpa pole mjana wa Lowasa aseee....jamani then akakimbilia press kusema akikuwa nae karibu baada ya ile ajali ....wanafiki sio watu kabisaa
 
Tutakukumbuka yake king crazy GK anasema nenda nasi ipo sipo siku tutafata kila nafsi itaonja mauti Mwenyezi Mungu atujalie mwisho mwema
 
Usiongozwe sana na hisia na kuongea huko kana kwamba una ukweli wowote kuhusu jambo hilo,mie kwangu atabaki kuwa rais bora sana kutokea kwani ni baba wa demokrasia haswaa hapa kwetu Tanzania.Na siku zote mkubwa ni jalala kila baya litokeapo lazima atanyoshewa kidole na hao binadamu waliomzunguka,Hata sifa anazopewa mwenda zake shughuli kubwa alikuwa anafanya boss wake kupitia baraka zake.Elewa kuwa boss wake ndio alikuwa msimamizi mkuu wa rasilimali zetu za Taifa na ndio alikuwa anajua kipaumbele ni kipi kwa wakati huo.Waziri mkuu hana maamuzi kuhusu mambo ya fedha yeye ni mshauri tu na kiongozi mkuu wa shughuli za kila siku.MMESEMA MENGI SANA KUHUSU YEYE NA HATUJAWAHI KUSIKIA AKIJIBISHANA NA MTU YEYOTE SIO KWAMBA HAONI WALA HASIKII,ANASIKIA SANA NA ANAONA SANA TENA SANA.USIJIFICHE HAPA JF NA KUONGEA MAMBO AMBAYO HUNA USHAHIDI ACHANA KABISA NA MAMBO YA KUSIKISIKIA KAMA UNATAKA KUONGEA JITOKEZE HADHARANI UONGEE KILA MTANZANIA AKUSIKIE,LONG LIVE THE FORMER PRESIDENT.
 
Wacheni ujinga na unafiki, Leo Lowasa katangulia WOTE tunampaka maradhi na kumfukiza Udi. Tuache unafiki. Lowasa alikuwa KIONGOZI mzuri lakini alikuwa na makandondo yake.

1. Lowasa Akipokuwa PM, alikuwa mla Rushwa Mkubwa Sana hata akapewa jina la MR 10%.
2. Aliuwa watu KISIASA haswa wake waliotaka kuingilia siasa zake za ufalme wake WA Monduli
3. Amepora Ardhi nyingi Sana za watu , wanavijiji na hata Ardhi ya Serekali. MFANO: kapataje hiyo Ranch ya huko Tanga, Ardhi zote za Arusha Mini anazimiliki yeye na Familia Take. Yeye ndiye mmiliki mkubwa WA Ardhi Arusha na Manyara
4. Ushirika WA yeye na Mheshimiwa Rostam Aziz unahutaji Magnifying Glass, haswa walivyoipata share za VODACOM.
5. Richmond Inamhusu Sana Lowasa, Rostam na grange Lao, ushahidi uko wazi na ulikuwepo Wizara ya Nishati.

Kuna mengi yake Marehemu Mazuri, lakini hakuwa msafi hata kidogo, na tuache huu ujinga WA kutaka kuifanya yeye alikuwa Malaika pekee. WENGI LEO WANAUTUMIA MSIBA WAKE KAMA KETE YA KISIASA, NA PIA KUTUMIA FURSA KUWADHALILISHA WENZAO KUWA WALIMTENDEA MABAYA LOWASA, ULA WAO NDIO WAZURI, SIASA ZA KUPAKANA MAVI
 
hata Uhuru Kenyata alipiganiwa sana na William Ruto na akaja kumpa Umakamu wa Rais

akamgundua ni zaid ya Mwizi na ni mtu anaemzunguka

Uhuru akashindwa kumchomoa haraka kwny system kama alivyofanya JK kwa Lowasa

wakati wa Uchaguzi kaambulia mabua kwa kuwa hakufanya kama alivyofanya Jakaya

Lowassa angeachwa kwny u PM hadi 2015 ingekuwa kazi sana kumchomoa

Fundi, Guru, Mwamba wa Siasa hizi anapatikana kijiji cha Msoga Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Nchini Tanzania

kawaacha watu wanahonga watu kwa miaka 10 wakateketeza hadi majumba kwa kuuza ili ku Finance Uchaguzi halafu wakaambulia patupu unadhan watakufurahia wao na wapambe wao?

'Urais sio Uji wa kila anaetaka kuramba analamba โ€ฆwa Makadara alambe, wa Bwejuu alambe, wa Mtambwe alambe '-Dr Salmeen Amour Juma Rais wa Zanzibar wa awamu ya tano
 
Mara nyingine heri lawama kuliko fedheha. Ukute msogaboy aliona mbali ndio mana akaamua kukubali Kuja bebeshwa lawama hizi zote kuliko fedheha zaidi.
You never know tungekua wapi sasa hivi. Bora uendelee tu kumlaumu.
 
Mara nyingine heri lawama kuliko fedheha. Ukute msogaboy aliona mbali ndio mana akaamua kukubali Kuja bebeshwa lawama hizi zote kuliko fedheha zaidi.
You never know tungekua wapi sasa hivi. Bora uendelee tu kumlaumu.
Bora lawama kuliko fedheha

na Chadema nao wanalalamika Jk kumkata Lowassa kwny mchujo ndani ya CCM โ€ฆhadi unajiuliza hawa wapo serious kweli kufanya Siasa?
 
Mara nyingine heri lawama kuliko fedheha. Ukute msogaboy aliona mbali ndio mana akaamua kukubali Kuja bebeshwa lawama hizi zote kuliko fedheha zaidi.
You never know tungekua wapi sasa hivi. Bora uendelee tu kumlaumu.
JK is a master. That cant be denied.
Mleta mada na wenzie ni kundi tu la wanafiki wanao amua ku trend na upepo wa marehemu. Hawana lolote wanalolijua kwa undanj kuhusu uhusiano wa Lowasa na JK
 
Bora lawama kuliko fedheha

na Chadema nao wanalalamika Jk kumkata Lowassa kwny mchujo ndani ya CCM โ€ฆhadi unajiuliza hawa wapo serious kweli kufanya Siasa?
Forget about us chadema, tumekua wajinga wajinga tu tusiojua hata ajenda ipi ya kushikilia kwasasa
 
Hivi kweli hakuingia ndani kumpa pole mjana wa Lowasa aseee....jamani then akakimbilia press kusema akikuwa nae karibu baada ya ile ajali ....wanafiki sio watu kabisaa
'โ€ฆMimi na Jakaya hatujakutana barabarani โ€ฆ' Edo
 
Mara nyingine heri lawama kuliko fedheha. Ukute msogaboy aliona mbali ndio mana akaamua kukubali Kuja bebeshwa lawama hizi zote kuliko fedheha zaidi.
You never know tungekua wapi sasa hivi. Bora uendelee tu kumlaumu.

Kinyume chake pia ni sahihi! Muhimu ni kuacha kufanya maagano ambayo unaona huwezi kuasimamia.

Yaani kuwacha unafiki. Sio wewe unataka usaidiwe ufanikiwe ila hutaki kurejesha.
 
Povu la nini? Kama wewe umeamua kuandika upande mmoja wa shilingi acha na wenzako waandike upande wa pili. By the way edward aliumizwa sana tu kisiasa na rafiki yake wa karibu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom