Ajali ya Meli: Maoni na mtazamo wa wananchi kwa yaliyojiri


Baada ya Tukio la MV Bukoba katika ziwa VICTORIA na kama idadi ya watu wanaohofiwa kupoteza maisha ikawa hiyo inayodhaniwa kati ya 1500 - 2000 itakuwa ni ajali ya majini kubwa kuliko zote katika historia ya Taifa hili. Huu ni msiba usioelezeka (endapo idadi itakuwa hiyo ama kuvuka)

Kwa mintarafu hiyo Uncle Lundenga na Ndugu yangu George Rwehumbiza hamna sababu yoyote ya kuwaweka Watanzania pale Mlimani City wakimkufuru Mungu huku wengine wanaomboleza. Najua mnaweza kutia pamba masikio na mkaamua kuobserve silence kwa dakika 1, lakini dhambi hii haitawatoka kamwe kama mtapuuza maono haya.

Kama kawaida yetu tutasema unajua tumekodi na kulipa gharama kubwa kwa wataalam kutoka maeneo mbalimbali ndani na Nje ya Tanzania kwa hiyo hatuwezi kupoteza fedha hizi na hakuna wa kuzilipa tena kuandaa Tamasha, Aaah nyie watu hizi fedha za nani kama si wauza vitumbua na karanga wa msata hadi mahenge ambao hawalali wakikesha kutuma meseji na kushiriki bahati nasibu wasiyoshinda hata siku moja huku shilingi zao zikiteketea kama fupa katika domo la fisi.

Ndugu zetu wapendwa wa VODACOM na LINO AGENCY INTERNATIONAL kaeni meza moja na mtafakari hili msiba huu leo ni mkubwa kwa Taifa, hatuna haja ya kusherekea kupitia matangazo ya LIVE katika Luninga kwa mabinti zetu kupita wakiwa Nusu Uchi huku mamia ya ndugu zao bado wapo majini miili yao ikiwa inasakwa na huzuni kubwa imeligubika Taifa.

Kila jambo ni mapenzi ya Mungu na kwa moyo wa Unyenyekevu kabisa natoa pole kwa familia zilizoguswa na msiba huu kwa niaba ya wana JF wenzangu.

Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa...Jina lake lihimidiwe

Ina lilah waina ilaih rajuun


ADIOS

Basically,hili shindano lenyewe ni laana tu,uwa nashangaa watu wanasababu nyingi tena za msingi kutetea uchafu huu,wengine watakwambia kuwa tunatangaza utamaduni? Je,utamaduni wetu ni kuvaa machupi na kuacha matiti wazi? wengine watakwambia ni ajira kwa vijana,Je,hao wasichana wakitoka hapo uwa wanafanya nini? kama sio upuuzi wa akina Wema Sepetu na umalaya wake....Hili shindano ni la kuzalilisha dada zetu na mama zetu....na kwa hakika dhambi hii itamla huyu Hashim Lundenga...kazi yake ya kuwaanika dada zetu kwa mabedeshee ili wanunulike si haki na wala halipaswi kuvumilika kabisa na kila mtu anayemuheshimu Allah(Mungu).....Huyu jamaa anakusanya mabilioni kupitia kuwaweka uchi dada zetu....MIMI NAUNGA MKONO HOJA KUWA HILI SHINDANO LIFUTWE KABISA NA SIO KUHARISHA KWASABABU YA VIFO VYA WENZETU KULE ZENJI.....

Mungu awatie nguvu wafiwa,maana kifo ni jambo lisilozoeleka...
 
katika janga kama hili la msiba mkubwa wa kitaifa tuache malumbano ya kisiasa.poleni ndugu zetu wote mliofiwa na mlio majeruhi.
Uchunguzi wa kina na wazi ufanyike ili kama ni uzembe wawajibishwe wahusika
 
Ukweli unabakia kuwa Zanzibar siyo Tanganyika. Hizi ni nchi mbili majirani. Period
 
Kawaida mtu akilia huwa anashika kichwa chake. Hashiki cha mwenzake! Ni kama usemi huu umedhihiri vile! Poleni wafiwa.
 
Siungi mkono hoja ya kuahirisha mashindano hayo kwa sababu ya hii ajali, kwa sababu kwanza mashindano yenyewe yako kibiashara zaidi kuliko kitaifa kwani sidhani kama kuna mkono wa serikali ktk mashindano hayo, na bahati nzuri hakuna hata mshiriki mmoja anayetokea Zenji kiasi tungesema hatendewi haki.

Labda niulize swali kwa mtoa maada na wengine walioungana naye mkono, kama kusingetokea msiba wangeenda? Ili tuone kwamba mashindano watayamiss kwa sababu hiyo, hivyo wanaomba iahirishwe ili wapate nafasi ya kushiriki.

Kuahirisha hii ni sawa na kusema night clubs, discos na shughuli zote za starehe zisimamishwe.
 
Nilikuwa nasoma habari ya ajali ya kuzama meli huko Unguja na Pemba, BBC kama tulivyo watanzania wengi nao wameshindwa kuelezea ajali ilipotokea.
Habari yao inachanganya na kuibua maswali Tanzania ni nchi gani? Je Zanzibar ni Nchi au Kisiwa? Je Pemba ni sehemu ya Zanzibar? Unguja ni wapi kwenye ramani ya dunia?
Angalia hii habari na ramani iliyowekwa na BBC BBC News - Zanzibar ferry disaster: Scores die, many more missing.
nadhani tunahitaji kuweka mambo clear kutambua nchi zinazotengegeza muungano wa Tanzania.

Ni ramani sio tamani mkuu,hata hivyo hiyo ramani iko wazi Mozze.Na hata wao wameonyesha vyema.
 
@dar_millionaire Yeah i agree with u , ur mom dies you just stop by and say 'pole' to your father then you take your wife go partying !after all she is your dady wife so what the heck! ARE YOU REAL?
 
Nini watu mi hata paka mzururaji akigongwa na gari nahisi uchungu usiniambie binadamu wenzangu kadhaa wankufa kifo kikatili cha maji! have a heart!
 
Nimetafakari sana siku ya Leo, sana tena sana, Jibu ninalolipata ni kuwa CCM ina Laaana ya Mungu,na wakiendelea hivi,sie tutabeba sana Msalaba wao, Kwa sisi wa Kristo tunaamini kuwa kuna Dhambi ambayo walifanya Adam na Eve na mpaka sasa inatu cost (Kifo).
CCM Walipoingia Igunga majuma kadhaa tumeshuhudia Kifo cha mtoto wetu mpendwa kule, Leo hii CCM wanazindua kampeni zao Tumeshuhudia Ndugu zetu wa Zanzibar/Bara wakipata ajali mbaya baharini,
Hizi ni Laana ambazo ni matunda ya Dhambi za CCM,ni jukumu letu sasa, Mungu emetufungua, tusimame na kulipiga vita Dudu CCM, na tuanze na Igunga.

Mungu tubariki Tanzania kwa Kutuondoshea Dudu CCM.
 
katika janga kama hili la msiba mkubwa wa kitaifa tuache malumbano ya kisiasa.poleni ndugu zetu wote mliofiwa na mlio majeruhi...
Ukiuona mambo uliyoyaita "ya kisiasa" kuhusu Muungano yanaibuka hata msibani ujue huo Muungano uko kwenye crisis, una saratani.

Hivi nani yukoultimately responsible kuratibu msiba/misaada katika maafa haya, Rais wa Zanzibar au Kikwete? Manake Shein hawezi kukubali Kikwete kufunikwa na Kikwete ndani ya visiwa wakati watu wake wamekumbwa na janga kubwa, akikubali mnyela na Zanzibar si nchi na haina Rais, hata wakati wa janga la nchi. Na Kikwete hawezi kwenda Zanzibar akafanywa second fiddle wa Shein, yeye ni Rais wa nchi inayoeleweka duniani kwamba ni nchi. Ndio maana hakuna kiongozi yeyote wa Bara amekwenda kwenye tukio mpaka hivi sasa. Muungano umekorogwa korogwa tu kama udongo wa mfinyanzi.
 
Muungano gani wa kulazimisha?? nani anayeuhitaji? si wao wala sisi. may be ni viongozi wachache wa CCM ndo wanaumind
 
Hii kitu ukiitazama kwa juu ni kama iko pouwa tu..ila ukiitazama kwa undani ni kama unaweza kushangaa
Usiku wa jana ...huko Zanzibar au Tanzania Visiwani..wamepatwa na msiba mkubwa sana..wakupoteza watu wengi kwa ajari ya meli

Leo jumamosi..Tanzania Bara tunafanya shindano kubwa la urembo ..Vodacom Miss Tanzania..kumbuka Miss Tanzania haina mshiriki toka Zanznibar(Tanzania Visiwani)...

Je hii haiwezi kuzua mjadala...kwa wazanzibari

Ni wangu mtazamo
Walahaiwezi kuleta madhara bana japo wanapenda sana kulalamika................ unajua Muungano nikama kiinimaacho si unaona jamaa wahuko wanavyofaidihuku bara lakini waowanachomabaa za wabara
 
<br />
<br />
Mkuu naungana na wewe kushangaa. Vyombo vingi vya habari vime cover hii habari,tena vingine live. Inasemekana zaidi ya watu 100 wamekufa na maiti wamezionyesha.Maskini ya mungu sisi radio na tv toka asubuhi vinapiga mziki na kuonyesha katuni! Hata wenzetu wa nje wanatushangaa kwa kweli.

Je baa zilipochomwa Tv zilifnya nini hasa TVZ
 
haiwezekani kuahirisha. Na si kosa lao. Si kazi ndogo kuandaa tena hiyo kitu. Cha msingi maisha lazima yaendelee
 
Basically,hili shindano lenyewe ni laana tu,uwa nashangaa watu wana sababu nyingi tena za msingi kutetea uchafu huu, wengine watakwambia kuwa tunatangaza utamaduni? Je,utamaduni wetu ni kuvaa machupi na kuacha matiti wazi? W engine watakwambia ni ajira kwa vijana,Je,hao wasichana wakitoka hapo uwa wanafanya nini?

Kama sio upuuzi wa akina Wema Sepetu na umalaya wake....Hili shindano ni la kuzalilisha dada zetu na mama zetu....na kwa hakika dhambi hii itamla huyu Hashim Lundenga...kazi yake ya kuwaanika dada zetu kwa mabedeshee ili wanunulike si haki na wala halipaswi kuvumilika kabisa na kila mtu anayemuheshimu Allah(Mungu).....

Huyu jamaa anakusanya mabilioni kupitia kuwaweka uchi dada zetu....MIMI NAUNGA MKONO HOJA KUWA HILI SHINDANO LIFUTWE KABISA NA SIO KUAiRISHA KWA SABABU YA VIFO VYA WENZETU KULE ZENJI.....

Mungu awatie nguvu wafiwa,maana kifo ni jambo lisilozoeleka...
we unaishi dunia gani? Hata china kwenye sheria kali hawana mawazo kama yako. Ni tatizo la watu wanaofanya kazi serikalini wanaoweza kuwaza kama wewe
 
kwakweli hii ni noma,huku Msiba mkubwa huku Miss Tanzania....Kwakua shetan ametawala nyoyo za watu na hata serikari yetu....utaona tu Miss Tz atapatikana usiku huu wa leo,,ikiwa part ya Tz ina msiba mkubwa....Mungu awalaze mahali pema peponi...ameen.
 
Rais wa Muungano sijui ndo Jk, nimesikia tu ametuma rambirambi za pole. Sijui kama yupo nchi au kaenda kutalii. Mungu awatia nguvu wote waliofikwa na janga hilo.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom