Ajali ya magari ya mizigo imesababisha foleni kubwa ya magari Barabara ya Moshi – Arusha kwa zaidi ya Saa 10

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,177
Reaction score
7,472
WhatsApp Image 2026-01-18 at 13.38.29.jpeg

Kuna magari kadhaa makubwa ya mizigo inadaiwa ni kutoka Rwanda yamepata ajali eneo la Mto Kikafu katika Barabara ya Moshi - Arusha na kufunga njia kwa zaidi ya Saa 10 sasa, kukiwa hakuna mpishano wa magari.

Hali hiyo imesababisha mabasi yasimame kwenye foleni kwa urefu wa zaidi ya Kilometa 20 na inavyoonekana foleni inaweza kuendelea kuwa kubwa zaidi.

Jeshi la Polisi limefika eneo la tukio pamoja na viongozi wengine kadhaa lakini bado hali haijakaa sawa, vyomvo vinavyopita ni Bodaboda tu.

Ni bora Polisi waombe vifaa kutoka makampuni yenye vifaa vya kubeba vitu vizito ili kusogeza pembeni magari yaliyopata ajali kwani foleni inazidi kuwa kubwa na kuharibu ratiba za watu watu wengi.
 
*....na kufunga njia kwa zaidi ya saa 10 sasa.🥺🥺🥺....
 
Waliokuwa wanawahi matibabu, mazishi, interview nk imekula kwao😭
 
Kuna magari kadhaa makubwa ya mizigo inadaiwa ni kutoka Rwanda yamepata ajali eneo la Mto Kikafu katika Barabara ya Moshi - Arusha na kufunga njia kwa zaidi ya Saa 10 sasa, kukiwa hakuna mpishano wa magari.

Hali hiyo imesababisha mabasi yasimame kwenye foleni kwa urefu wa zaidi ya Kilometa 20 na inavyoonekana foleni inaweza kuendelea kuwa kubwa zaidi.

Jeshi la Polisi limefika eneo la tukio pamoja na viongozi wengine kadhaa lakini bado hali haijakaa sawa, vyomvo vinavyopita ni Bodaboda tu.

Ni bora Polisi waombe vifaa kutoka makampuni yenye vifaa vya kubeba vitu vizito ili kusogeza pembeni magari yaliyopata ajali kwani foleni inazidi kuwa kubwa na kuharibu ratiba za watu watu wengi.
Zile helicopter zilizokuwa zinatafuta waandamanaji ziko wapi? Wafike haraka kuongoza watu ili wapishe mitambo kuja kuondoa magari yakiyopata ajali
 
Back
Top Bottom